Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Nimeisoma hii thread yako nikapata hisia Kali sana. Kwanza pole sana, watu wengi hawatakuelewa coz sisi waafrika hatuna Mila wala desturi zakusaidia wanaume kwenye swala la afya ya akili. Unachopitia wengi tumeshapita huko.

Usharudi wangu kwako ni, kama wewe ni mkristo embu mtafute mchungaji mmoja mtu mzima au kama.sio mkristo basi tafuta hata therapist ambaye unaweza kukaa naye chini myaongelee haya mambo kiundani.

Usichukilie poa tu kwamba ni mzee wako so huwez fanya lolote, unamsamehe nakukaa naye mbali, hapana, hyo haufai na Wala haiyoshi, we ona tu hapo ulipo bado unateseka moyoni na bado unasema umemsamehe, hicho kitu sio rahisi kukuyoka moyoni, unahitaji msaada mkubwa wakisaikolojia.

Kitu kingine, karibu kukaa na baba yako hata mara moja Moja, mwanzo sio lazma muonge mambo makubwa au mazito kaa tu naye hatafor small talks, na baada ya mda flani muambie la moyoni, hii mwanzo unafanya hvi ili kubuild trust na respect baina yenu. Muambie kila kituusibakishe hata kimoja, au kama unaona ngumu kuongea muandikie hata barua.

Fanya maombi sana juu ya hili, hichi kitu Kiko sana spiritual. Kumuweka Mungu kwenye hili jambo ni muhimu sana.
Fanya hichi kitu mapema mtu wangu, wazazi hawaishi milele, Mimi mwenyewe sikuwa naelewana na baba yangu mzazi na sasa hivi ni marehemu. Kuna upande wa maisha yangu Nlishindwa kabisa kunyoosha naye mambo, ila cha mwisho nlikaa naye karibu coz nlikuwa namuuguza.
Kila.la.kheri ndugu, Mungu akutie nguvu kwenye hii changamoto unayopitia
Nashukuru sana kiongozi..
Kwa sasa mpaka umeona nimeshare hii stori ni kwamba nimesha heal kisaikolojia..

Ni naelewa kabisa jinsi mambo yalivyo unfold na namna jinsi mzee wangu alikuwa kipindi kile mpaka sasa...

Nitafanya jitihada niweze kwa namna niwezavyo ili mambo yakae sawa mkuu

Nashukuru na pole kwa kuondokewa na baba mzazi.
 
Mkuu, jilazimishe, kuwa karibu na mzee.

Kama alitoa fedha yake ukapata huduma hiyo inatosha sana sana sanaaa.

We piga simu nenda kamchomee nyama mpige story hata mara moja kwa wiki.

Mkisha kaa mara mbili tatu story zitakuja nyingi tu na parts za story zinaweza kuwa hizi hizi ulizozipiga hapa kumhusu. Anaweza kukupa upande wake wa hadithi ukamuelewa sana.

LIFE IS SHORT, KUNA SIKU HUTAKUWA NA HIYO NAFASI ACHA MARINGO.
Sawa, nitafanya Kadri niwezalo mkuu
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kila binadamu huwa anakuwa na mtihani wake... Leo nimeona nitoe japo snippet yangu, kwa vile hili jukwaa ni kubwa nadhani naweza kupata mtu wa kunibadilisha mawazo..

Kwanza kabisa.... I'll be 29 this month. Na kuna vitu huwa navipuuza but they're starting to make clear sense now..

Si unajua utu uzima dawa Buddha! So japo mapambano yanaendelea kuna time inabidi uwe vulnerable kidogo uache ego ikae pembeni maana haiweki chakula kwenye sahani wala kulipa kodi.

So, kufupisha stori ni hivi...

Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena... Maana Kadri siku zinavyoenda nazidi kupata picha yake halisi na ninazdi kukosa connection nae kabisa sioni kama kuna umoja kati yetu..

Ninamheshimu sana mzee, amenipa maisha, ya kipekee sana, katusomesha, he was overly protective. Ila alikuwa sijui itakuwa sahihi kusema kapitiliza kutoa protection..

Baba yetu alikuwa mtu wa perfection yaani hataki kusikia ulisahahu nini, alikuwa hataki mazoea na watu growing up nimelelewa maisha ya geti kali.. Hatukua wa kishua hata ila ni vile tu mzee alikuwa na secure job.

