Kwa ufupi sana,
1. Huyu Kigaila anayesema Lissu ni CCM mke wake yuko Bungeni bila baraka za Chama hii kwa akili ya kawaida kabisa inawezekana?
2. Hata Salumu Mwalimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mke wake yuko Bungeni bila baraka za chama lakini jambo hili kwa akili za kawaida kabisa inawezekana?
3. Taifa hili linajua fika Halima na Bulaya ni maswaiba wakubwa wa Freeman Mbowe je hoja kwamba wadada hawa waliapa bila baraka za rafiki yao huyo zinaukweli?
4. Mimi nasema hawa wanawake wanaonewa bure nashauri Mbowe, Mwalimu na Kigaila waadhibiwe kwa makosa haya na Chama kitamke msamaha juu ya hao wanawake wote 19
5. Napendekeza wabunge hawa warudi kundini ili Maisha yaendelee ila hawa Wala rushwa waondoke na Uenyekiti apewe mtu asiye Mbowe.