Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Pole mkuu aisee, pole sana.
 
Pole sana mkuu
Wakati mwingine mambo hutokea kwa ajili ya kutufunza uvumilivu na ustahimilivu

Nakupongeza pia kwa kufungua moyo wako na kuwa samehe
 
Yeah... That "a" wasn't intentional sio kwamba sijui..
Japo sio rahisi tu kukubali na kuachilia jambo lipite, I'll keep on remorphing myself niwe sawa na mzee wangu.
 
Sawa mkuu nimekuelewa 🙏
 
Ndo maisha kuna kutereza na kunyanyuka tena
 
Ndo maisha kuna kutereza na kunyanyuka
Asante sana mkuu Kwa maneno yenye hekima nitayafanyia kazi kwa nguvu zote
 
Ningekuwa mzee wako ningekutafuta nikupe kipondo kwa huu ujinga ulioandika hapa
 
Najitahidi sana madam...

Usiwe una changanya tabia yangu humu hasa katika drama za hapa na pale, irl niko tofauti kabisa na ni najitahidi kuyaishi yale nayo ya sema...
Sidhani kama nachanganya, bali ni uhalisia ambao hata wewe umeukiri kwenye nyuzi zako mbili nilizosoma.
Kumbe na wewe ni Gen z na sijui.. 😂 Kwa kweli wazazi wetu walijitahidi sana.
Hapana, mie sio gen z. Mie kizee kama ulivyosema.
 
Sidhani kama nachanganya, bali ni uhalisia ambao hata wewe umeukiri kwenye nyuzi zako mbili nilizosoma.

Hapana, mie sio gen z. Mie kizee kama ulivyosema.
Haya kama utaendelea kuamini vile... Nashindwa kukuelewa, hiyo ni zone ya kuchukua kijiji just for fun na wengi wanajua

Kizee wapi wewe mama wa kidijitali?
 
Unamiaka 29 mean umezaliwa 1997.. very yangu bado u mvulana unaye elekea kwenye utu uzima...

Maisha yako na hasira zako zitakufanya usifanikiwe kwenye maisha, Baba yupo sahihi na atakuwa sahihi daima..

Isivyo bahati hujajua kuwa Baba alikuunda hivyo kutokana na makosa ambayo aliyafanya utotoni? Vivyo hvyo ulipaswa kufurahi kuwa Baba amefanya kazi kubwa hata tu kujieleza na kukupa elim hii ameumia sana..


Mpende Baba yako ipende familia yako.. Mungu anasema ukitaka kuwa na maisha marefu waheshim wazazi wako kabisa..


Unataka kufupisha maisha yako kwa kutumia hasira yako ambayo inatokana na kukuunda?

Nikufundishe tu kdg sim zinatengenezwa kwa series ndo maana mpka sasa to iPhone 18 kila toleo linamakosa yake ila ni bora kwa wakati huo.. makosa ya toleo 1 hufanya tolelo jingine kuwa bora.. fanya kizazi chako kuwa bora si kwa kulaum Bali kujenga cha kwako kwa kurekebisha makosa yakiyopita..


Mwisho usiichezee bahati ukiyo nayo unababa bora mno mnooo
 
Naelewa ulichopitia mkuu.
Mtu ambae hajawahi potia situation kama hii lazima alete kejeri.
Mimi mzee ametangua mbele za haki, lakini i truly hate him as my daddy.
Kuna wazee wanazingua sana.
Pole mkuu, nakuombea upone.
 
Inawezekana ikawa sio vipigo au kuumizana physically but ni ile psychological torture, mzazi anaweza asikupige Sana lakini kuna moments Fulani za maneno na hisia zinatolewa na mzazi mfano mzazi hataki ukosee hata kidogo na ukikosea Tu maneno atakayotoa hapo ni ya kuonesha namna ulivyo kilaza wa mwisho wakati ilikuwa labda ni suala la kukuelekeza ili uelewe Tu na wala sio kulalamika lalamika, Yeye ni kunyoosha vidole Tu mwanzo mwisho akiingia ndani, Kwanza kukuita Tu ni Kwa Ukali...

Kuna wazee akiingia nyumbani hacheki na kima, Hakuna hata siku moja mnaweza kukaa kama familia Kuongea tu vitu vya Hapa na pale, yeye anachojua ni kuelekeza Tu tena Kwa ukali Sana, anachukulia familia Yake kama wafanyakazi wake kazini, watoto wanaweza kuwa na mambo Yao ya kukwambia lakini hawawezi Kwani Baba haingiliki, yaani hata mke nae pia anashindwa Kuongea na mume wake Hadi akuvizie, Mzee anatengeneza Aura mbaya Kwa watoto, Yaani utakuta mzazi hapigi Sana fimbo lakini Ile interaction Yake na familia Yake imekaa kipumbavu Sana nahisi ndio mtoa mada katokea mazingira haya...

Pwani watu wa Aina hiyo huitwa watu wenye GUBU ambapo uzee wao wanaishi maisha ya upweke na ya kusikitisha Sana maana Ile bond na watu wengine kama watoto haikutengenezwa vizuri Kipindi cha makuzi.... waswahili waliposema "MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO hawakukosea. Ukitengeneza furaha Kwa mtoto baadae itakurudia halikadhalika na huzuni pia vle vle ukitengeneza baadae pia itakurudia...Sio Kila kitu ni cha kuwa mnazi.
 
Naelewa ulichopitia mkuu.
Mtu ambae hajawahi pitia situation kama hii lazima alete kejeri.
Mimi mzee ametangua mbele za haki, lakini i truly hate him as my daddy.
Kuna wazee wanazingua sana.
Mkuu, mkumbuke mzee kwa mazuri usitunze chuki kwa mtu aliye kuleta duniani hata kama ana mapungufu makubwa kiasi gani
 
Yaani mzazi anakuwa mkali hadi mtoto akifanyiwa kitu kibaya anaogopa kusema,hii kitu mimi naiepuka sana. Ndo baadae mtu anashtukia mtoto alikuwa anafanyiwa ukatili ila hasemi kisa baba au mama mkali, mtoto anakosa msaada kwa ukali wa mzazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…