Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Wa
Ndio maana ukiwaangalia Watanzania/ waafrika wengi ni kama wana matatizo ya afya ya akili. Maofisini, kwenye biashara, celebrities, wanasiasa etc

Mtu anaona bora afukuze mtu kazi na wengine wapo radhi waue ili kuepuka simple criticism.

Violence kuna namna inatengeneza watu wenye matatizo makubwa sana ya kihisia na kiakili. Angalia tu sehemu zilizopitia ubaguzi mkali kama blacks wa South Africa, USA, India.. Kuna namna utaona tabia zao zinafanana haswa kwenye kuzoea na kutenda violence

Kwa hiyo jamaa namuelewa,

Watoto wenye ufahamu mkubwa huwa hawapo kwenye hilo group la "wengi". Huwa wanaangalia usahihi wa kitu na sio mazoea ya watu. Ndio maana kwako ilikuwa kawaida ila kwake haikuwa kawaida
Waafrika hawana matatizo mengi ya kisaikolojia kama Wazungu wazungu ni waoga wa sheria tu ila wengi wana matatizo ya akili kuliko sisi.
 
And, I'm not saying you dislike him. I'm simply saying you don't even have to like him to meaningfully connect with him. Talk to him frequently about different subjects. You will find something you both agree on. Then use that to cultivate a positive relationship with him. You obviously also have your own psychological issues. Work on those separately with the help of a professional or religious therapist.
Hayo ni mawazo yako..

Ila kuhusu ku cultivate positive relationship is what am working towards.
 
Pole mkuu kwa uliyopitia na hongera kwa ujasiri wa kuongea. Your feelings are valid na wala usiruhusu mtu yoyote akushawishi uone kwamba hujaumia wala baba yako hakukosea, childhood trauma is real na hakuna trauma inayoweza kulinganishwa na hiyo hali endapo ikimpata mtu.
Kama una pesa, nenda kwa mtaalamu wa afya ya akili, kama private ni gharama nenda serikalini.
Kama uliwahi kuwa suicidal huko nyuma na hiyo hali haikupatiwa matibabu ,kuna uwezekano mkubwa hiyo hali ya suicidal ikarudi baadae. Nenda kapone na hakikisha umepona.
Pole mkuu,pole sana.
😂😂😂huyo daktari anaapoanza project ya kumhudumia mgonjwa,atataka dhumuni la mogonjwa mwenyewe kwanza.
What if kwa mtu anayesema haoni haja ya kuwa awa tena?
 
Ukifika umri wa kua na familia ya mke na watoto,utagundua kua Baba yako hakukosea kitu bali yalikua ni malezi kwa manufaa yako wewe mwenyewe .
Nilitaka kuandika comment ya namna hii, kuna wakati wazee wetu tunawaelewa ila ni baadae sana, huenda baada ya kuwa na familia, au wao wakishatoweka dunia.

Kuwa baba sio kazi rahisi.
 
Pole mkuu kwa uliyopitia na hongera kwa ujasiri wa kuongea. Your feelings are valid na wala usiruhusu mtu yoyote akushawishi uone kwamba hujaumia wala baba yako hakukosea, childhood trauma is real na hakuna trauma inayoweza kulinganishwa na hiyo hali endapo ikimpata mtu.
Kama una pesa, nenda kwa mtaalamu wa afya ya akili, kama private ni gharama nenda serikalini.
Kama uliwahi kuwa suicidal huko nyuma na hiyo hali haikupatiwa matibabu ,kuna uwezekano mkubwa hiyo hali ya suicidal ikarudi baadae. Nenda kapone na hakikisha umepona.
Pole mkuu,pole sana.
I think kwa mental stamina nilonayo na yote nilopitia... Nimesha vuka hayo yote mkuu. Nimesha fanya healing sana by 2023 nilikuwa soo healed. Kilichobaki ni repetition tu ya vile tayari nimesha anza kuvi embody.


So, niko salama salmini
 
Ukifika umri wa kua na familia ya mke na watoto,utagundua kua Baba yako hakukosea kitu bali yalikua ni malezi kwa manufaa yako wewe mwenyewe .
That’s what nilisamehe kila lililotokea mwanzo na kuanza maisha mapya ya furaha na watu wote,tuko pamoja na maisha yanaendelea.

NB:kila mtu ajue nafasi yake tu.

de Gunner samehe,usamehewe buddy no one is perfect.
 
