Mimi Nimeshajiandaa kusikia haya. Wewe je?

Mimi Nimeshajiandaa kusikia haya. Wewe je?

Trimmer

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
2,443
Reaction score
4,007
Kutokana na kelele za walio wengi huku mitandaoni na jinsi tunavyojua kuwa Mama amekuwa ni wa kusikia sana habari za mitandaoni nategemea na binafsi nimeshajiandaa na haya machache kutokea.

1. Kuanzishwa tena kwa mradi wa bandari ya Bagamoyo ambao tunajua kuwa moja ya masharti yake ni kuwa hatutakanyaga pale kukusanya kodi kwa miaka 35.

2. Kusitishwa kwa mradi wa umeme bwawa la Rufiji ambalo lingezalisha zaidi ya Megawatts 2100.

3. Kuuzwa ama kukodishwa kwa ndege zote za ATCL

4. Mwendo wa kusua sua wa mradi wa reli mpya treni ya umeme

5. Madawa ya kulevya kuuzwa kama pipi mitaani

6. Kutokuwa na Waziri au naibu Mawaziri kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita
 
Kwa jinsi ulivyohusisha point namba 6 katika bandiko lako umeonesha wewe ni wa kundi gani

Kwa unyenyekevu mkuu tumekubaliana na maandalizi yako na hakika kimsingi tunakutakia pumziko jema
 
Nimejiandaa kutosikia tena watu wakitekwa, nimejiandaa kutosikia watu kubambikiwa kesi, nimejiandaa kutosikia maiti zimeokotwa kwenye viroba ufukweni, nimejiandaa kutosikia raisi anajijengea uwanga wa ndege, nimejiandaa kutosikia wakulima kama wa korosho wakidhulumiwa.
 
Mama aruhusu matumizi ya Bange na Mirungi ili Maafsaa wake wakimbizane na Mazungu ya Unga.

Huwezi kuwafunga Watanzania miaka 30 kwa kuvuta Bange wakati wakiwa Magereza wanaipata kwa bei nafuu au kwa Kulawitiwa

Sanity must return.
 
Pole sana. Kama upo kwenye ripoti ya CAG jiandae kwenda jela au kuzitapika/kuziharisha hela ulizoiba.

Usimtishe mama na kesho anaenda kwa Museveni kuchukua mbinu za kuwashughulikia watu kama nyie!
 
Hiyo #5 natamani ianze hata sasa ( leo ) kwani itasaida sana tu Kukuza Uchumi kama ikifanyika Kimkakati.

Kuna Watu mnadhani hii Biashara ni mbaya Ulimwenguni kwa Ufafanuzi mbovu mliopewa na Watu Majuha.

Hakuna nchi Kubwa na Tajiri duniani ambazo hazitumii hii Biashara katika Kukuza Uchumi wake hasa katika Kuikusanyia Kodi yake ( japo inafanywa Kisiri ) mno ili hizo nchi ziepuke lawama kutoka kwa Jumuia za Kimataifa.

Ambacho kingefanyika Tanzania ni kuruhusu tu yapite nchini kama Transit kuelekea Kwingineko hasa South Africa, Nigeria, Msumbiji na huko abroad and overseas pia ila Serikali ikusanye Kodi yake Kubwa hapo ambayo itatumika katika Kuboreshea Huduma zingine za Kijamii.

Ni Unafiki mkubwa Kutaka Kuhalalisha Bangi hala Dawa za Kulevya tunazipinga kwa Nguvu zote. Kwani zote hizi si ni Dawa tu za Kulevya?

Nawapongeza Uganda ( Nchi ) wao wamesharasimisha Kilimo cha Bangi ili baadae wawe wanaichakata vyema na Kuiuza huko Ulaya, America na Asia ambako inasaidia sana katika Utengenezaji wa Dawa ( hasa antibiotics ) na nyinginezo.

Cha kufanya tu kwa Tanzania ni kuhakikisha Udhibiti wake ( hasa kwa Raia ) wake kuwa wasitumie Uraibu huu wa Unga ( Ngada ) ila waruhusu ipitishwe tu na Wachukue Kodi ( Pesa ) yao.
 
Viporo vya mikate mikavu unayofakamia, kuparamia na kubugia matokeo yake ndio haya unasikizia huku unaqunyer
Dah we jamaa kama ulisoma shule ya bweni utakua ulikua muhifadhi mzuri sana wa vtafunwa[emoji23][emoji23]
 
Kwa jinsi ulivyohusisha point namba 6 katika bandiko lako umeonesha wewe ni wa kundi gani

Kwa unyenyekevu mkuu tumekubaliana na maandalizi yako na hakika kimsingi tunakutakia pumziko jema

wewe ni mchagga gang
 
Uhuru wa maoni hata jamii forums mods hawafuti threads hovyohovyo....Kikundi cha wasiojulikana kutoweka, magazeti ya musiba kufilisika,nyuso za furaha na matumaini kurudi kwa Watanzania.
 
Kutokana na kelele za walio wengi huku mitandaoni na jinsi tunavyojua kuwa Mama amekuwa ni wa kusikia sana habari za mitandaoni nategemea na binafsi nimeshajiandaa na haya machache kutokea...
Serikali kurudi Dar es salaam
 
Serikali kurudi Dar es salaam

Kutokana na kelele za walio wengi huku mitandaoni na jinsi tunavyojua kuwa Mama amekuwa ni wa kusikia sana habari za mitandaoni nategemea na binafsi nimeshajiandaa na haya machache kutokea...
Nadhani una mawazo kama ya mfalme juha sio kosa lako.

Kwanza hiyo namba mbili ya mradi wa umeme tayari PM ameshatembelea mradi na ameshawahakikishia watanzania wote kwamba mradi upo asilimia 46 na mpaka 2022 tutaanza kuzalisha umeme na kwa kuongezea amesema bado tutaendelea kutumia fedha za ndani kuukamilisha huo mradi, so hiyo ifute akilini kwako.

Pili, kuhusu Mawaziri wa kutoka Kanda ya ziwa umechemka, Kalemani, Bashungwa, Dotto Biteko etc bado wapo wapo tena ni Mawaziri kamili kwenye Serikali hii ya sita.

Hayo mengine lazima yafanyike msitake tuendeleze utawala wa kijuha simply mliaminishwa ujinga kwa maslahi ya mtu mmoja na genge lake. Hii ni nchi sio ukoo.

Mnatafuta vijimaneno vya kuteteresha utawala huu kwa sababu zenu binafsi simply mlishaona mnapendelewa kipuuzi. Hii ni nchi yetu wote, na maendeleo lazima yaende kwa uwiano sawia sio kujenga mavitu yasiyo na msingi kama ile airport ya vichakani kule.
 
Back
Top Bottom