Mimi sio kungwi ila ni mwanamke, ichukue hii

Nimezaliwa Makete, Mwakauta. Nikaishi Zambia, Njombe, Makambako, Mafinga.

Nimeishi Mwananyamala, Temeke, Kigamboni, Kawe, Makumbusho, Tegeta, Masasi, Dodoma, Korogwe na sasa nipo Kondoa.

Na sijawahi kukutana na pattern ya OP.
Umeishi sehemu nyingi Sana mkuu, ndomana unaongea mambo mengi Sana bila kujua tukujibu nini?
 
Nimezaliwa Makete, Mwakauta. Nikaishi Zambia, Njombe, Makambako, Mafinga.

Nimeishi Mwananyamala, Temeke, Kigamboni, Kawe, Makumbusho, Tegeta, Masasi, Dodoma, Korogwe na sasa nipo Kondoa.

Na sijawahi kukutana na pattern ya OP.

Kwahiyo mzee unaijua vizuri mitaa ya amani,luvanyina,namanga,utege,megeo,ilolo,utanziwa etc

[emoji28][emoji28]
 
Hayo maneno unatuambia sisi au mwanamke mwenzako aliyeleta uzi!? Una tatizo la kutojiamini.
 
Nimeshangaa imetoka kwa mwanamke, kutafuta cheap popularity

Kitu nimegundua katika maisha ya sasa. Mwanamke Innocent au bikra zaidi ya miaka 28 ni ngumu kupata mchumba na hao mnaita malaya kwa vile wana uzoefu wa jinsi ya kuwakamata vijana ambao ni Innocent - wanaolewa chap chap. Ndiyo maana kijana akiangukia single mother hachomoki.

Nina mifano miwili ya wanangu, mmoja nilikosea na akaanza haya masuala mapema, akawa chakalamu, mpaka nikamtimua kwangu, hata digrii ya kwanza hana ila ameolewa na mtoto juu.

Kuna wa pili ambaye wote wanalingana, huyu nilijisahihisha nikambana kama mzazi mpaka akamaliza masters, PhD akakataa ati umri umeenda atasoma badaye. Mpaka sasa sijawahi kusikia kuwa ana mchumba. Ni feminist wa kutupwa na kanisani kwa sana kama mtoa mada alivyosema. Kazi kweli kweli maana miaka inasogea (35yrs) na kila wakati akinipigia simu natamani anieleze kuwa nimepata mchumba, lakini hola.

Kusema za ukweli, hivi vitu havina fomula!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…