Hassan Mambosasa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2014
- 3,963
- 5,757
Ukija kupata watoto wako na kuwa na familia yako ndiyo utaelewa Mzee wako alikuwa namna hiyo kwa sababu zipi. Licha ya kuwa umeshaanza kutambua msingi wa maisha yako na nidhamu alikujengea imetokana na hayo malezi. Bado utajua zaidi
Kwa umri wako uliyotaja wewe ni Gen Z, mikumbo ya wenzako wa umri hup isikupoteze mwelekeo ukamuona Mzee ni mbaya. Ana upendo mkubwa sana kwako na angekuwa hakupendi hata kukuhudumia na kukusomesha asingefanya.
Unatakiwa ujue baba zetu wanaficha mengi sana vifuani mwao na pia ni wagumu kuonesha hisia zao za waziwazi aa upendo kama mama zetu. Hadi unapewa huduma muhimu, ukiumwa unatibiwa na umesomeshwa mpaka unatoka home. Unaona kayafanya hayo yote sababu gani? Yaani unaona msaada wake kama mtoto kaumaliza ndiyo unaapa usirudi nyumbani hata kumsalimia.
Ndugu nikwambie kama ni upweke wa mzee wako na kutaka walau urudi, kugoma ni utamtia msongo wa mawazo uje kumfanya augue na kupoteza maisha mapema. Huwezi jua uwepo wako wewe kwake una maana gani.
Wanaume hatutamki nakupenda ndiyo ujue mzee wako anathamini vipi. Usisubiri mpaka uje kumpoteza ndiyo uone ana umuhimu gani kwenye maisha yako. Wakati huo una majuto makuu moyoni mwako, utatamani muda urudi nyuma huwezi.
Kuhusu suala la mama yako naomba nisiliguse sana. Ila nikwambie tu yanayotokea ndani ya kuta nne za chumba cha wazazi waachie wenyewe. Huwezi ukawa unajua kila kitu kuhusu mambo yao na hakuna hata mmoja ambaye atakuwa tayari kukueleza kila kitu kuhusu maisha yao. Kujifanya kuchukua upande na kulaumu mmojawapo ni kufanya makosa sana. Na wewe utakuja kuwa na watoto utayaona hayo pia.
Muda ambao utayajua kuwa ya wazazi ni ya kubaki nayo wenyewe. Ndiyo utajikuta ukijuta. Sasa nakushauri usije kusubiri uje kuishi maisha ya majuto kisa mihemko ya hisia zako. Tulia
Hatukuzaliwa na kulelewa na malaika, bali na wanadamu kama sisi. Wana mapungufu na kukosoea kama sisi..... Mzazi mmoja hisia zake ni ngumu hata kama mwenza wake ana mapungufu hawezi mwambia mtoto, mwingine ana hisia dhaifu huweza yasema yote. Chukua mazuri ya kila mzazi yawe mfano, mapungufu jifanye hayakutokea
Baba yako hawezi kukwambia mapungufu ya mama yako, sababu atakuwa anajitukana mwenuewe kukuonesha alikuwa mzembe hakuchagua mama bora. Anakaa kimya kumpa heshima mama na wewe pia... mama ni tofauti sana ingawa wapo wachache wanaficha pia.