Tony Cipriano
JF-Expert Member
- Nov 17, 2022
- 2,139
- 5,109
Hata utengenezaji wake huko kiwandani utakuwa balaa tupu.
Tupunguze au tuache kutumia vyakula vilivyosindikwa sio salama.
Tupunguze au tuache kutumia vyakula vilivyosindikwa sio salama.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli kabisa pacha, kitambo! Mambo yalibana hapa kati aisee!Pacha kwema. Long time asee.
Sema jamaa kaibua jambo ambalo hata mimi huwa linanitatiza sana sio bidhaa za Tanzania tu ni bidhaa zote. Kuipata Expiry Date/Best Before ni lazima mtu uhangaike sijui hawa watengenezaji kwanini huwa wanaficha sana hiki kitu.
Mamlaka zetu tumewapa wauwaji. Juzi hapa nilisikiliza speech moja ya PLO Lumumba aliongelea hili jambo.Kweli kabisa pacha, kitambo! Mambo yalibana hapa kati aisee!
Yaah jamaa ana point kubwa sana kwenye huu uzi, vitu vina expire ila vinazunguka mtaani, na wenye mamlaka husika hawajali!
Juzi nimekutana na Blue Band zimebakisha Siku 15 zi Expire. Jamaa wanatembeza mitaani na kuuza Elf 2,500/=Tsh badala ya 7,000/=Tshs. Hawa jamaa wapo sehemu nyingi! Najua watu wengi wameshakutana nao na bado wanakutana nao mitaani!
Week iliopita nlipita Pharmacy fulani kumnunulia dawa za Mzee wangu mmoja tunaefanya nae harakati za kutafuta maisha, ana matatizo ya mshipa mmoja wa moyo kuziba, basi nikampitishia kwake. Bila mimi kuzisoma expire date, yeye bahati akazisoma kumbe dawa zime Expire tokea January 2023. Akaniulia mwanangu mbona umeniletea Sumu badala ya dawa? Nikashtuka sana na kumuuliza kulikoni tena? Mbona sikuelewi?
Ndio akanielewesha zime expire!
Nikajiuliza maswali mengi sana.
Pole sana ndugu tuongeze umakiniNoma juzi nimekunywa juice nikawa siewi ladha yake ndio nikaanza kutafuta mwisho wa matumizi bhana wewe nilitoka jasho hapo mwisho nikakuta imepita mda aisee, duka lipo mtaani sijakachaga tena duka lile.
TZS 574 AZAM
Shida sio ya Watanzania.Shida ya watanzania mnapenda ku conclude mambo bila ya kuwa na uhakika.
Expired date kwa bidhaa zinazo ifadhiwa kwenye makopo zinandikwa kwenye ubavu wa chupa au chini kwenye kitako
View attachment 2671433
View attachment 2671434
Hiyo hapo jju kwenye mfuniko sio tarehe ni product ID au Bach number. Hizi zinatumiwa na scaner na viwandani kujua product and kuzipanga. Zipo juu ya mfuniko kwa sababu za urahisi wa kuzi scan.
Ukujaribu ku scan hicho ulicho weka kitaleta kama hivi:
Mfano
Code:TZS 574 AZAM
Dawa za meno, sabuniTaja mifano ya bidhaa hizo.
Mi nadhani sababu ni wenye jukumu la kusimamia kujisahau na kuishi kwa mazowea.Hivi kwa mfano
View attachment 2671366
Naomba nisaidiwe kusoma hiyo expire date hapo kwenye picha
Na bidhaa za aina hii zipo nyingi yani expired date haieleweki kabisa utakuta imeandikwa ila huwezi kuielewa kabisa
Ni nini tatizo mbona bidhaa za nchi zingine zinasomeka vizuri kabisa tarehe ya kuzalishwa na mwisho wa kutumika vinaonekana na vipo wazi kabisa.
Hii nchi uhuni umezidi sana