Jaribu kuzingatia uandishi wako, usichanganye sana lugha.

Kuna matatizo hayarekebishwi kwa lawama, mfano ni hili hapa. Lawama haitokuponya, lawama haitorudisha muda nyuma.

Chamsingi umeshalijua tatizo, wajibika kama mtu mzima.

Usimuwekee kinyongo huyo mzee. Chuki huumiza pande zote mbili.
I'm trying my best mkuu
Ukishazoea kitu inakuwa ngumu sana kuacha... Hata misamiati ya kiswahili huwa haiji sana sana... Nimeshazoea kingereza kwa sababu ndo nakitumia sana

Nimekupata mkuu
 
Kila binadamu huwa anakuwa na mtihani wake... Leo nimeona nitoe japo snippet yangu, kwa vile hili jukwaa ni kubwa nadhani naweza kupata mtu wa kunibadilisha mawazo..

Kwanza kabisa.... I'll be 29 this month. Na kuna vitu huwa navipuuza but they're starting to make clear sense now..

Si unajua utu uzima dawa Buddha! So japo mapambano yanaendelea kuna time inabidi uwe vulnerable kidogo uache ego ikae pembeni maana haiweki chakula kwenye sahani wala kulipa kodi.

So, kufupisha stori ni hivi...

Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena... Maana Kadri siku zinavyoenda nazidi kupata picha yake halisi na ninazdi kukosa connection nae kabisa sioni kama kuna umoja kati yetu..

Ninamheshimu sana mzee, amenipa maisha, ya kipekee sana, katusomesha, he was overly protective. Ila alikuwa sijui itakuwa sahihi kusema kapitiliza kutoa protection..

Baba yetu alikuwa mtu wa perfection yaani hataki kusikia ulisahahu nini, alikuwa hataki mazoea na watu growing up nimelelewa maisha ya geti kali.. Hatukua wa kishua hata ila ni vile tu mzee alikuwa na secure job.

Mama yangu was such a best woman ever existed (may she rest easy)

Sitaki kwenda deep zaidi, ila hayo maisha ni mabaya sana kwa watoto. Yanawaharibu sana kisaikolojia..
Mzee wangu alikuwa so controlling na ikifika hatua by the age of me getting to secondary school nikawa naona kabisa haya maisha sio right.. Yaani he was dealing with alot for sure, but even when since mom was still available akifanya vile vile kwake, so nimekuwa nikiona familia iliyo njema na yenye furaha kwa nje, but giza likitanda usiku ni hatari.. Kelele torture kwa wanaishi ndani.

Sitaki kuingia sana kuelezezea nini kulikuwa kinatokea ila nahisi mmepata picha sahihi..

Ili fika kipindi ikawa ukifika muda wa kurudi shule moyo unafurahi... Ila bado unatoka home na Maumivu tu, yaani it was hell... Na ukiwa mtoto wa kiume inapaswa umezee ndani. Usiwe weak, usiwe coward..

My school life was nerve wrecking, I never enjoyed it.. Hata ndugu hawakutaka kusikia kuhusu mimi na drama za mzee wangu. It was lonely as fvck.. It reached a point nikawa suicidal kabisa.. Ningekuwa najua mbinu za Kujimaliza ningelifanya hivyo.. I always thought of my mom.. Na hata kifo chake mzee pia alichagiza(she was tired of all the mess)... Na muda nikikaa kufikiri huwa natumia vibaya sana.

Kupunguza stori, ni kuwa beside yote hayo mzee katufunza kuwa disciplined, alikuwa ni mtu wa nothing happens usipo jituma. Na ilinisaidia sana kuperform shule I despite mazito niliyo kuwa na pambana nayo ndani.

Ila with all the chaos, nilipo fika chuo nilisema mazima home, or tuseme nilikuwa soo tired hata kumface mzee machoni ilikuwa trauma inducing. Ilikuwa hata akinioigia simu natetemeka kuokota.. Hiyo ni miaka ya 2021 na huko na maliza chuo nikasema.. I have nothing to do with him, nikajiapia ntarudi ila I was terribly tired of thinking atakuwa sawa. Ilikuwa ni kelele daily aisee..

