Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Ana andika, Robert Heriel
Mtibeli
Mimi ni miongoni mwa wale Watu àmbao wakati nilipokuwa mwanafunzi sikuwahi kuibia mtihani tangu naanza Shule mpaka namaliza Chuo Kikuu kwasababu nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wa kutegemewa na ambao wanafunzi wengine walikuwa wakihitaji msaada wa Majibu kutoka kwetu. Sikuwa kipanga lakini pia sikuwa Kilaza. Ni wale wanafunzi wa kiwango cha Kati ambao tupo karibia sekta zote.
Tabia yangu ya kusaidia wengine wala haikunipa shida na nilikuwa najivunia sana kusaidia wengine kwa hali na mali. Kimawazo na hata kifedha kama nikiwa nazo kwa wakati husika nikiombwa.
Waliokaa karibu na mimi hunijua kama Mtu mwema 😉 mwenye Roho safi, nisiyehitaji ugomvi na Mtu, mpenda upatanishi, Mpole na Mtu ninayependa wengine wafurahi.
Nilijua tabia yangu ni kusaidia wengine lakini sikujua kuwa kumbe sio kwa kîla kitu na kîla jambo, mpaka siku nilipopewa MTIHANI fulani na baadhi ya wabongo ndipo nikajua kuwa mimi sipo vile nilivyokuwa najichukulia au vile wanaonizunguka wanavyonichukulia.
Mtihani huo, upo hivi:
Tayari nimekua Mkubwa, Shule nimemaliza, Sasa natakiwa kujitegemea na nisiwe mzigo Kwa Mtu yeyote Yule. Zaidi napaswa kusaidia Wazazi, ndugu na jamaa na Taífa Kwa ujumla.
Piga Akili wee nini chakufanya, nikaona fursa kadhaa. Mojawapo ni fursa ya kuuza Dagaa wa kukaanga WA Mwanza.
Nikaanza hiyo biashara baàda ya kupata chimbo Bora lenye bei nafuu Kabisa, ambao nikiuza napata faîda Nono. Kuhusu Soko siô tatizo Kwa sababu Taikon NI mtu WA mitikasi na ninajulikana Kwa kiwango fulani hivyo kupata wateja kwangu siô shida Kabisa.
Fanya biashara wee! Uza wee pata faîda wee!
Sasa Siku Moja akanipigia Simu MTU mmoja, baàda ya kuwasiliana akaniambia yeye naye anataka Kufanya biashara ya Dagaa, Mimi nikajua NI mteja bhana. Hivyo lugha ya kibiashara ilizingatiwa vilivyo.
Yule Mtu akaniambia, anataka nimsaidie kumpa location ya Mahali ninapochukulia Mzigo wa dagaa. Dadeki!😃😃
Hapo ñdipo nikajua kuwa kiwango changu cha Kutoa msaada hakipo kîla sehemu.
Kwa kweli Hapo nilikubali kuonekana Nina Roho mbaya. Uwezo wa kumpa hiyo tàarifa ninayo. Yeye mwenyewe akaniambia hata Kwa kumuuzia hiyo tàarifa yupo tayari. Na akataja kiwango cha pesa. Siku hiyo ndiyo nikapata uzoefu mpya ndàni ya moyo wàngu kuwa Mtu akikuomba msaada n unauwezo WA kumpatia huo msaada jinsi Moyo unavyokuwa.
Nilishindwa Kwa Kwèli. Nilikuwa tayari kuwagawa wateja hasa wale ambao niliona wanamitaji midogo lakini Kamwe sikuwa tayari kugawa Siri ya Jeshi, Siri ya chimbo.
Hapo ñdipo nikaelewa ule usemi usemao, MTU hawezi kukupa Siri ya Wapi anapata Pesa yake.
Yaani Taikon au Watu weñye maneno mengi wanaweza kuandika hata Biblia nzima lakini hata Siku Moja hawezi kuweka Siri ya mafanikio yake hata Kwa sentensi Moja tu.
Ukiona Mtu anakupa Siri ya mafanikio yake jua anasiri nzito kuliko hiyo aliyoitoa.
Mimi Acha nipumzike
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Soma:
==> Tujadili Maisha: Ni kweli Watu wenye roho nzuri hawafanikiwi kimaisha wakati wenye roho mbaya wanatoboa Kirahisi?
==> Masikini wana chuki na roho mbaya sana