Mindset za Vijana kuhusu Ajira

Fahami Matsawili

Senior Member
Joined
Mar 8, 2018
Posts
172
Reaction score
153
WASOMI NA WASIOKUWA WASOMI NAOMBENI MNISIKILIZE KWA MAKINI KATIKA HILI [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

[emoji871] Ukimwambia Bakhressa kuwa [HASHTAG]#mihogo[/HASHTAG] ni biashara nzuri atakuita board room muongee vizuri apate kujua vizuri lakini ukimfata msomi mwenye labda masters ya biashara ukamwambia kitu kile kile anaweza kukuona huna idea kichwani.


[emoji871] Nilipoona video ya [HASHTAG]#DiamondPlutnumz[/HASHTAG] akizindua biashara yake mpya ya [HASHTAG]#DiamondKaranga[/HASHTAG] nikawaza tena.

[emoji871] Nikamforwadia mdogo wangu mmoja anasoma "ELIMU YA JUU" kwa sasa. Alipoiangalia whpp nikamuuliza maswali machache [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]


1. Hiyo ni video ya Diamond na karanga?
Akajibu [HASHTAG]#NDIYO[/HASHTAG] BRO
2. Nikamuuliza: Diamond amechuja kimuziki ndo maana kakimbilia karanga?
Akajibu [HASHTAG]#HAPANA[/HASHTAG]
3. Nikamuuliza: Diamond alisomea biashara Chuo?
Akajibu [HASHTAG]#HAPANA[/HASHTAG]
4. Nikamuuliza: Ana akili ya kibiashara?
Akajibu [HASHTAG]#NDIYO[/HASHTAG]
5. Nikamuuliza: Ana hela nzuri nzuri benki?
Akajibu [HASHTAG]#NDIYO[/HASHTAG]
6. Nikamuuliza: Sasa haoni aibu kuuza karanga?
Akajibu [HASHTAG]#HAPANA[/HASHTAG]
7. Nikamuuliza: Kwa nini haoni aibu? Akajibu nadhani sababu ya pale juu NAMBA 4
Nikajisemea: Good.
8. Nikamuuliza: Wewe umesoma kuliko Diamond?
Akajibu: [HASHTAG]#NDIYO[/HASHTAG] KAKA.
9. Nikamuuliza: Unaweza kuuza karanga? ......... (KIMYA)....... ..........
10. Nikataka kuuliza tena ........... nikaona "Typing............"
Jibu likaja: INATEGEMEA

[emoji871] Anyway mpaka hapo nikawa nimeelewa jibu sahihi ni lipi. Kwamba nikimpa huyu msomi option mbili baada ya masomo yake. Moja apate AJIRA pale Azikiwe CRDB, mshahara labda laki 9 kwa mwezi na mkopo nafuu wa kununua IST, halafu option nyingine iwe idea ya kuuza karanga/mihogo/maharage kuanzia zero ipi atachagua?

[emoji871] Nadhani jibu wote tunalo.

Kuna binti mwingine wa "Elimu ya Juu" alikuja kwangu akiomba msaada wa kutafutiwa mahali (sehemu ya kuajiriwa)

[emoji871] Hili ni [HASHTAG]#JANGA[/HASHTAG].
Tuna wasomi wetu wengi ambao wao wanachotaka ni AJIRA TU. Serikali nayo inadhani itaweza kutatua tatizo la ajira kwa a one-sided view.

[emoji871] Kwamba mtu asiye na ajira dawa yake kumpa ajira. Si kweli kwamba hiyo ndo dawa pekee. In fact tuendako hiyo ni wrong solution.

[emoji871] Mfano mdogo ajira za madereva kwa dunia ya leo zinaondoka moja moja.

Fikiria: [emoji871] Siku jiji hili la Dar es Salaam kwa mfano hili likiwa na Mwendokasi kila Kona ya jiji na huko mbali na city centre kote kuanzia Bunju (au Bagamoyo) hadi Mbagala na hadi huko Chalinze.

[emoji871] Halafu treni za umeme ziko
[emoji871] Halafu self driving cars
[emoji871] Halafu drones za kudeliver mizigo kwa wateja (yani uko zako nyumbani labda Bunju unaagiza chakula KFC Posta unalipia kwa M-PESA kinaletwa na drone ndani ya robo saa tu hadi mlangoni kwako)
Hapo mtu aliyesomea udereva ataendesha nini?