Sasa baada ya kutoka home life ilikuwa ngumu mbaya mbovu... Sijawahi kuona uchungu wa kutafuta wazee, that's when life kicked me to the curve. Nililala chini mimi. All I had was money ya kodi tu. Nikifanya kazi kama mtumwa, na sijui hata ujasiri huo Ulitoka wapi.. All I did was for money, imagine unafanya kazi kutwa unapata elf5? Hapo Natafuta Ajira ya kujishikisha.

All was well, baada ya muda nikaanza kuwa stable, na maisha ya kaanza kuwa smooth, but trust me kuna muda kidogo nirudi home, ila ili shindikana kwa sababu ningeaibika tu. I worked my ass off nikaanza kuona matunda.. Japo Sija fika ila I see progress.

So baada ya miaka kama mi3 hivi ya ku struggle ndo sasa naanza kuiona picha halisi ya mzee, wangu. He only instilled fear on me. Nimejikuta nikichukia watu sana, nikichukia hasa kuona mtu ana I control... Hasa makazini. Sipendi mtu aniamrishe(huwa ina induce pain kutoka kwa mzee wangu)

I know ni kwa sababu ya zile kumbukumbu za mzee wangu, nimekuwa nikijibizana sana na maboss kazi baada ya kazi, nataka niwe my own boss. Ila we both know sio rahisi. Maisha ya nahitaji kujishusha ila kwangu inakuwa kipengele maana huwa naweza kuwa people pleaser au kujiona kupitiliza(hii ni imbalance ya bad treatment utotoni)
Najaribu kujifunza na kuwa bora, na naona matokeo kuhusu hilo(it's taken me years of shadow work)

Tukiachana na hayo yote, baada ya muda mrefu mzee amekuwa kama anataka nirudi, najua uzee na upweke utakua unammendea ila sioni kama nitaweza hata kumface tena.

Hivi unajua ile ya kuwa huna commonness na mtu? Yaani unajua kabisa huyu ni mtu wa namna gani, na unajua hata iweje hawezi kuwa wamoja?

Ndo ninavyo mwona baba yangu, I do respect and love him for being a good Dad. Ila ile treatment yake udogoni iliniharibu vibaya sana mustakabli wa maisha yangu, nimesha samehe na namtakia afya na maisha marefu sana but sioni kama tutakaa kuelewana tena. Yeye ana namna anayaona mambo ambavyo mimi sioni..

So kama mtu mzima, na utu uzima dawa nimeona hakuna haja tena ya kukaa na jambo lenye kuja kuwa na impact ambayo mimi huenda nisiione now.

Ningependa kama tungeacha drama kidogo katika hili, ingependeza kidogo.
Pole sana. Naelewa kwa kiasi fulani maisha uliyopitia, na bahati mbaya watu wengi wamepitia hali kama hiyo. Kwa wale ambao hawajawahi kuona madhara yake, mfano mzuri ni maisha ya Michael Jackson na baba yake, Joe Jackson.

Joe aliamini kwamba ukali, vipigo na maneno makali vitamjenga mwanawe na kumfanya awe bora. Lakini kwa upande mwingine, malezi hayo yalimwachia Michael majeraha makubwa ya kisaikolojia na kumbukumbu ambazo ziliendelea kumfuata hata alipokuwa mtu mzima. Hapo ndipo tunapojifunza kwamba si kila kitu mzazi anachokiita “malezi” mtoto anakiona hivyo; wakati mwingine mtoto anakiona kama mateso.

Na hili ni jambo muhimu sana ambalo wazazi na walezi tunapaswa kulielewa: mtoto akiumizwa sana na mtu aliyepaswa kuwa sehemu yake salama, maumivu hayo yanaweza kumfanya ajitenge hata akiwa mtu mzima. Anaweza kufikia hatua ya kutotamani kurudi nyumbani, kutotaka kukutana na familia au hata kutotaka chochote alichorithishwa, kwa sababu kila anapokanyaga pale anakumbuka yale aliyopitia.

Ninasema hivi kutokana na uzoefu wangu binafsi. Baba yangu alifariki miaka 10 iliyopita, lakini majeraha ya kisaikolojia aliyoniachia yamekuwa makubwa kiasi kwamba sijawahi kujisikia kugeuka tena nyumbani. Hata baada ya yeye kufariki, sikuhisi kwamba kifo chake kilitosha kufuta yale yaliyopita. Niliwaambia ndugu zangu wazi kwamba kuhusu urithi wake, sitaki chochote; wagawane wao, mimi mniondoe. Si kwa sababu sina thamani ya vitu hivyo, bali kwa sababu kuna wakati amani ya moyo ina thamani kubwa kuliko mali.

