Minyukano CCM: Ushauri wa bure kwa Bashiru na wenzako kokote kule mliko

Kipigo kitakatifu cha 2020 bado maumivu mnayasikilizia na haya japungua. Mungu awasaidie mumtunze huyo mmoja wa Nkasi awe mbegu. Bashiru na Pole pole oyeeeeeee.
 
Nimegundua humu tuna watoto wadogo sana ama akili ni ndogo za kuwaza au wavivu wa kufikiria. Bashiru alitolewa kwenye Chama na kupelekwa serikalini. Hakuna namna Bashiru angerudi kuongoza Chama. Samia kampeleka Bungeni. Nini shida hapo? Polepole aliteuliwa kuwa Mbunge. Baada ya uteuzi alikuwa anasubiri mtu ateuliwe kuja kuchukua nafasi yake ya Uenezi. Nafasi ni kwamba Mtu mmoja nafasi moja. Walishatolewa kufanya kazi za Chama. Alikuwa anataftwa katibu mkuu wa chama pamoja na mwenezi. Mbona watu mna nongwa? Wenzio wapo Bungeni na wamekitumikia Chama wamepambana sana. Hata Mungu akiwachukua leo wamefanya jambo na jamii inaona. Wewe unayeandika haya bila kufikiria umefanya nini? Kiufupi kama ni Maslahi Bashiru na Polepole wanapata zaidi kuliko walivyokuwa wanapata ndani ya Chama kama Malipo ya kazi. Tutumie akili muda mwingine. Ni sawa sasa kwa level yangu nianze kumnanga Mbowe wakati Mbowe ka achieve mengi. Ingekuwa unawasema kwenye masuala ya hoja sawz lakini huu udaku unakupunguzia hadhi.
 
Bashiru aliisaliti taaluma yake kisa ni njaa. Sidhani kama anaweza kutoa mhadhara wa kisomi na akaeleweka leo kama zamani. From critical thinker to compromise thinker!
mwenzio anapiga mshiko. Angebaki katika taaluma asingepata hayo. Lakini pia alikuja ku practice politics. Mmuache Bashiru
 
Bashiru, Pole na Magu walipaswa kupigwa pingu, wakaozee jela au kunyongwa. Ni miongoni mwa watu wabaya zaidi waliowahi kutuharibia nchi yetu.
 
Wivu tu....kwani kuserereka namna hiyo alikuwa anajiteua?
Wivu upi, tangu lini mtu ambaye yuko kwenye active politics kwenye ngazi ya katibu mkuu wa chama akateuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi, hizo sarakasi ziliwezekana tu kwenye utawala wa malaika wenu mkuu....
 

Watoto hao unaowaongelea CCM nako wapo? Au hawa nao ni wakubwa wenzio?




Hawa nao je? Ni wakubwa wenzio?




Nyuso zao je? Nazo hazikufumbui lolote?



Ni uzwazwa kudhani mnaweza wadanganya watu wote siku zote. Bashiru, pole pole na genge lao walilikoroga awamu ya tano. Sasa wanavuna walichopanda.

Huu ulikiwa ushauri kwao binafsi. Labda kama wewe ni Bashiru au Polepole au mshirika katika genge lao.

Tumekuwa wazi vilivyo ya Ngoswe (CCM) yatuhusu sisi wengine vipi?

Awamu ya sita haikubaliani na yao ya awamu ile. Kama waliyosimamia yalikuwa na mashiko taabu gani kuendelea kuyapigania?

Pamoja na kutoyaona au kuyafumbia macho yote hayo ninashawishika kukuona kuwa, wewe ni kubwa zima lenye akili za kitoto.

Mwendazake alipenda kusema, "mtanzania wa leo mbona si yule wa jana?"

Au nasema uongo ndugu zangu?

Hiiiiii bagosha!
 
mwenzio anapiga mshiko. Angebaki katika taaluma asingepata hayo. Lakini pia alikuja ku practice politics. Mmuache Bashiru

Kwa hivi:



Atakuwa ame practice politics ki vitendo!
 
Mwacheni Mwl. Balozi Bashiru amalize kwanza majonzi ya msiba wa kipenzi chake. Bado anamachungu. Kidonda hakijapona.
Mimi ukiachia mambo mengine yote ya hovyo aliyoyafanya Bashiru dhidi ya watanzania kwa lengo la kumfurahisha Mwenda zake, ikiwemo kauli yake kuwa watatumia dola kubaki madarakani.

Kubwa zaidi ni lugha na maneno yake ya kejeli dhidi ya Lissu kwa tukio lililompata kwamba eti Lissu anadeka.

Yaani kweli hawa watu kiburi cha uzima na madaraka viliwalevya sana.
 
Bashiru haamini kili hotokea kama kukufurualishakufuruuu.....haamini ukuu Mungu anaona anaota hadi leo change over ( change kota) .....haelewiiii
bashiru ana roho mbaya sana, amenyanyasa sana watumishi wa CCM makao makuu, huku yeye anayejinasabu mjamaa akiwa anapenda rushwa
 
bashiru ana roho mbaya sana, amenyanyasa sana watumishi wa CCM makao makuu, huku yeye anayejinasabu mjamaa akiwa anapenda rushwa

Kwa tathmini kama hizi kwa watendaji hawa wa awamu ile bado hamsikii tu? Wajameni, hamtufai!

Mmekomaa kama luba bado, au mpaka mtumbuliwe au kufurushwa kwa fedheha?

Cc: mparamagamba, katelefoni, bashiri, pole pole na dream team yote inayounda lile genge lenu pendwa la wasukuma uchwara wa imani.

Hiiiiii bagosha!
 
kuna watu walikuwa wanaserereka tu utafikiri wamepanda treni ya mwendokasi, leo katibu mkuu wa chama, kesho katibu mkuu kiongozi utafikiri nchi ilikuwa mali yao binafsi..
Hiyo kawaida,kila zama/utawala kuna watu watapeta wengine wataumia

Ova
 
Bashiru, Pole na Magu walipaswa kupigwa pingu, wakaozee jela au kunyongwa. Ni miongoni mwa watu wabaya zaidi waliowahi kutuharibia nchi yetu.
Leta ushahidi wa uharibifu wao hapa. Naomba ulete hapa wana Jamvi wauone. Hizi zote ni chuki binafsi hizi.
 
Kwani mkuu wale vijana wanaowahamasisha kila leo kujiajiri, kwani wao wanaishi je?

Hawa watu mbona tayari wako vizuri tu?
Na ndio msemo wao huo,wakati wao wanang'ang'ania kwenye nafasi ambazo hawafit, kiufupi hawana uwezo wa kupambana huku mtaani,ni sawa na samaki akitupwa nchi kavu lazima afe
 
Leta ushahidi wa uharibifu wao hapa. Naomba ulete hapa wana Jamvi wauone. Hizi zote ni chuki binafsi hizi.

Mwingine huu hapa:



Ukihitaji mwingine sema. Kukuongezea mwingine "itapendeza zaidi." - Dr. Shika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…