MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Huyu kocha ni mtu wa hatari sana, katika vitu nafurahishwa navyo ni pale ninapoona 5imba hawana mpango naye, Ila katika makocha wajuzi na hatari hususan kwa Ligi yetu ni Juma Mgunda a.k.a Mzee wa acha boli litembee, mzee wa pira biriani. Huyu jamaa akiachiwaga timu mfano pale alipofukuzwa Tinyo, alikichafua utadhani sio ile 5imba ya Tinyo😀 akamuibua Edwin Balua sijui kutoka wapi huko, hakupoteza hata mchezo mmoja, alituumiza sana vichwa 😀 hana woga sio juu,kati,mbele anakichafua tu!
Anajua sana kuwatumia wachezaji kulingana na weakness na strength zao, alafu sio kocha wa majina.Hawa ndiyo wale makocha unampatia pilipili na vitunguu unakuta ametengeneza kachumbari safi 😀
Wapinzani bado hawajalitambua hili, Jambo linalotufurahisha mno! Hata pale kikosi cha Taifa stars nina uhakika mchango wa mwamba ni mkubwa sana.