Ndiyo maana huwa nawaambia wazazi na walezi: waacheni watoto waishi utoto wao. Msiwapokonye utoto wao kwa kisingizio cha “tunawajenga.” Mtoto anahitaji nidhamu, lakini nidhamu si sawa na kumdhalilisha, kumtukana au kumpiga bila mipaka.

Mtoto pia anahitaji kukosolewa, lakini akosolewe kwa heshima. Mfundishe kosa lake, mpe mipaka, msimamie, lakini usimvunje utu wake. Usimfanye mtoto aogope uwepo wako kiasi kwamba akue akitamani siku moja tu aondoke nyumbani na asirudi tena.

Kuna tofauti kubwa kati ya kumlea mtoto kwa ukali na kumuumiza mtoto. Na wakati mwingine tunatambua tofauti hiyo tukiwa tumechelewa.

Wazazi, watoto hawahitaji tu chakula, shule na mavazi. Wanahitaji pia usalama wa kihisia, upendo, kusikilizwa na kuheshimiwa. Utoto unapita mara moja. Usimnyang’anye mtoto utoto wake halafu miaka 20 au 30 baadaye ujiulize kwa nini hataki tena kuwa karibu na wewe.

Mlee mtoto kwa nidhamu, lakini usimlee kwa hofu. Mjenge, usimvunje.
 
Bwana Mdogo;
Wala usifikiri kwamba uko ulivo kwa sababu ya namna mzee wako alivyokutreat,Uko ulivyo kwa sababu wewe ni kama mzee wako alivyo.

Pili kama hakukua,hakukunyima chakula,hakukunyima mahitaji ya muhimu basi wala usithubutu kumsingizia iwapo wewe una changamoto zako.Mzazi humlea mtoto wake kwa kadiri anavyoweza yeye na anavyelewa malezi.

Mwisho Huu ni wakati muhimu sana wa wewe kukaa karibu na mzee wako kama watu wazima,sio kwa ajili yake bali ni kwa ajili yako.Hawa waze wetu pamoja na udhaifu wako huwa wana perspective.Kuna makosa walifanya na hawatataka wewe kama mtoto wao uyarudie/uyafanye?Kuna historia za familia,ushauri wa kiutu uzima,Urafiki n.k.

Kama anakutafuta basi ni wakati wa wewe kuwa naye karibu usijesema hukuambiwa.

CHILDHOOD TRAUMA zipo na kila mtu anazo.Hata kudekezwa na kupendwa sana huwa kunafanya watu wapate Trauma za aina yake kama vile kuwa narcicists.

Mpigie Mzee simu ukamsalimie acha ukauzu kama wa mzee wako umeshakuwa sasa its time to be your own man.Do not live in the Past.
🙏🙏🙏
 
Usielewane na mzazi?,kivipi?
Changamoto za maisha ni moja ya hatua ya ukuwaji,japo si wote watateseka kwenye hii dunia….

Mzazi naye ni mwanadam,niliwahi kumissunderstand na mzee lakini dakika za mwisho win is win.

Ok,unapojua kwanini upo duniani,unaweza kujichagulia maisha yako na huwezi pata kibaya chochote.

KAMA UPO UWEZEKANO WA WEWE NA MZEE KUKAA NA KUJADILI,(fanya hivyo)
Will do
Nashukuru mkuu
 
Kitendo cha kuendelea kukumbuka kua sijui Baba yako alikua mkali kwenu au kukumbuka mabaya yake,kina ashiria kua maisha yamekupiga so far,ungekua na good life usingekumbuka hayo,

Ndio maana kwenye ule uzi wako nilikwambia kua Get a life and you'll be better coz nilishaona tatizo lako,ila wewe ni kiumbe usie shaurika.
 
Kitendo cha kuendelea kukumbuka kua sijui Baba yako alikua mkali kwenu au kukumbuka mabaya yake,kina ashiria kua maisha yamekupiga so far,ungekua na good life usingekumbuka hayo,

Ndio maana kwenye ule uzi wako nilikwambia kua Get a life and you'll be better coz nilishaona tatizo lako,ila wewe ni kiumbe usie shaurika.
Actually my life is alot better... Sio kama kipindi naishi naye, financially... Am making a quite decent money.. Siwezi fika hata robo ya mshua. Ila am so good in terms of both aspects of life.. Naweza kuendesha maisha yangu vizuri tu... I see a bright future ahead kwa mipango niliyo nayo

So emotionally, kuishi home ilikuwa even worse.. Ndo maana I feel good in being this way, sioni haja ya kutaka kuvuka stage za mafanikio nitafika tu
 
Mom hakutudekeza japo alikuwa mpole..

