"Mimi ni Mwenzenu Hapa, Sijabadilika ni Yule Yule "KaJoni" - Ni Maneno Simple, Humble and Down to Earth Yenye Maana Kubwa!

Yap amwombe msamaha lisu kwa Yale aliyotaka yamtokee mungu akaepusha. pia amlipe stahiki zake zote, aombe msamaha kwa kumnyanganya ubunge kwa bila,

kisha amkaribishe nyumbani, amuhakikishie ulinzi ili arudi nyumbani aungane na familia ndugu na marafiki zake
 
2020 mwaka wa uchaguzi huu kingine naomba pitia comment moja moja utapata jibu kingine unaic kwa nn kila siku chuki inazidi kuwa kubwa juu yke wivu wa kike km mzee Mkapa alivyosema au Kuna tatizo Gani kubwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh..

2 mzunguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kutumia prefix ya ‘Ka’ kwa maana ya kudogosha/kupunguza ukubwa wa kitu/ mtu na labda toka zamani akiwa bado mdogo mtu anaambiwa hivyo inaweza pia ika muathiri ki saikolojia mtu ktk makuzi yake kwa ndani yake na ita onekana katika matendo yake pindi mtu huyu akipata nguvu fulani na hasa za madaraka na uchumi na ataonyesha sasa yeye sio mdogo/dhaifu na akiamua kutumia vibaya ili kufidia dhihaka hiyo ya udogo/udhaifu wa toka akikua kuna maamuzi yake yatakuwa ya kushangaza either mazuri sana au mabaya pia maana hisia pia ndo zinatangulia zaidi kwa sehemu kubwa
 
Tabia moja inayomtofautisha sana huyu na wengine wote waliomtangulia ni hii ya 'ubinafsi wake.'

Kila mara anataka watu wamwone katika mwonekano anaotaka yeye wamwone, au wamfanyie.

Hakuna kiongozi yeyote aliyewahi kuwa anajitangaza yeye ni hivi, au vile, au akiomba afanyiwe hiki au kile

Hii tabia inayo tafsiri yake kiisaikolojia.

Mara nyingi kujinyenyekesha huko anakutumia tu kwa mda, huku kiuhalisia akifanya mambo mengine kinyume kabisa na hicho anachojifanya kionekane.

Hili ni tatizo, na hakuna mtu wa kumwambia kuwa watu wanajua yeye alivyo, kwa hiyo aachane na hadaa zilizo wazi.

Lakini nisiwe mgumu kwake. Inawezekana sana kwamba moyoni anataka na anatamani awe kama hivyo anavyotaka watu wamwone kuwa ndivyo alivyo kiuhalisi, lakini kimatendo inamuwia vigumu kabisa kuyaishi hayo anayotamani kuwa.

Hata walevi wa pombe waliopitiliza na wale wa madawa ya kulevya, hujutia sana hali zao hizo nyakati mbalimbali, na huahidi kuachana nazo, lakini nguvu ya kuyashinda hayo maulevi inakuwa ni hafifu.

Sitaki huu mfano umhusu yeye, lakini hata wagonjwa wa akili (vichaa wa aina fulani); hali hii pia huwapata sana, wanakuwa kama wana 'personalities' zaidi ya moja. Inawezekana naye akawa huko?
 
Pasco!.
Hongera sana! Unauwezo mkubwa na mzuri wakuandaa na kuandika Andiko!
Uishi maisha marefu japo una umri zaidi ya 50+.
Post zako zimejaa mafunzo na iliuzielewe lazima uwe na akili😂😂😂.

Sijui ni meandika kutoka moyoni au mdomoni?
 
KAJONI ...ahaaa , samahani Pascal Mayalla , nataka Kujua nawezaje kama neno mtu analoongea linatoka moyoni.
Mimi nijaribu kusaidia, lakini mwenye jibu kamili huenda atakuja baadae kukujibu.

Huyo huyo anayetaka aonekane kuwa neno lake linatoka moyoni atakuonyesha alama uamini. Mara nyingi ni alama za kimwili.

Sasa basi, hebu jaribu kuiangalia hiyo video vizuri tena uone mwili wake ulivyokaa anapoyaongea maneno hayo., na hata sauti yake inavyotoka akiyasema.

Swali ulilouliza:"nataka kujua nawezaje kama neno mtu analoongea linatoka moyoni." Yeye atakuonyesha alama hizo, ni juu yako kuzisoma na kuziamini au kuzikataa.

Hebu na mimi nikuulize swali mkuu 'Mshumaa_Tz', ulishawahi tongoza demu?

Haya bwanah, hata kama ukiona swali langu ni la kipuuzi, lakini imenibidi niulize! Ikikupendeza, utanijibu kwa ukweli; lakini nitajua vipi?
 
Unafiki wa kiwango cha lami
Muuigizaji tu
Swali mbona amezeeka haraka sana nini shida?
Afya iko
Amechoka akili mwili na roho dah!
 
Paskali, hata vi DC vinapokuwa kwenye "Chato zao" navyo bila shaka vinakuwa "KaJoni"!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…