Mama yangu was such a best woman ever existed (may she rest easy)

Sitaki kwenda deep zaidi, ila hayo maisha ni mabaya sana kwa watoto. Yanawaharibu sana kisaikolojia..
Mzee wangu alikuwa so controlling na ikifika hatua by the age of me getting to secondary school nikawa naona kabisa haya maisha sio right.. Yaani he was dealing with alot for sure, but even when since mom was still available akifanya vile vile kwake, so nimekuwa nikiona familia iliyo njema na yenye furaha kwa nje, but giza likitanda usiku ni hatari.. Kelele torture kwa wanaishi ndani.

Sitaki kuingia sana kuelezezea nini kulikuwa kinatokea ila nahisi mmepata picha sahihi..

Ili fika kipindi ikawa ukifika muda wa kurudi shule moyo unafurahi... Ila bado unatoka home na Maumivu tu, yaani it was hell... Na ukiwa mtoto wa kiume inapaswa umezee ndani. Usiwe weak, usiwe coward..

My school life was nerve wrecking, I never enjoyed it.. Hata ndugu hawakutaka kusikia kuhusu mimi na drama za mzee wangu. It was lonely as fvck.. It reached a point nikawa suicidal kabisa.. Ningekuwa najua mbinu za Kujimaliza ningelifanya hivyo.. I always thought of my mom.. Na hata kifo chake mzee pia alichagiza(she was tired of all the mess)... Na muda nikikaa kufikiri huwa natumia vibaya sana.

Kupunguza stori, ni kuwa beside yote hayo mzee katufunza kuwa disciplined, alikuwa ni mtu wa nothing happens usipo jituma. Na ilinisaidia sana kuperform shule I despite mazito niliyo kuwa na pambana nayo ndani.

Ila with all the chaos, nilipo fika chuo nilisema mazima home, or tuseme nilikuwa soo tired hata kumface mzee machoni ilikuwa trauma inducing. Ilikuwa hata akinioigia simu natetemeka kuokota.. Hiyo ni miaka ya 2021 na huko na maliza chuo nikasema.. I have nothing to do with him, nikajiapia ntarudi ila I was terribly tired of thinking atakuwa sawa. Ilikuwa ni kelele daily aisee..

Sasa baada ya kutoka home life ilikuwa ngumu mbaya mbovu... Sijawahi kuona uchungu wa kutafuta wazee, that's when life kicked me to the curve. Nililala chini mimi. All I had was money ya kodi tu. Nikifanya kazi kama mtumwa, na sijui hata ujasiri huo Ulitoka wapi.. All I did was for money, imagine unafanya kazi kutwa unapata elf5? Hapo Natafuta Ajira ya kujishikisha.

All was well, baada ya muda nikaanza kuwa stable, na maisha ya kaanza kuwa smooth, but trust me kuna muda kidogo nirudi home, ila ili shindikana kwa sababu ningeaibika tu. I worked my ass off nikaanza kuona matunda.. Japo Sija fika ila I see progress.

So baada ya miaka kama mi3 hivi ya ku struggle ndo sasa naanza kuiona picha halisi ya mzee, wangu. He only instilled fear on me. Nimejikuta nikichukia watu sana, nikichukia hasa kuona mtu ana I control... Hasa makazini. Sipendi mtu aniamrishe(huwa ina induce pain kutoka kwa mzee wangu)

I know ni kwa sababu ya zile kumbukumbu za mzee wangu, nimekuwa nikijibizana sana na maboss kazi baada ya kazi, nataka niwe my own boss. Ila we both know sio rahisi. Maisha ya nahitaji kujishusha ila kwangu inakuwa kipengele maana huwa naweza kuwa people pleaser au kujiona kupitiliza(hii ni imbalance ya bad treatment utotoni)
Najaribu kujifunza na kuwa bora, na naona matokeo kuhusu hilo(it's taken me years of shadow work)

Tukiachana na hayo yote, baada ya muda mrefu mzee amekuwa kama anataka nirudi, najua uzee na upweke utakua unammendea ila sioni kama nitaweza hata kumface tena.