[emoji871] Licha ya hayo mambo kukawia yatafika. Lakini hata kabla hayajafika ajira ngapi zipo na nani atapata nani akose.

[emoji871] Wasomi wetu ni lazima waanze kuwaza tofauti na wasomi wa mwaka 1970. Lazima kuwaza option ya kusurvive nje ya mfumo wa ajira.

Wasomi wamefungwa na Elimu zao kama amesomea fani ya Sheria au Sociology basi lazima atumikie hiyo professional yake kumbe anaweza kuwa mwanasheria bado akawa Mkulima au mfanyabiasha akachepuka kulingana na mahitaji ya soko la jamii sio kufungwa na professional yako miaka 3 unasubilia Ajira ya professional yako..

Tatizo wengi wanachotaka ni MSHAHARA tu. Ndo maana wakikutana na wewe utasikia: "BRO NIUNGANISHE BASI HATA KWA RAFIKI ZAKO NIPATE KAZI".

[emoji871] Ndo lugha yao. NIUNGANISHE. Yaani utadhani wewe umekuwa fundi welding... Ukimpa idea nyingine HATAKI.

[emoji871] Ndo maana watu wasio na shule ndeefu ndo wanakuwa matajiri. Si bure. Katika matajiri wote 2000+ kwenye Forbes wenye MBA unaweza kuta hata 10 hawafiki. Na hao wenye hiyo MBA siyo kuwa ndo imewafanya wa excel in business.

[emoji871] Lazima kuwaza kwa mapana. Wasomi hawataki kuumiza kichwa wanataka ready made things. Hii si njema kwa afya ya uchumi wa taifa letu.

[emoji871] Ukitazama [HASHTAG]#DiamondPlutnumz[/HASHTAG] na karanga unashangaa kwa nini msomi akikuona unaanzisha biashara yako anataka umpe tu AJIRA hataki umfundishe afanye.

[emoji871] Makanisani nako wasomi wanaombewa tu wapate AJIRA. Basi. Kweli? Ina maana hakuna MAONO mengine kwa wasomi wetu isipokuwa ajira?

[emoji871] Elimu ya juu kwa vijana wengi imepeleka creativity yao na uthubutu wao CHINI!
So sad!

Sikiliza kijana msomi:
[emoji871] Ni muhimu kuyatazama maisha yako kwa mapana na kwa upya kabisa pasipo kuyahusisha na elimu yako ya darasani kabisa

MUNGU AWABARIKI SANA

[emoji871] Jifunze Kuthubutu tusiwe na kikomo cha kufikiri.
[emoji871] Fikiri hata mara 1000 usiochoke unapoanguka ndo inakuongezea uwezo wa kutatua Changamoto zinazokukakabili.

UNAWEZA WAKATI NI SASA.
 
Wewe juzi ulisifia kilimo leo jingine, Soma gazeti la mwananchi leo kuhusu waliojiajiri kulima mbaazi na hasara wanayopata

Mwananchi tarehe 21 March 2018

Usilaumu bila kutafiti, wewe unauliza maswali juu juu, Kwani tulipeleka madaktari India ili wajiajiri au watusaidie wakirudi kuepukana na magonjwa haya tunayoshindwa kuyafanyia tafiti

Sio kila alienda shule lengo lilikuwa akimaliza afanye biashara wengine tuliwapeleka waje saidia kufanya tafiti za kilimo kusaidia watu wengine

Wewe ni zero brain
 
Hahaaa duu mzee baba inaonekana umeamka na hasira sana leo
 
Point zuri sana nimeipenda
 
Hii nchi haiendelei sababu ya watu kama wewe! Unawasema wenzio je wewe unauza karanga! Utakuta umeajiriwa na una kipato kizuri kwa hiyo unamuona mwenzio fala mjinga!Kufanya kitu chochote inahitaji elimu ya kitu hicho,msingi wako wa kimaarifa na mtaji.Karanga ambazo faida yake ni shilingi thelathini auhamsini unahitaji uwe na umejipanga vizuri sana na mtaji uwe si haba.Shilingi hamsini ili ifike milioni unahitaji kuuza 20000 pcs na sijui masaa mangapi ya kazi> Fikiria sasa mdogo wako anataka ale ,ajenge nyumba ya kuishi ya say 40mil awe na usafiri ,watoto wasome english medium n.k,n,k unamshangaa mdogo wako! Ulichopaswa kufanya kama wewe una mwanga wa hicho unachokisema ni kumsaidia!Kwa nini usianzishe patnership naye ya ,sema 40/60 Yeye apate na wewe upate na kwa kuwa wewe ni guide mzuri lazma atafanikiwa. Otherwise you are just trying to be a smartass! A good teacher never forsakes their weak students!Kwa Diamond ni rahisi anafanya top down approach ,ungemwambia auze karanga kabla hajawa alipo sasa .............................
io
 
