Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Mkuu katika hiki ulichokiandika mfano nikisema unioneshe convincing part inayoelezea ubaya wa mzee wako, unadhani unaweza ku point maelezo gani?
Nimeeleza kwa ufupi sana na nahisi wengi wameelewa mkuu

Kuchimba zaidi haina haja tena.
 
Wazazi wangu walinipiga vibaya sana wakinituhumu kuwa nimeiba pesa za mishahara zao na kiukweli sikuiba Wala Sina taabia ya wizi , nilikuwa ndio naingia form one

Niliapa kuwa sitowasamehe na wao wakinisikia sikulala usiku mzima nawalaani tu

Kitendo kilikuwa cha maudhi na udhalilishaji, ingekuwa mambo ya human rights ningetolewa nisiishi nao hata miaka miwili

Ila nilisamehe kutoka moyoni ila sitosahau kamwe na nikivurugwagwa nawaulizaga zile pesa alichukua Nan? Kwa sababu Mimi sikuchukuaga, ilitokea 2008 now 2026 ila nawachanganyaga Kwa kuwauliza, sikupendezwa na lile jambo

Kevzy
 
Sijamaliza stori yako but inaonekana mzee alikuwa anakutakia mema japo muda mwingine jinsi ya kudeal na watoto kila mtu na mbinu zake so sijaona kosa la mzee
 
Mama yangu was such a best woman ever existed (may she rest easy)
Kwanza hongera sana kwa wito mkubwa ulio nao kwenye kuandika kiingereza chenye makosa. "A best"?? Kiwanglish waachie dada zako. Binafsi kulingana na maelezo yako sijaona tatizo la baba yako. Ingekuwa umeandika alikuwa hawahudumii mahitaji yenu muhimu na kuwapeleka shule ningeona kuna hoja. Yeye kuwalinda ni jambo kubwa sana kawafanyia. Kijana acha pigo za kiwaki kujiliza kifala. Hata wewe utakuwa baba na utaona changamoto kuhakikisha familia inakuwa sawa kwenye kila angle.
 
Unajua hapa kuna context nyingi sana za kuongelea...

Ila naona kama Scars amedive moja kwa moja kwenye malezi...

Kwenye malezi kuna facets nyingi sana..

Hauwezi kureduce malezi kirahisi na kuja na conclusion ya moja kwa moja eti mzee alikuwa sahihi kuwaadabisha... To consider him sane kisa alikuwa mzazi bora, without looking on the psychological welfare, lakini pia kuingia ndani zaidi... Kujua how both culture and environment zinachagiza vikubwa growth ya mtoto..

It ain't that simple na kuridhika na mawazo ya namna hiyoo..

Waafrica tunapenda kureduce mambo ambayo ni soo complex, tunapenda kufeel closure kwenye kila jambo.. Na hii ndo inafanya hata matatizo ya kifamilia yasiishe kila kukicha
Niweke wazi mlezi mkuu ni Mungu pekeake

Wengine tumejilea wenyewe na kujionea hili baya hili zurii...

Kuna dogo baba Yao alikua mkali sana ukitoka shule saa nane unakula then kulala mchana baadae tution jioni

Walikua wanabanwa sana ila mbona mzee hakutoboa

Wengine tumejilea wenyewe mpaka tunakua wazazi walikua ni kutupa miongozo ila sio kutu guide kidicteta
 
wewe Ni wa kike
au wa kiume
kama ni wa kiume
utakuwa unamsikiliza mama yako na mama yako anakuona hu na akili na hujui
na Kama Ni wa kike
utakuwa una Fanya ngono
na wat u wanao
lingana na Baba yako
 
Niweke wazi mlezi mkuu ni Mungu pekeake

Wengine tumejilea wenyewe na kujionea hili baya hili zurii...

Kuna dogo baba Yao alikua mkali sana ukitoka shule saa nane unakula then kulala mchana baadae tution jioni

Walikua wanabanwa sana ila mbona mzee hakutoboa

Wengine tumejilea wenyewe mpaka tunakua wazazi walikua ni kutupa miongozo ila sio kutu guide kidicteta
Sisi mzee wetu alikuwa anatupeleka sinema miaka hiyo ya 90 kwenye 93 hivi. Alitupa uhuru wa kutosha ila giza likikukuta nje ni kichapo cha haja. Udikteta sana pia sio mzuri.
 
Sema wazee nao sometimes miyeyusho sana, mimi kuna kipindi nilikuwa sielewani na mzee mpaka akanifukuza home, akatangaza kwa ndugu zake nimekuwa muhuni na nimempiga😂 nilikaa kimya sikumjibu na nikampotezea kabisa kwenye life langu. Ila baadae aliniita kwake akaniomba msamaha, now tupo fresh japo mimi kiukweli sipo kama nilivyokuwa nae kabla.
 
Fikisha miaka 35+ kwanza, ndipo utamwelewa baba yako. Achana na hizo movie za Kikorea na Kifilipino.

Wengine tumepigwa sana na wazazi wetu kuliko hata wewe, lakini hatukuwahi hata siku moja kufikiria kutoa kauli kama yako.

Leo hii tuna familia zetu, na ndipo tumeanza kuwaelewa wazee wetu. Tunatamani wangekuwepo ili tuwaombe msamaha na kuwashukuru, lakini kwa bahati mbaya hawapo tena.

Heshima kwa wazazi ni jambo la muhimu. Mara nyingi, kadiri umri unavyoongezeka na majukumu yanavyoongezeka, ndipo mtu huanza kuelewa kwa kina sababu za maamuzi yao.
 
Back
Top Bottom