Minyukano CCM: Ushauri wa bure kwa Bashiru na wenzako kokote kule mliko

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana kwa yanayotokea huko CCM kwa wengine kina sisi, hayo ni mambo ya Ngoswe.

Hata hivyo kama binadamu ambapo wengine huwa hawana huruma, wengine tumeumbiwa na roho za huruma. Ashukuriwe mola muweza wa yote.

Ni ukweli ulio wazi kuwa mh. Dr. Bashiru, Pole pole na vigogo wengine mliokuwa vinara kwenye awamu ile, tokea kuondoka kwa mwendazake kama mlikuwa hamjui, tathmini ya utendaji wenu na hata kukubalika kwenu katika jamii ndiyo hii mnayoiona sasa.

Bila ya shaka mtakuwa sasa mmejielewa vyema na pasi na shaka yoyote. Kwamba sasa mambo ni hadharani. Hakuna cha unafiki wala nini. Hii ni timamu kabisa ndani na nje ya CCM.

Ukweli mchungu:

"Ni wazi kuwa hamkuwa mkipendwa wala kukubalika kwenye chama wala katika jamii. Mlikuwa wababe mliopitiliza, mliokuwa mmejisahau. Hamkuukumbuka hata ule usemi wa kuwa - Dunia Mapito."

Kwani ni lini basi mwenye macho alisubiri kuambiwa tazama? Au ni lini afukuzwaye aliwahi kuambiwa toka? Labda kama ni mgeni na imegonga hadi siku ya kumi!

Ukweli mchungu zaidi ni kuwa, enyi machampioni kabisa wa awamu ile katika serikali na katika CCM, hamkuwa mkikubalika kabisa, kiasi kuwa katu hamuwezi kutosha tena kwenye awamu ya sita.

"Ni vipi awaye yote aweze kuwa rafiki wa Mungu na Shetani kwa wakati mmoja? Hii ndiyo changamoto ya wazi inayowakumba sasa."

Si mnamwona wanayemwita katelefoni anavyokuwa kama kanyeshewa mvua?

Muda wa kutumia busara zenu za kisomi ulikuwa sasa, kujiengua wenyewe kwa maslahi ya nchi na chama hiki, kama kweli mlivipenda.

Zaidi sana kama kweli mnadhani mliyokuwa mnayasimamia kwenye awamu ile yalikuwa na mashiko, bora mngefikiria kuanzisha hata chama chenu cha siasa chenye agenda hizo mkapata kuendelea kuzipambania.

Wakuu, kunyong'ong'onyezwa hivi mpaka mnatia huruma hadi lini? Hamjionei huruma wenyewe? Hata hamshauriani wenyewe kwa wenyewe?

IMG_20210328_223958_589.jpg

Mbona mko wengi wa kutosha mkisheheni hadi maaskofu wafufua wafu kwenye hilo ambalo leo linaitwa kuwa ni genge lenu?

Mh. Dkt Bashiru, pole pole na timu yenu, mbona kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi?

Wapiganaji wanasema "Aluta Continua." Kazi inapoendelea, hebu mapambano na yakaendelee!

Ninawasilisha.
 
Bashiru haamini kili hotokea kama kukufurualishakufuruuu.....haamini ukuu Mungu anaona anaota hadi leo change over ( change kota) .....haelewiiii
 
kuna watu walikuwa wanaserereka tu utafikiri wamepanda treni ya mwendokasi, leo katibu mkuu wa chama, kesho katibu mkuu kiongozi utafikiri nchi ilikuwa mali yao binafsi..

Huu ulikiwa muda mzuri kwao kupata tathmini isiyoegemea upande wowote kuwahusu wao.

Kuuvaa ujasiri na hata kuwaomba radhi waliowakosea hadharani ndiyo uliokuwa ukomavu wenyewe.

Walikuwa wamejisahau. Dunia Mapito!
 
Mabibi na mabwana kwa yanayotokea huko CCM kwa wengine kina sisi, hayo ni mambo ya Ngoswe.

Hata hivyo kama binadamu ambapo wengine huwa hawana huruma, wengine tumeumbiwa na roho za huruma. Ashukuriwe mola muweza wa yote.

Ni ukweli ulio wazi kuwa mh. Dr. Bashiru, Pole pole na vigogo wengine mliokuwa vinara kwenye awamu ile, tokea kuondoka kwa mwendazake kama mlikuwa hamjui, tathmini ya utendaji wenu na hata kukubalika kwenu katika jamii ndiyo hii mnayoiona sasa.

Bila ya shaka mtakuwa sasa mmejielewa vyema na pasi na shaka yoyote. Kwamba sasa mambo ni hadharani. Hakuna cha unafiki wala nini. Hii ni timamu kabisa ndani na nje ya CCM. Ukweli mchungu:

"Ni wazi kuwa hamkuwa mkipendwa wala kukubalika kwenye chama wala katika jamii."

Kwani ni lini basi mwenye macho alisubiri kuambiwa tazama? Au ni lini afukuzwaye aliwahi kuambiwa toka? Labda kama ni mgeni na imegonga hadi siku ya kumi!

Ukweli mchungu zaidi ni kuwa, enyi machampioni kabisa wa awamu ile katika serikali na katika CCM. Hamkuwa mkikubalika kabisa kiasi kuwa katu hamuwezi kutosha tena kwenye awamu ya sita.

"Ni vipi awaye yote aweze kuwa rafiki wa Mungu na Shetani kwa wakati mmoja? Hii ndiyo changamoto ya wazi inayowakumba sasa."

Si mnamwona wanayemwita katelefoni anavyokuwa kama kanyeshewa mvua?

Muda wa kutumia busara zenu za kisomi ulikuwa sasa kujiengua wenyewe kwa maslahi ya nchi na chama hiki kama kweli mlivipenda.

Zaidi sana kama kweli mnadhani mliyokuwa mnayasimamia kwenye awamu ya ile yalikuwa sahihi, bora mngefikiria kuanzisha hata chama chenu cha siasa chenye agenda hizo mkapata kuendelea kuzipambania.

Wakuu, kunyong'ong'onyezwa hivi mpaka mnatia huruma hadi lini? Hamjionei huruma wenyewe? Hata hamshauriani wenyewe kwa wenyewe?

View attachment 1771352

Mbona mko wengi wa kutosha mkisheheni hadi maaskofu wafufua watu kwenye hilo ambalo leo linaitwa kuwa ni genge lenu?

Mh. Dkt Bashiru, pole pole na timu, mbona kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi?

Pia Aluta continua. Kazi inapoendelea, mapambano na yaendelee.

Ninawasilisha.
Enzi zao kilichokuwa kinajampa ni tumbo like(Magu)wao walikuwa makalio ambayo ndo spika ya kijampo
 
Mkuu unapiga za uso...hahaaaa
 
Enzi zao kilichokuwa kinajampa ni tumbo like(Magu)wao walikuwa makalio ambayo ndo spika ya kijampo

Ni aibu kwao kuwa wakiwamo kina katelefoni, mparamagamba na wenzao wangalimo wakimtumikia nani?

Jamii haiwataki.

Kujiongeza nako shida?

Hiiiiii bagosha!
 
Huu ulikiwa muda mzuri kwao kupata tathmini isiyoegemea upande wowote kuwahusu wao.

Kuuvaa ujasiri na hata kuwaomba radhi waliowakosea hadharani ndiyo ukomavu wenyewe.

Walikuwa wamejisahau. Dunia Maputo.
Hivi Kalamagamba Kabugi ana hali gani?
 
Back
Top Bottom