Lusematic
JF-Expert Member
- Feb 2, 2017
- 12,039
- 11,822
Habari wanajamvi?
Nachukua fursa hii ili tuweze kujadili kwa pamoja hoja husika kuhusu wizara husika kwa upande wa mipango miji kwa nchi yetu ya Tanzania."
kwanza niipongeze Wizara kwa kujitahidi kusimamia utendaji wao japo si kwa kiasi kikubwa.
Kutokana na uzalendo na kupenda mandeleo kupitia sekta tofauti tofauti, Leo ningependa tulijadili hili swala la mipango miji yetu, kiuhalisia wizara husika kama inalega kwa hili swala haswa kwa upande wa kupima maeneo ili jamii ijayo iweze kuishi sehemu yenye mpangilio bora kwani hii itasababisha hata miundo mbinu iweze kufika kirahisi pamoja na huduma nyinginezo muhimu za kijamii.
Tunaona miji inakuwa kinacholeta changamoto bado muendelezo wa makazi holela hata sehemu za makazi mapya ama miji mipya baadhi ya sehemu bado ujenzi holela unaendelea na kuleta shaka kuwa hii hali ya ujenzi holela itaendelea kuwepo miaka na miaka na hii yote sababu wizara husika haijatia nguvu za kutosha kwa kutolea macho hili swala kwa kila sehemu inayoanzishwa makazi mapya na yale ya awali kwa kuhakikisha wanawapa watu utaratibu maalum kwa kuhakikisha nyumba zinakaa kwenye mpangilio.
Hususani ni sehemu ambayo muhanga kwenye suala la ujenzi holela.
Kwa kweli hili swala la kuruhusu kila mtu ajenge atakavyo linaleta changamoto kimakazi, japo ni sawa kila ajenge nyumba aitakayo lakini wizara inabidi isimamie utendaji wao kwa umakini zaidi kwa kuwapa watu mwongozo maalum.
Nawasilisha hoja mezani ili tuweze kulijadili hili kwa pamoja na kutoa ushauri bora kupitia hoja husika.
1. Je, wizara husika utendaji wake unaridhisha?
2.Je kipi kifanyike ili majiji ya Tanzania yaweze kuwa kwenye mpangilio mzuri wa kimakazi....?
Karibuni
#TUIAMSHE WIZARA YA UJENZI NA MIPANGO MIJI