Umeeleweka mkuu nitashirikiana na Wangapi message hii ni kwa vijana milioni 17 nchi nzima ambao hawapo kwenye ajira rasmi hata Bakhressa alianza hivyo hivyo kidogo na na ufundi viatu mara ice cream sasa yupo wapi now
 
Umeeleweka mkuu nitashirikiana na Wangapi message hii ni kwa vijana milioni 17 nchi nzima ambao hawapo kwenye ajira rasmi hata Bakhressa alianza hivyo hivyo kidogo na na ufundi viatu mara ice cream sasa yupo wapi now
Unaamini kweli Bakhresa alianza kwa kushona viatu! Seriously! Ulitakiwa kuanza na mdogo wako uliyemzungumzia Charity...........
 
Haaa Haaa [emoji134] comrade kwa hiyo kama zao la mbaazi limeshuka bei na sisi wakulima wa mihogo, Mpunga, Alzeti tuache au wakulima wa katani, Korosho, Maharage, nanasi, matikiti maji, vitunguu maji, Tumbaku, Parachichi, Karoti, Kabichi n.k nao tusambaze hilo gazeti la Mwananchi hao wakulima waache kulima sote tuanze kulalama.....

Hilo gazeti la Mwananchi lini wamechapisha Fursa za kilimo cha Muhogo kuwahamasisha wakulima wetu wachangamkie Fursa. wachina wanahitaji mihogo Tani Milioni 2 kila Mwaka

Hilo gazeti umewahi kuona wanaandika hayo na kuonesha ni aina gani ya mihogo inahitajika na Mkulima akishalima hiyo mihogo amuone nani au kampuni gani inahusika kukusanya hiyo mihogo kwa wakulima Mashambani........

Habari za majanga ndio news kwako na wao ila sio Habari za Fursa na Elimu badirikeni Taifa letu bado linatuhitaji sana kusonga mbele
 
Nyani haoni kundule.
bahati mbaya wote wanao toa ushauri kama huu unakuta wameajiriwa na wanategemea mishahara. Soo sad
 
Ushauri wa mtu kama huyo kaajiriwa ...sema anatafuta sifa tu ..
Akiachishwa kazi miez miwil tu analialia hapa.
 
Utakuwa anafanya shughuli fulani anapata laki 4 na analalamika maisha magumu sijaajiriwa.
Huwa najiuliza hivi wanajua maana ya neno ajira?? Hawajui hukohuko serikalini kuna watu wanapata laki 3??
 
Nilichogundua comment nyingi humu zinaathiriwa na comment ya kwanza. Yan kama wa kwanza atakuwa negative basi asilimia kubwa ya comments zitakuwa negative.

Bibafsi yangu nimemuelewa mleta mada. Regardless na changamoto zilizopo ambazo wengi mnalalamikia but ye amebase kuelezea hali halisi na mindset za wahitimu wao wanafikiri kuajiriwa ndio solution badala ya kufikiri nje ya box. Hakuna kinachofanikiwa bila changamoto na ukifanikiwa bila changamoto jiangalie mbele yaweza kuwa huo ni mtego unaenda kunasa pabaya.

Sasa mtu mwingine ukimwambia afikiri nje ya box unamchanaganya pengine hata hilo box halioni. Na ndio wengi humu JF tatizo lilipo ugumu wa maisha unawafanya kuona kila kitu hakiwezekani pengine kwa kutumia changamoto hizi zilizopo ndio fursa ilipo. Tubadilike jamani lakini nakubali kuwa hatuwezi kulingana maono na uwezo wa kufikiri.
 
Ubarikiwe sana kiongozi
 
So kama wamepata hasa kwenye mbaazi watu wakatafute kazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…