Mimi nauliza nini sababu ya kuficha ficha Expiry date kwenye bidhaa nyingi hapa Tanzania? Kwanini zinaandikwa wala hazieleweki nini sababu?

Mimi nauliza nini sababu ya kuficha ficha Expiry date kwenye bidhaa nyingi hapa Tanzania? Kwanini zinaandikwa wala hazieleweki nini sababu?

polokwane

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2018
Posts
3,361
Reaction score
5,842
Hivi kwa mfano

.trashed-1689684791-IMG_20230618_154827.jpg


Naomba nisaidiwe kusoma hiyo expire date hapo kwenye picha

Na bidhaa za aina hii zipo nyingi yani expired date haieleweki kabisa utakuta imeandikwa ila huwezi kuielewa kabisa

Ni nini tatizo mbona bidhaa za nchi zingine zinasomeka vizuri kabisa tarehe ya kuzalishwa na mwisho wa kutumika vinaonekana na vipo wazi kabisa.

Hii nchi uhuni umezidi sana
 
Watu hawataki kupata hasara,matokeo yake tunaoathirika ni sisi.
 
Unaposema bidhaa za nchi nyingine unamaanisha zinazotengenezwa kutumika nje?
 
Zinafichwa mnooooo
Sasa kama wanaficha maana ya kuziweka nini?
Unakuta kopo jeupe halafu expire date imeandikwa kwa rangi nyeupe ili isionekake , lakini unakuta kopo jeusi halafu expire date imaandikwa kwa rangi nyeusi ili isionekane yaana ujanja ujanja tuu! Na ikionekana basi haieleweki.
 
Unaposema bidhaa za nchi nyingine unamaanisha zinazotengenezwa kutumika nje?
Hata zinazo ingizwa ndani lakini zimetoka nje nyingi zinasomeka na kueleweka , hata za kutoka kwa jirani zetu tu hapo kenya na uganda.
 
Unashangaa expire date hazieleweki siku hizi, wakati imefikia hatua mpaka jinsia za watu hazieleweki!
Pacha kwema. Long time asee.

Sema jamaa kaibua jambo ambalo hata mimi huwa linanitatiza sana sio bidhaa za Tanzania tu ni bidhaa zote. Kuipata Expiry Date/Best Before ni lazima mtu uhangaike sijui hawa watengenezaji kwanini huwa wanaficha sana hiki kitu.
 
Hao janja janja rejea lile tukio la azam juce kukutwa na tarehe ambayo haifika Yani Leo tare 28/6/2023 unakuta juice imetengenezwa tare 5/07/2023
 
Back
Top Bottom