"Kilimo ni moja kati ya sekta kwenye uchumi inayobeba sana maendeleo kwenye nchi yetu", ni kauli ambayo husikika ikisemwa na watu wengi hususani viongozi wa serikali. Ila kwangu mimi hapo mwanzo niliipinga hii kauli lakini baadaye nikaja kuelewa maana halisi ya hii kauli.
Nakumbuka mara baada ya mimi kumaliza elimu yangu ya shahada ya kwanza na ya pili hapo Chuo kiukuu cha Dar es Salaam mnamo 2016, nilijihisi mwenye mafanikio sana maishani maana yake hii huwa ni ndoto ya watu wengi lakini si wote wanaoweza kufanikiwa kufika pale ambapo nimefika.Basi nyumbani nilifurahiwa na familia yangu ndugu na marafiki zangu wengi na kufanyiwa sherehe kubwa ya ushindi hivyo basi, nilijiona wa thamani kubwa kwenye familia yangu kwani mimi ndo mtoto wa kwanza kwenye familia yetu.
Mikosi ikaanza pale nilipokua natafuta kazi au ajira nilikosa na sikuweza kupata na sio kwamba nilikua sifai bali sehemu nyingi na makampuni mengi nilipoenda kuomba kazi walitoa mishahara midogo na kwa kiwango changu cha elimu nilichonacho kilinifanya nijione sana wa thamani na hapo ndipo nikashindwa kupata kazi.
Mkosi wa pili ulikuja pale ambapo mama yangu alipewa jukumu la kulea watoto wa mke wa pili wa baba yangu kwani baba alifariki miaka ya nyuma huku akiacha mke wa pili na watoto wa tatu wa kiume na mbaya zaidi ni pale yule mke wa pili wa baba alifariki dunia mwaka uliopita hivyo, kufanya mama yangu na huruma yake kuwa mama mlezi wa wale watoto wadogo na hapo ndo nilipoona maisha magumu kwa kuwa matumizi ya vitu yalikuja juu na wale watoto walihitaji elimu bora na kutunzwa vyema kwani " Damu ni nzito kuliko maji".
Hali hii ilinitia hofu na kufanya nichanganyikiwe mno na kukosa amani kwenye maisha na ukiangalia sikuwa na kazi.
Siku moja mama aliniita na kunishauri nijaribu kilimo. Duu! nilipigwa na butwaa na hapo ndipo nilihisi kama kuchanganyikiwa yani mimi na elimu yangu niwe mkulima na nisubirie mazao majira na majira na hela inayokuja sio kubwa.
Nilimbishia sana mama na kumwambia siwezi kujihusisha na kilimo. Kuna rafiki yangu alinishauri na kuniambia kuna kazi itanifaa kwani nina muonekano na utanashati na hilo ni kweli kwani tangu chuo wasichana wengi walinisumbua ila sikuwa nawataka.Kesho yake akanipeleka baa na kunieleza kuwa yeye hupata ela kupitia kutoka na wanawake watu wazima na hapo kichwa kiliniuma nikasema nikapiga moyo konde kwani nilikua na shida na ela kwa hiyo sikuona ubaya sana nikakubali.
Nilipoonyeshwa mwanamke wa kulala naye iyo siku nilishiwa na nguvu kwani nilipomuangalia alilingana sawia na mama yangu na hapo nikaamua kuondoka kwa hasira kwani nilikua nakosea sana hata kama nahitaji sana pesa sikuweza kujaribu kujikosesha heshima na rafiki yangu alinilaumu sana baadae lakini sikujali kwani nilikuwa nimelelewa kwenye misingi ya kikristo na kitendo kama kile ilikuwa ni dhambi kubwa sana ya uasherati, na pengine ningepata magonjwa ya ajabu ya kujitakia.
Mkosi wa tatu niliupata pale nilipoambiwa na mama yangu kwamba anaumwa na hivyo, nilitakiwa kumuuguza na kuwalea wadogo zangu na bili zilikua nyingi kwani hata pensheni ya baba na biashara ya mama hazikuweza kutosha kulea familia yetu basi nikaamua nikakope kwenye kampuni ya mikopo na nilifanikiwa sema sharti nilipe hizo ela baada ya mwaka , la sivyo kila kitu changu maana yake mali za familia yetu zitauzwa.Mkopo ulisaidia sana kwenye ada, chakula na tiba ya mama.
Mara baada mama yangu alipopona aliniuliza ela niliitoa wapi na sikumficha nikamwambia nilikopa, ghafla akaanza kugomba na kunitusi sana kwamba mi mbishi na kuniambia niondoke nyumbani sikuelewa na nikajua anatania ila alimaanisha na kuniambia niondoke mpaka nitakapopata kazi nzuri nirudi hiyo ni kwa kuwa aliogopa sana sitoweza kurudisha deni nililonalo.
Nikaamua kwenda kwa bibi huko Mtwara kupunguza mawazo na nilipofika huko alinikaribisha vizuri na nilifurahi sana. Baada ya muda kuishi na bibi alinishauri kujaribu kuanza kilimo nilikataa na hapo tu punde nilipokea ujumbe kutoka kwa kampuni ya mikopo kwamba nisisahau rejesho ya ela yao maana ilisalia miezi sita hivyo, nikaanza tu kilimo bila kupenda.
Nilikua mvivu mwanzoni lakini nikikumbuka nina deni na bila kulipa familia yangu italala nje. Ikanifanya nijikite na kilimo. Nilijitoa mno kwenye kilimo na kuomba sana kwa Mungu na hapo baadaye nikaja kugundua " Baada ya dhiki ni faraja".
Baada miezi kadhaa kilimo changu cha ufuta na alizeti kilistawi na nikaweza kuuza mazao yangu na kupanua wigo hata kwa kuuza kwa nchi jirani kama Malawi, Zimbabwe, Kenya, Rwanda na Mozambique. Nilifurahi sana kwani nilifanikiwa sana baada ya mwaka mmoja na nikaweza kulipa deni la mkopo, na nimeweza kuisaidia sana familia yangu. Siku moja mama akanikumbusha kuwa hakunifukuza kwa kupenda bali alitaka nijue jinsi maisha yanavyotafutwa na kupambaniwa.
Hivyo, basi nazidi kuwahasa vijana wenzangu kwamba tusichague kazi na kudharau kujiajili na pia hasa wale wanaokidharau kilimo wanapaswa kutoa shukurani kwa wakulima kwani bila juhudi zao hakuna maendeleo nchini.
Kilimo kinapaswa kiendelezwe na kupewa sehemu kubwa ya kuboreshwa na kuwezeshwa ili kutoa michango mikubwa katika jamii yetu.

Upvote
8