Reality ni Reality, eti kwani reality kwako ni nini? Kama kwangu au kwako au kwa yule ikiwa tofauti ndo itaifanya isiwe reality? Kuwa na ufahamu tofauti au wa kimakosa wa neno fulani hakuondoshi maana halisi ya neno
Reality, tumetoka kuiweka sawa nilipomjibu kwa post namba 225. Najua ameisoma na kuikubali na hajataka tu kuitolea majibu [nimechukulia silence means yes]
Tukiachana na pande tulizoshikilia [za God or no God] kuna kitu kimoja hapa natamani kila mmoja binafsi akichallenge kwa uelewa wake kwa kile anachoona ni sensible:
Hoja kuu: Tunauishi ukweli kulingana na tunachohisi ni kweli binafsi. Yaani mimi binafsi ninaushi ukweli ninaoujua binafsi kwamba ni ukweli na ndio iko hivyo. Na wewe binafsi unauishi uhalisia wako binafsi kutokana na unachokijua kuwa ni kweli wewe mwenyewe. Mambo ya relativity.
Mfano 1.a. Yule anayeamini ukweli wa maisha baada ya kifo basi akifa ataendelea kuishi katika namna sambamba na alivyoamini. Huyu ameamini katika
uhai
1.b. Na yule aliyeamini kuwa hakuna lolote la ziada ukweli ni mnyama akifa kila kitu kinasambaratika na kuwa viinilishe kwa wanyama wengine basi akifa atapata sambamba na ukweli wake binafsi. Huyu ameamini katika
kifo
Mfano 2.a Yule atakayeamini kuwa ukweli ni tunaishi katika mazingira ya hatari ya, wizi, uonevu, magonjwa na vita ni vitu vya maisha ya kawaida na vingi kuliko hali ya amani basi kila kitu chake kitaitikia kwa kujiweka mkao wa vita mbeleni. Atajikusanyia bima ya rasilimali nyingi zaidi physically. Na kimwili atajiwekea bima ya rasilimali muhimu kama mafuta[nishati] na protini kujiandaa na vita inayokuja.
Na ikitokea akaamini kuwa sio hatari tu bali tayari tumo katika vita, iwe ni kuchumi, kiroho, kisaikolojia, familia, kazini etc. Basi tutashuhudia akiwa na nishati ya kutosha mwilini ili apambane sasa hivi. Namaanisha sukari. Mfano wake ni bosi wa wastani[CEO] anayeongoza kampuni kubwa yenye faida kubwa na hatari kubwa zaidi ya kufilisika ni kwa nn wanakuwa na vitambi/sukari?
2.b. Kinyume chake atakuwa ni jamaa anayeamini kwamba tunaishi na watu wa amani na upendo zaidi kwamba wengi ni wa upendo kuliko wa vita na mimi. Basi huyu mwamba hata hajiandai na rasilimali zozote za kimali binafsi physically. Na hasahasa kimwili hajiandai kwa kujirundikia mafuta[nishati] wala maprotini mwilini. Mfano ni rastamani wa wastani mwenye imani ya kirasta kwa nini wanakuwaga wembamba?
Mfano wa kwanza tuachane nao kutokana na asili yake utatusumbua. Naomba muuchallenge huu mfano wa pili. Ila nahisi hapa naharibu uzi ngoja nikipata muda niuanzishie uzi wake. Ila nipeni challenge ili nijipange vizuri.