Mipango miji Tanzania

Mipango miji Tanzania

Lusematic

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2017
Posts
12,039
Reaction score
11,822
Habari wanajamvi?

Nachukua fursa hii ili tuweze kujadili kwa pamoja hoja husika kuhusu wizara husika kwa upande wa mipango miji kwa nchi yetu ya Tanzania."

kwanza niipongeze Wizara kwa kujitahidi kusimamia utendaji wao japo si kwa kiasi kikubwa.

Kutokana na uzalendo na kupenda mandeleo kupitia sekta tofauti tofauti, Leo ningependa tulijadili hili swala la mipango miji yetu, kiuhalisia wizara husika kama inalega kwa hili swala haswa kwa upande wa kupima maeneo ili jamii ijayo iweze kuishi sehemu yenye mpangilio bora kwani hii itasababisha hata miundo mbinu iweze kufika kirahisi pamoja na huduma nyinginezo muhimu za kijamii.

Tunaona miji inakuwa kinacholeta changamoto bado muendelezo wa makazi holela hata sehemu za makazi mapya ama miji mipya baadhi ya sehemu bado ujenzi holela unaendelea na kuleta shaka kuwa hii hali ya ujenzi holela itaendelea kuwepo miaka na miaka na hii yote sababu wizara husika haijatia nguvu za kutosha kwa kutolea macho hili swala kwa kila sehemu inayoanzishwa makazi mapya na yale ya awali kwa kuhakikisha wanawapa watu utaratibu maalum kwa kuhakikisha nyumba zinakaa kwenye mpangilio.

Hususani ni sehemu ambayo muhanga kwenye suala la ujenzi holela.

Kwa kweli hili swala la kuruhusu kila mtu ajenge atakavyo linaleta changamoto kimakazi, japo ni sawa kila ajenge nyumba aitakayo lakini wizara inabidi isimamie utendaji wao kwa umakini zaidi kwa kuwapa watu mwongozo maalum.

Nawasilisha hoja mezani ili tuweze kulijadili hili kwa pamoja na kutoa ushauri bora kupitia hoja husika.

1. Je, wizara husika utendaji wake unaridhisha?

2.Je kipi kifanyike ili majiji ya Tanzania yaweze kuwa kwenye mpangilio mzuri wa kimakazi....?

Karibuni

#TUIAMSHE WIZARA YA UJENZI NA MIPANGO MIJI

images%20(1).jpg
 
NI KWANINI NI VIZURI KUPANGA MIJI YETU...?
manufaa ya upangaji. miji
1. Kuweka utararibu mzuri wa kuishi kwa
pamoja.

2.Kutumia vizuri eneo la ardhi lililopo.

3.Kutenga maeneo ya wazi kwa kupumzikia,na pia kwa ajili ya ujenzi wa shule, zahanati na kadhalika.

4. Kuhakikisha kuwa kila eneo linafikika kwa urahisi, linapata hewa nzuri ya kutosha pamoja na mwanga wa kutosha.

5. kupunguza gharama za kupitisha bomba za maji pamoja na bomba za maji
machafu/taka.

6. kuondoa migongano baina ya wakazi wa eneo hilo
 
Ni kweli kabisa mkuu, unajua nchi yetu tumebarikiwa sn, sisi WaTz kwa kweli tumejitahidi kujenga unakuta maeneo mengi hususan kwa hapa Dar es salaam watu wamejenga nyumba nzuri za blocks tofauti na wenzetu katika nchi jirani ambapo unakuta wananchi wengi wana nyumba za mabati au za udongo lkn ss tatizo letu kubwa ni jinc tunavyojenga nyumba zetu, hebu nenda Tandale, Yombo, Buza, Magomeni, Tandika, Karakata, lkn pia hata baadhi ya maeneo ambayo tunayaona km ni uzunguni watu mejenga hovyo hovyo na mipango miji wapo na tunawalipa mishahara na hakuna wanachofanya zaidi ya kuwaacha watu wajenge watakavyo hili jambo halikubaliki na hatuwezi kulifumbia macho.

Hivi karibuni serikali ilitoa idhini watu wawekewe mawe (pegs) katika viwanja vyao ili kurasmisha umiliki wa ardhi kwa maeneo yasiyo rasmi ss kilichonishangaza ni kwamba hao watu wa ardhi badala ya kufuata kanuni na taratibu husika pamoja na kufuata ramani kinyume chake wamefuata wenye viwanja wamejipangiaje, yn mtu eneo lake iko wazi alifuata barabara lkn ardhi wameenda kuweka mawe pale pale alipoishia kujenga mwenye kiwanja yn kwa kifupi hakuna walichofanya cz nilitegemea kupitia urasmishaji wa viwanja wangeweka sawa ukiukwaji wa sheria ya makazi badala yake wameongeza tatizo.

Sasa nashindwa kuelewa je serikali msimamo wake ni upi juu ya ujenzi holela na je imeshindwa kuweka misingi imara juu ya ujenzi wa kufuata ramani? Au serikali haijui umuhimu wa ujenzi wa kufuata ramani?
 
