Kama huna kazi ya maana utafanya.
Hakuna mtu anapenda kufanya kazi zisizo na maana ila watu huzifanya huku wakiangalia michongo mingine.
Kuliko ukae home kama zindiko, unaomba hadi vocha kama kuna fursa ya wewe kua boda fanya kazi huku ukilenga michongo mingine mizuri.
Nilimaliza chuo nikawa manager wa bar, sinywi pombe wala kuvuta sigara na sipendi makelele ya bar na miziki mikubwa, lakini kuliko kukaa nyumbani ikabidi niwe meneja wa Bar. Pale pale bar ndio nikapata mchongo wa maisha maana hr wa taasisi moja kubwa alikua anapenda kuja kunywa pale. Baada ya kuona kujitathmini kwa muda na kusikia hoja zangu siku moja akaniuliza nina elimu gani, nikawamwambia ndio nimemalza chuo mwaka jana, akaniuliza kama nina vyeti original, nikasema bado, akasema ukivitapa njoo ofisini kwangu, kweli nilipovipata nikaenda, baada ya wiki 2 nikapigiaa simu kwenda kusaini mkataba.
Usidharau sana watu wanaofanya kazi flani, ni vile hawajapata fursa ya kazi wanazozipenda, wakipata wataenda huko.