Kuna baadhi ya members humu JF ni wajinga wajinga tu kama wajinga waishivyo.
Binafsi wazazi wangu walikuwa Walimu though by the time Baba yangu nyakati za mwisho wa uhai wake alikuwa akitumikia kama Afsa Elimu Wilaya na alibakisha miaka 4 kufikia ukomo katika ajira ya utumishi wa umma.
Mama yangu ni mstaafu kwa sasa.
Nakumbuka kipindi nahitimu kidato cha sita(2004 SONGEA BOYS) mimi na wazazi wangu tulisigana sana kuhusu kipi napaswa kusomea chuo kikuu make walikuwa na uhakika lazima nitapass. Wote waliafiki niwe mwalimu kama walivyo wao!
Binafsi sikutaka kabisa ajira yoyote iwayo amma lah iwe kama daraja tu! Kweli Mungu ni mwema alijaalia nikapata div II nikawa enrolled kusoma Accounts na mwishowe nikaajiriwa kuwa Assistant Accountant kwenye kampuni ya Wazungu. Baada ya miezi15 nikapiga chini na kurudi mtaani mpaka leo hii.
Ninayo mengi sana ya kuelezea but i reserve them all execept to all who deserves like this guy
Felice1
Mdogo wangu usikatishwe tamaa na watu waoga njoo ntakupa shamba, waterpump n.k bure.