Mimi ni mzaliwa na raia wa Tanzania bara nataka kuwa raia wa Zanzibar, je inawezekana? Nifuate taratibu zipi?

Ukienda Zanzibar leo hii huwezi miliki ardhi. Lakini ukienda sehemu nyingine yoyote tz bara unaweza kumiliki ardhi
Huu muungano umekaa kinyonyaji zaidi. Sijui katiba mpya itaweza kutupatia mabadiliko kwenye huu muungano feki?

Wao Tanzania ni nchi yao na vilevile Zanzibar ni nchi yao. Sisi Tanzania bara ndo nchi yetu kule kwao Zanzibar sisi kama wageni tu.
 
Saa100 alikotokea huwezi kwenda huko Upewe uraia, Yeye yuko Huku ni Raia kwa kigezo gani?
 
Huu muungano umekaa kinyonyaji zaidi. Sijui katiba mpya itaweza kutupatia mabadiliko kwenye huu muungano feki?

Wao Tanzania ni nchi yao na vilevile Zanzibar ni nchi yao. Sisi Tanzania bara ndo nchi yetu kule kwao Zanzibar sisi kama wageni tu.
Nikikumbuka neno Muungano huwa ninasema bora mwalimu alikufa mapema.

Ulafi wake wa madaraka aliingiza nchi gizani.
 
Mwanzo nilikuwa naona kama Zanzibar wanatunyonya sana Tanganyika ila kwa miaka miwili sasa tangu nimekuja kuishi hapa kweli nimegundua wazanzibar wanamaisha magum sana.

Bidhaa zote wanazotegemea toka Tanganyika bei zake ziko juu sana kama mazao ya chakula

Chukulia mfano hizi bidhaa bei ya Tanganyika na Zanzibar
1. Nyama - Tang 8,000 & Zanz 12,000
2. Bia za kawaida - Tang 1,500 & Zanz 2,000
3. Sabuni ya unga - Tan 1,000 & Zanz 1,200
4. N.k

Kwa biadhaa zinazotoka ughaibun mfano za Electronic, Magar, nguo bei zake ziko chini kulinganisha na Tanganyika.
 
Mimi ni mzaliwa na raia wa Tanzania bara nataka kuwa raia wa Zanzibar, je inawezekana? Nifuate taratibu zipi?
Wanakupa ukikaa miaka 3 mfululizo kwa mujibu wa katiba yao basi una qualified kuwa mzanzibar.
 
Zanzibar Wana sheria zao tofauti na bara,wazanziba ruhusa kumiliko ardh bara ila wabara si ruhusa mpk Kwa kibali maalum
Ikitokea nikawa Rais haki vile nawatema hao wanyonyaji
 
Muungano unawabana sana Zanzibar kuwa na sera za kujitegemea kuhusu suala zima la Uchumi ambalo ndio litakayoikomboa Zanzibar kiuchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…