Nimezaliwa mwaka 1960 na Muungano umenikuta nina mika 4. Nimesoma kwenye nchi ya Tanzania hadi shahada ya uzamili ndani ya Tanzania.
Leo hii nitakuwa kichaaa kudai Tanganyika. Tanganyika ili cease 1964 na sijawahi kupungukiwa kitu kwa kutokuwapo kwa Tanganyika.
Wengi wa wanaochangia huu mjadala wanafurahishwa na uropokaji wa Lissu tu lakini ukiwauliza Tanganyika itakupa nini ambacho leo huna ndani ya Tanzania wanabaki hawana jibu.
Kwa mfano ardhi huko Tanzania bara tuna 945,000 Square kilometres na mapori kibao. Mtu hajashika hata ekari moja kwenye mapori ya Kisarawe, ila anatamani apate ardhi ZNZ yenye 2,045 Square kilometres,