Mimi sigomi, siandamani, na nitafungua biashara yangu kama kawaida hiyo tarehe 15/5/2023

Mimi sigomi, siandamani, na nitafungua biashara yangu kama kawaida hiyo tarehe 15/5/2023

mahindi hayaoti mjini

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2022
Posts
2,120
Reaction score
2,709
Sababu zangu kubwa za kutokuunga mkono huu mgomo wa wafanyabiashara ni nyingi, ila nitataja chache tu

1-Sie tumepigwa faini sana na hakuwepo wa kututetea, leo wamebanwa wakubwa huko wanataka support yetu, si sahihi

2-Hivi kuna kipindi wafanyabiashara waliteseka kama awamu iliyopita? Mbona hatukusikia mgomo wala maandamano? Nahisi dini au siasa inatumika hapa

3-Kwanini zisifanyike juhudi za maongezi kwanza?

4-Sie wengine hata hicho chama cha wafanyabiashara hatujui hata ofisi zao zikwapi

Ushauri
Wafanyabiashara tulipe kodi kwa maendeleo ya inchi yetu

Angalizo
Kwa kuwa nitakuwa nimefungua biashara yangu basi mkinitumia wahuni kunifanyia fujo mjue japo mmoja nitakufa nae

Usiku mwema
 
Sababu zangu kubwa za kutokuunga mkono huu mgomo wa wafanyabiashara ni nyingi, ila nitataja chache tu

1-sie tumepigwa faini sana na hakuwepo wa kututetea, leo wamebanwa wakubwa huko wanataka support yetu, si sahihi

2-hivi kuna kipindi wafanyabiashara waliteseka kama awamu iliyopita? Mbona hatukusikia mgomo wala maandamano? Nahisi dini au siasa inatumika hapa

3-kwanini zisifanyike juhudi za maongezi kwanza?

4-Sie wengine hata hicho chama cha wafanyabiashara hatujui hata ofisi zao zikwapi

Ushauri
Wafanyabiashara tulipe kodi kwa maendeleo ya inchi yetu

Angalizo
Kwa kuwa nitakuwa nimefungua biashara yangu basi mkinitumia wahuni kunifanyia fujo mjue japo mmoja nitakufa nae

Usiku mwema
Wasaliti wako kila sekta

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Ukigoma utakosa hela mzee fungua duka lako

Iko chama special kwa wafanya biashara wakubwa kama wakina mo ndio wanakutana lakini sio ninyi wa wakujikongoja
 
Nakupongeza kwa uamuzi bora na sahihi, usifuate mkumbo utakaokutesa na likitokea la kutokea asiwepo wa kukusaidia wala kukutetea. Tanzania fanya kila kitu kwa akili, hakuna wa kukusaidia wakati wa shida na utaonekana mjinga wakati huo
 
Huyu sio mfanyabiashara! Atakuwa ni TISS anajarbu kumoderate jambo humu😂😂
 
Ukigoma utakosa hela mzee fungua duka lako

Iko chama special kwa wafanya biashara wakubwa kama wakina mo ndio wanakutana lakini sio ninyi wa wakujikongoja
Sahihi kabisa, tukibanwa sie wao hata habari hawana, sasa wamebwanwa wao wanatafuta support kwetu wadogo, tumeshtuka hatudanganyiki, lipeni kodi kwa maendeleo ya inchi
 
Nakupongeza kwa uamuzi bora na sahihi, usifuate mkumbo utakaokutesa na likitokea la kutokea asiwepo wa kukusaidia wala kukutetea. Tanzania fanya kila kitu kwa akili, hakuna wa kukusaidia wakati wa shida na utaonekana mjinga wakati huo
Umenena vyema sana
 
Sasa wewe ulishawahi kupanga maandamano na ukagomewa. Hao wenzako wameanzisha mwendo wa mgomo na wewe organize ili mgomo mwingine upatikane shughuli ianze.
 
Anyways, sijaona tangazo wala habari ya huu mgomo, anyone anaweza nipa briefing.
 
wakigoma wenye maduka sisi wa machinga tuendelee kuuza kama kawaida tutumie fursa maana wakati sisi tunalia wao walichelewa kulia kupokezana
 
Back
Top Bottom