Wanabodi,
Sisi binadamu tumeumbwa na uwezo tofauti wa uelewa kuanzia kwenye kusoma maandishi hadi kwenye kusikiliza na kuelewa.
Kwe kusoma maandishi utaalamu wa kubaini psychological state of a writer wakati anaandika, unaitwa graphology, zamani kwenye barua za kuomba kazi sehemu nyeti, waombaji walitakiwa kuandika barua kwa mkono, na wataalamu wa graphology, walizipitia barua hizo na kuamua wamuite nani kwenye interview.
Wataalamu wa kubaini genuineness ya kauli, kama mtu akitamka maneno fulani yanatoka moyoni au mdomoni tuu inaitwa intuition, hii intuition kila mtu anayo, ila wanawake wanakuwa more sensitive kuliko wanaume.
Ukimtamani msichana mrembo kwa tamaa tuu za mwili ili kumtumia, yaani lust and infatuation, utamwambia "I love you" na mtu ukimpenda msichana huyo kwa upendo wa kweli, true and genuine love, pia utamwambia "I love you"
Kati ya wawili hao kuna mmoja ni mkweli na mmoja ni muongo, huyu mrembo anayependwa, how will she know, kama anapendwa kweli au anatamaniwa tuu atumike na kutoswa?.
Kitu kinachoitwa female intuitive kitamhulisha huyu mwanamke nani ni mkweli na nani ni muongo.
Utabaini kwa kusikiliza sauti kutoka ndani yako, yaani listening to yourself ili usikie, the voices from within, the voices from inside by listening to yourself.
Kutamka kitu kinachotoka mdomoni na sio moyoni kinaitwa paying lip services, unapofika mwaka wa uchaguzi wanasiasa wengi wanazungumza mengi kutoka mdomoni tuu na sio moyoni. Wanazungumza kile ambacho wananchi watapenda kusikia hata ikibidi kutoa ahadi za uongo ili kupata kura.
Elimu ya kufanya uchambuzi wa kauli za viongozi kama wanasema kweli au just paying lip services, inaitwa psychoanalysis scrutiny ya baadhi ya kauli za viongozi wetu.
Mimi ni miongoni mwa wana jf wachache ambao from time to time, huwa nawaletea psychoanalysis scrutiny ya baadhi ya kauli za viongozi wetu.
Leo nimeisikia kauli hii
"Mimi ni mwenzenu hapa, sijabadilika ni yule yule "KaJoni". Kauli hii japo ni maneno machache simple, lakini yamebeba maana kubwa sana, hii kauli ni kutoka moyoni, ambayo inaonyesha humbleness, simplicity and down to earth ambayo ina maana kubwa sana kwa mustakabali wa nchi yetu.
Kufuatia baadhi ya makabila kuwa na mijitu yenye miili mikubwa, mijitu ya miraba minne, akitokea mtu mwenye umbo dogo, jina lale linatanguliwa na neno "ka", "kapasiko", hivyo zamani enzi za utotoni, udogoni, kule kijijini Chatto, kumbe rais Magufuli alikuwa anaitwa "KaJoni" kujilisha kuwa jina lake ni Joni, lakini kutokana na kuwa na umbo dogo akawa anaitwa KaJoni.
Mtu anayukuwa kwa kuitwa kwa prefix ya neno ambalo ni deamining kuonyeshea udogo au kudogoshwa akiukwaa ukubwa hadi kuwa ni rais wa nchi....
Kwa muda mrefu humu mimi nimekuwa nikichambua baadhi ya kauli za viongozi, kwenye nzuri nazipongeza na mbaya nazikosoa.
Sikiliza kauli hii
Kauli hii niliyousikia leo, ya "Mimi ni mwenzenu hapa, sijabadilika ni yule yule "KaJoni", ni kauli yenye maana kubwa sana ya self realization of going back to his roots. Japo rais Magufuli alikuwa akizungumza na Wana Chato, kuwaeleza kuwa japo kwa sasa mimi ni rais wa JMT, ni mtu mkubwa sana, mwenye nguvu nyingi na mamlaka makubwa kama rais wa nchi na Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, lakini kwa nyinyi wana Chato, mimi ni mwenzenu yule yule KaJoni, huu urais wa JMT, vyeo, madaraka, mamlaka, ni vitu vya kuja tuu na kupita, lakini mimi ni yule yule KaJoni ka Chato.
Katika baadhi ya analysis zangu kwa kauli za viongozi, niliwahi kusema baadhi ya viongozi wana kauli za kujiinua mno, kauli hizo za kujiinua zilizoanzia juu, zikapelekea viongozi wa chini nao kujiinua wakiwemo ma RC hadi vi DC navyo vimejiinua hadi masikio kutaka kuzidi kichwa kwa kuongea kwa vitisho, ukali, kugomba na kusweka watu ndani ikiwemo kutukama watu hovyo hata waliowazidi umri.
Kitendo cha rais Magufuli kuwaeleza wana Chato, yeye ni yule yule KaJoni, inatuma ujumbe mzito wa kujishasha, humbleness, being down to earth, na kuongea kwa humility ambazo changes for the better.
Mwelekeo wa kauli kama hizi mwaka wa uchaguzi, they are expected, kwasababu huu ni mwaka wa viongozi kuwarudia wananchi kujinyenyekeza kuombea kura, wanasiasa wenye kauli za maudhi na majigambo ya jeuri ya mamlaka, wanapojinyenyekeza kuomba kura, ndiko paying lip services kwenyewe, lakini kwa kauli hii ya rais Magufuli, mimi kwa kuisikiliza nimeibaini, kuwa ni bonafide genuine imetoka moyoni na sio lip services, hivyo haitegemewi mtu ambaye ni humble na down to earth akaja kujiinua tena na urais kumpanda kichwani,
One KaJoni, always KaJoni
Hongera rais Magufuli, kujishusha kutoka Joni hadi KaJoni, utabarikiwa sana na Tanzania itabarikiwa.
Pasaka Njema
Pasakali.
Rejea za kauli mbalimbali za viongozi
Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!. - JamiiForums
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais Magufuli!, Alimaanisha Nini?!. - JamiiForums
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje? - JamiiForums
Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni kosa la nani kati yake na aliyetoa kauli hii? - JamiiForums
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba! - JamiiForums
Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?. - JamiiForums
Awamu ya tano: Kuweni Wakali, msionee! Tangulizeni utu na ubinaadamu kwanza! - JamiiForums