Ulicho ongea hapa ni positive impact za kuwa strict.... Which is good nimekuelewa vizuri mkuu.

That's my plan too..
Keep helping your daughter lakini usimfanye awe uncomfortable sana, ikamharibu..

Nashukuru mkuu🙏
Kashasaidika mpaka sasa na wala hatuogopani. Mimi nikiwa sipo watoto ndio wananitafuta nirudi so hawaniogopi kwa namna yoyote ila discipline wanayo. Bila kuwanyoosha tutawapa walimwengu adhabu ya KUWALEA.

Kwa wewe umri wako ulipofikia ni muda wa wewe kuanza ku deal na mindset yako. Umri ulionao sio wa kulaumu malezi ya wazazi ni kuendelea kujidekeza. A man must stand strong.

TAfuta ushauri sehemu mbalimbali kama hv stay POSITIVE tiba inaanza na wewe otherwise you will transfer hayo mambo kwa wanao.

Mzee ametimiza wajibu wake na mpaka sasa humdai mengine ni wewe KUJIONGEZA na kurudisha hali ya kawaida maisha yaendelee.

Do that before it is too late...

Just simple question. Wewe ni wangapi kwenu na mpo wangapi? How old is the older one na mdogo ana umri gani?
 
😂😂😂🤣🤣🤣
Mom hakutudekeza japo alikuwa mpole..

Ulicho ongea hapa ni positive impact za kuwa strict.... Which is good nimekuelewa vizuri mkuu.

That's my plan too..
Keep helping your daughter lakini usimfanye awe uncomfortable sana, ikamharibu..

Nashukuru mkuu🙏
Kwa namna unavyoandika tu,inaonesha kuwa mzee asingekukazia tungeshakupoteza.Mara mom,mara dad,viingereza vingiii.Tumia lugha moja utaeleweka.Mzee wqko ni jembe,hapa namlaumu mama yako kwa sababu hata hizi chuki dhidi ya mzee inaonekana mama anazichochea.POLE SANA JUNIOR MKUBWA
 
Kashasaidika mpaka sasa na wala hatuogopani. Mimi nikiwa sipo watoto ndio wananitafuta nirudi so hawaniogopi kwa namna yoyote ila discipline wanayo. Bila kuwanyoosha tutawapa walimwengu adhabu ya KUWALEA.

Kwa wewe umri wako ulipofikia ni muda wa wewe kuanza ku deal na mindset yako. Umri ulionao sio wa kulaumu malezi ya wazazi ni kuendelea kujidekeza. A man must stand strong.

TAfuta ushauri sehemu mbalimbali kama hv stay POSITIVE tiba inaanza na wewe otherwise you will transfer hayo mambo kwa wanao.

Mzee ametimiza wajibu wake na mpaka sasa humdai mengine ni wewe KUJIONGEZA na kurudisha hali ya kawaida maisha yaendelee.

Do that before it is too late...

Just simple question. Wewe ni wangapi kwenu na mpo wangapi? How old is the older one na mdogo ana umri gani?
I understand mkuu.
Futhuer questions nitazidi kufanya isiwe na privacy..

Ila I get your point 🙏
 
Sijaelewa kitu naona vingereza tu.

Kwani ulitakaje? Ulitaka upakwe mafuta kisogoni?

Binti yangu Lamomy naomba unieleweshe hii hoja ya huyu GEN Z.
 
😂😂😂🤣🤣🤣

Kwa namna unavyoandika tu,inaonesha kuwa mzee asingekukazia tungeshakupoteza.Mara mom,mara dad,viingereza vingiii.Tumia lugha moja utaeleweka.Mzee wqko ni jembe,hapa namlaumu mama yako kwa sababu hata hizi chuki dhidi ya mzee inaonekana mama anazichochea.POLE SANA JUNIOR MKUBWA
Hayo ni mawazo yako. Hujui kitu kuhusu my mom.
 
Back
Top Bottom