Mimi ni mwalimu, naacha kazi nijiajiri

Ujue walimu wengi awajielewi mwalimu degree unalipwa laki 9 harafu unalalamika njaa mnashindwa hata tuisheni
Usilichukulie kirahisi hivyo, sio kila sehemu tuition inafanyika! Maeneo mengine yana changamoto sana!

Halafu sio lazima iwe hiyo tuition, wewe unasema hilo kumbe wao wameona nyingine zaidi,
 
Unataka kujiajiri for wrong reasons na kufikiri kujiajiri ni kuakimbia matatizo yako. Kijana you need a mentor ambaye ni mfanya biabishara akupe A to Z kisha ufanye ifnrmed decision. Biashara inahitaji uifanye kwa moyo ndo utafanikiwa na si kwa sababu ilizozitaja hapo juu. Ushauri wangu mtafute mtu aliyefanikiwa ndo akupe ushauri don't seek advice from losers
 
Una busara sana mkuu!

Kuacha kazi sio suala ma mihemuko kama hivyo! Mtu anasema anaacha ajira halafu bado ana muda wa kuanzisha thread za namna hii[emoji18] [emoji18]
Huyu akiacha kweli maisha yatampiga balaa maana hajielewi - labda kama atajiunga na bavicha humu kutukana na kulaumu serikali 24/7
 
sisi tunaamini vp kama kweli ulikuwa mwl na sasa umeacha kweli? Tupe taarfa zako bila kusahau cheque namba yako
 
Da kweli hiyo kada inadharaulika sana yaani unashangaa lakini 9 kupata MWL. Sijajua unashangaa as a basic salary or take home?? Vyovyote iwavyo wengi tu wamevuka kiwango hicho
Acha kudanganya watu wewe basic salary ya mwl mwenye degree yaani TGTSD1 ni tshs 716000 (laki saba na kumi na sita elfu tu) na take home yake haifiki laki nne na nusu
 
Acha kudanganya watu wewe basic salary ya mwl mwenye degree yaani TGTSD1 ni tshs 716000 (laki saba na kumi na sita elfu tu) na take home yake haifiki laki nne na nusu
Ina maana walimu wote wanamadaraja sawa kwa uelewa wako siyo..... yaani walimu wote wenye digrii wanamdhahara sawa???
 
Ina maana walimu wote wanamadaraja sawa kwa uelewa wako siyo..... yaani walimu wote wenye digrii wanamdhahara sawa???
Rejea maelezo yako niliyoyarejea mpk kukueleza hili halafu ukumbuke kuwa toka aingie huyu mheshimiwa hakuna cha nyongeza ya mishahara wala increament kwa walimu mbali na kutopanda madaraja so hali ya mshahara wa mwl upo stagnant usisahau kuzingatia kuwa tofauti ya kiwango cha mshahara kwa madaraja tofauti kwa walimu ni kidogo sana yaani mfano mwenye E1 hawezi kujigamba sana kwa mwenye D1 japo wamepishana umri kazini miaka mingi
 
Mmmm bwana wewe maneno yote ya nini ninachosema dhana kwamba mwl. hakuna anayepata laki si kweli, sasa ukisema mishahara ipo stagnant kwa sasa hilo bado halitengenezi iyo dhana kuwa ukweli.
 
Weee nimekoma kukopa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…