Hivi unajua ile ya kuwa huna commonness na mtu? Yaani unajua kabisa huyu ni mtu wa namna gani, na unajua hata iweje hawezi kuwa wamoja?

Ndo ninavyo mwona baba yangu, I do respect and love him for being a good Dad. Ila ile treatment yake udogoni iliniharibu vibaya sana mustakabli wa maisha yangu, nimesha samehe na namtakia afya na maisha marefu sana but sioni kama tutakaa kuelewana tena. Yeye ana namna anayaona mambo ambavyo mimi sioni..

So kama mtu mzima, na utu uzima dawa nimeona hakuna haja tena ya kukaa na jambo lenye kuja kuwa na impact ambayo mimi huenda nisiione now.

Ningependa kama tungeacha drama kidogo katika hili, ingependeza kidogo.
Hongera kwa kujisimamia na kujifunza kadiri maisha yanavyokwenda. Inaelekea utakuwa mwenye mafanikio kwani unajua udhaifu wako, unaurekebisha. Mzee mjulie hali, msaidie inapobidi, umeshaanza maisha yako, kurudi nyumbani ni kusalimu tu.
 
Hongera kwa kujisimamia na kujifunza kadiri maisha yanavyokwenda. Inaelekea utakuwa mwenye mafanikio kwani unajua udhaifu wako, unaurekebisha. Mzee mjulie hali, msaidie inapobidi, umeshaanza maisha yako, kurudi nyumbani ni kusalimu tu.
Asante sana kiongozi 🙏
 
Nimesoma hadi mwisho lakini sijaona sehemu yeyote ambayo mimi kama msomaji naweza kupata connection ya ubaya wowote aliofanya Baba yako ambao unaweza ku link up na chuki yako dhidi yake.

Hujafafanua vizuri uliposema giza likitanda ni mateso kwa wanaoishi ndani, so mpaka sasa sijaelewa ubaya wa Baba yako ni kukupiga, kumpiga Mama yako pamoja na wadogo zako?

Na kwasababu kwenye maelezo yako umesema hautaki kwenda deep nashindwa kuelewa kama Baba yako alikuwa na tabia ya ulevi kwamba hayo mambo ambayo alikuwa akiyafanya, pengine hakuwa katika utimamu sahihi.

Na kama alikuwa anakuadhibu, hujaelezea ulikuwa ukiadhibiwa kwa namna gani yenye kufanya neno torture liwe neno sahihi ku describe hiyo situation.

Kwasababu makuzi yetu ya kiafrika ni ngumu sana watoto kukua na kufuata matakwa ya wazazi wao bila viboko.

Sasa sijajua kama hivyo viboko na adhabu ndio vilikuwa ni sababu ya hiki ulichoakiandika au kuna mengine ambayo hujaweka wazi.
Kwa kifupi hajafunguka kueleza nini hasa baba alikuwa anawafanyia. Kwa maelezo yake naona baba yake alikuwa mlezi mzuri tu. Tatizo liko kwa mtoto kuona kuwa baba anawanyima uhuru!! Huo uhuru alikuwa anaitaka ili autumieje?
Kuna watu wakishakuwa watu wazima huwalaumu na kuwalaani sana wazazi wao kwa kuwadekeza na kuwapa uhuru wote na wakajikuta wameharibika kwenye ulevi wa kupitiliza, madawa ya kulevya na mambo kama hayo!
 
Hiyo will sinayo niliona tu bahati mbaya kwenye karatasi zake😀

Malengo makubwa ya mtoto wa kiume ni kufanya zaidi ya alichoweza kufanya baba yake. So at this point am in my journey

Sijawah wazia mali ya mzee kabisa. Not even entartaining the idea
Nikujoin basi kwenye hiyo journey niwe side mirror yako Mangi..!! 😹

Nyie msiowazia mali za urithi siku zote ndio wale The chosen one katika familia..!! Utajiri kwenu kugusa..!
 
Nikujoin basi kwenye hiyo journey niwe side mirror yako Mangi..!! 😹

Nyie msiowazia mali za urithi siku zote ndio wale The chosen one katika familia..!! Utajiri kwenu kugusa..!
Utajiri mzuri unatoka kwa Nuru 😀 Treasury of Light.
 
Back
Top Bottom