Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Nimeisoma hii thread yako nikapata hisia Kali sana. Kwanza pole sana, watu wengi hawatakuelewa coz sisi waafrika hatuna Mila wala desturi zakusaidia wanaume kwenye swala la afya ya akili. Unachopitia wengi tumeshapita huko.

Usharudi wangu kwako ni, kama wewe ni mkristo embu mtafute mchungaji mmoja mtu mzima au kama.sio mkristo basi tafuta hata therapist ambaye unaweza kukaa naye chini myaongelee haya mambo kiundani.

Usichukilie poa tu kwamba ni mzee wako so huwez fanya lolote, unamsamehe nakukaa naye mbali, hapana, hyo haufai na Wala haiyoshi, we ona tu hapo ulipo bado unateseka moyoni na bado unasema umemsamehe, hicho kitu sio rahisi kukuyoka moyoni, unahitaji msaada mkubwa wakisaikolojia.

Kitu kingine, karibu kukaa na baba yako hata mara moja Moja, mwanzo sio lazma muonge mambo makubwa au mazito kaa tu naye hatafor small talks, na baada ya mda flani muambie la moyoni, hii mwanzo unafanya hvi ili kubuild trust na respect baina yenu. Muambie kila kituusibakishe hata kimoja, au kama unaona ngumu kuongea muandikie hata barua.

Fanya maombi sana juu ya hili, hichi kitu Kiko sana spiritual. Kumuweka Mungu kwenye hili jambo ni muhimu sana.
Fanya hichi kitu mapema mtu wangu, wazazi hawaishi milele, Mimi mwenyewe sikuwa naelewana na baba yangu mzazi na sasa hivi ni marehemu. Kuna upande wa maisha yangu Nlishindwa kabisa kunyoosha naye mambo, ila cha mwisho nlikaa naye karibu coz nlikuwa namuuguza.
Kila.la.kheri ndugu, Mungu akutie nguvu kwenye hii changamoto unayopitia
 
Kuna Binti alikuwaga anachapwa hivi na yeye kwa kuchangiwa kaka na mama,nilikuwa naumia nikimuona anachapwa vile, wote wanainua mikono juu wanashusha fimbo kwa pamoja daah, pole kama na wewe ulipitia hayo mkuu.
 
Kuna wazazi wengine ni monsters.
Sawa
We subiri aondoke ndio utaelewa vizuri,,hata kama Sasa unamuona mbaya kiasi gani.

Siku akiwa hayupo nakwambia, hayo mabaya yote unayomsemea sasahivi yatayeyuka yote.
Utakumbuka mema yake tu,hata kama ni kidogo.
Acheni kujiona wakamilifu, na kuona wazazi wenu hawana maana.
 
Natumia sana kuona watu wenye Baba mnawachezea, kuwapuuza na kuona hawana maana.
Ikibidi mtubu kabisa,Hamjui mlitendalo.
Hizo hisia haziji zenyewe mkuu, mtoto anapitia maumivu makali mfufulizo ndo anafikia hiyo hali. Jiulize mfano watoto wanaobakwa na baba zao, hawa nao wakilalamika utasema wanawapuuza baba zao?
 
Hizo hisia haziji zenyewe mkuu, mtoto anapitia maumivu makali mfufulizo ndo anafikia hiyo hali. Jiulize mfano watoto wanaobakwa na baba zao, hawa nao wakilalamika utasema wanawapuuza baba zao?
Sawa
Endeleeni kulalamika watoto.
 
Alisha kufilia mbali na sijaona pengo lake mpka umri huu.
Huwezi jua maumivu ya mtu, chuki hujengwa. Vipi baba aliekukataa na mama aliekutupa ukaokolewa na wapita njia, utakuwa na hisia gani kwa hao wazazi.?
Ni mzazi wako tu
 
Hama au ujitoa kwenye familia
 
Kama ukiwa hai watu hawaoni umuhimu wako,siku ukiondoka hakuna atakaekukumbuka. Undugu ni jinsi ulivyoishi na mtu sio kwa sababu wewe ni mzazi basi ukiondoka watu wataumia, watu huwa wanaumia kwa sababu ya mema waliyotendewa na aliyeondoka. Ila kama muondokaji aliumiza watu, pengo lake hakuna atakayeliona.
 
Kwahiyo watu wameumizwa wasilalamike? Wao ni maroboti?. Kama wewe ukiumizwa au ukikerwa hulalamiki ni wewe mkuu, wengine wanaongeaga kutoa sumu.
Mkuu
Mbona meseji yangu inaeleweka,nimeandika endelea kulalamika,
Kwani nimekulazimisha usilalamike?
 
Kwahiyo watu wameumizwa wasilalamike? Wao ni maroboti?. Kama wewe ukiumizwa au ukikerwa hulalamiki ni wewe mkuu, wengine wanaongeaga kutoa sumu.
Huyo aliwahi pigwa ban SF alilalamika utazani wanatoa mishahara kuwepo JF. Lakini hapa kaja na ushauri as if anajua maumivu ya watu wote na kayapima kaona hayana uzito huo wa kulalamikiwa.
 
Umewahi kufiwa na mzazi?
 
Huyo aliwahi pigwa ban SF alilalamika utazani wanatoa mishahara kuwepo JF. Lakini hapa kaja na ushauri as if anajua maumivu ya watu wote na kayapima kaona hayana uzito huo wa kulalamikiwa.
Unajuaje kama sipati mshahara/rizki kwa kuwepo Jf?
Ushauri wangu siyo sheria.
Halafu niliyemshauri alishanielewa.
 
💯
 
Unajuaje kama sipati mshahara/rizki kwa kuwepo Jf?
Ushauri wangu siyo sheria.
Halafu niliyemshauri alishanielewa.
Kama tukio lile lilikuuma basi jua na wengine kuna situation wanapitia zinawaumiza. Huo ni mfano tu.
 
Kama tukio lile lilikuuma basi jua na wengine kuna situation wanapitia zinawaumiza. Huo ni mfano tu.
Sijawalazimisha mkubali mtazamo wangu kuhusu wazazi.
Ukiona ushauri haukufai ni wa kipuuzi, unaachana nao tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…