Ni kweli kabisa mkuu, unajua nchi yetu tumebarikiwa sn, sisi WaTz kwa kweli tumejitahidi kujenga unakuta maeneo mengi hususan kwa hapa Dar es salaam watu wamejenga nyumba nzuri za blocks tofauti na wenzetu katika nchi jirani ambapo unakuta wananchi wengi wana nyumba za mabati au za udongo lkn ss tatizo letu kubwa ni jinc tunavyojenga nyumba zetu...
Hiko ndicho kikubwa maana tunasikia tu maneno ila tunataka maneno yaendane na utendaji kwa kufuata sheria itolewe kauli moja tu yenye utendaji.

ili tujue serikali ina mpango gani kuhusu kuzuia makazi holela na ujenzi holela unaoendelea..?!!!!
 
Pendekezo langu ni kwamba serikali haipaswi kulifumbia macho jambo hili km tunataka kuona Tz mpya ya uchumi wa kati, inapaswa kuhakikisha mwananchi hana mamlaka ya kujenga jengo lolote pasipo kupata ruhusa kutoka mipango miji, yn kuwe na utaratibu fulani ambao ikitokea mtu kauvunja basi jengo lake livunjwe pasipo kuwa na huruma yyte.

Mfano katika kila ofisi ya serikali ya mtaa kuwe afisa mipango miji na kwamba mtu haruhusiwi kujenga mpk huyo afisa ajiridhishe kwamba mjenzi amejenga eneo sahihi na katika muundo unaotakiwa.

Na hii kwa kiasi kikubwa imetokana na watu kuuziana viwanja kiholela holela unakuta mtu ana kiwanja chake kakikata nusu kamuuzia mwengine hapo ndio chanzo cha ujenzi holela unakuta nyumba hii imegeukia huku uwani kuna nyumba nyingine imegeukia kule yn hovyo hovyo kabisa.

Serikali kupitia mipango miji na wizara ya ardhi kwa ujumla tunaomba msilifumbie macho jambo hili cz tunaona kazi kubwa mnayoifanya lkn itakuwa haina maana kama tuna nyumba nzuri lkn zimelundikana hovyo hovyo kama slums, tunaomba serikali iitazame ofisi hii ya mipango miji kwa jicho la mwewe cz imekuwa ni ofisi mzigo kwa miaka mingi ss.
 
Bora luse umeanzisha uzi huu... Maana miji mingi tz inakua kwa speed kipindi hichi so maafisa mipango wa wilaya na mikoa waanze kuliangalia hili mapema, Tusirudie makosa.

Wekeni mkazo kwenye miji inayokua hakikisheni ramani zake ni za mipango ya muda mrefu.

Shida ramani za mipango miji sio longterm planned..
 
Tanzania kuna miji mingi inayokua kwa kasi sasa hivi waanze kushughulika na hii miji waipange vizuri na wathibiti upimaji holela wa viwanja,

Kwa Dodoma nawapa pongeza,

Kila baada ya nyumba kadhaa Dodoma unakuta barabara,
Nadiriki kusema Dodoma ndio jiji lililopangwa vizuri ukanda wote huu wa Africa mashariki,

Dar es salaam mipango miji hamjachelewa sana mnaweza kufumua zile sehemu ambazo watu wamejijejengea walipwe fidia na kuwahamishia sehemu nyingine tena ikiwezekana mikoa ya jirani imegwe na kuongezwa ndani ya DSM na kuweka usafiri wa haraka na uhakika.
 
Mfano wakianza kufumua kwa awamu zile sehemu ambazo watu wamejijejengea ndani ya miaka kadhaa tu wanakuwa wamemaliza,

Maana sasa jiji la Dar es salaam linakuwa sana,

Watu wahamishwe nje ya mji walipwe fidia halafu hayo maeneo wapewe shirika la nyumba la taifa ili wajenge vitega uchumi na nyumba za bei nafuu,

NB: Wasipewe wawekezaji wa nje.
 
Sawa sawa na hii thread inatakiwa tuitunze mpaka kieleweke pia ingekuwa poa km tungelikuwa tunatupia na picha za ujenzi holela, unakuta nyumba nzuri ila hazina mpangilio mzuri inakera sana.
 
Mnh kwa muda huu, huu uzi unaweza kukosa wachangiaji...naona watu wako busy na uchaguzi

Jr[emoji769]
Ni kweli kabisa. Tuseme kwa mfano kwenye jimbo ninalogombea Ubunge mimi, ukiwatajia kitu kingine tofauti na jina langu, wanaweza hata kukupiga mawe. Yaani hapa nilipo mimi tayari Mbunge, uwaziri pekee tu ndiyo uliobaki haujulikani kwangu mpaka muda huu
 
Pendekezo langu ni kwamba serikali haipaswi kulifumbia macho jambo hili km tunataka kuona Tz mpya ya uchumi wa kati, inapaswa kuhakikisha mwananchi hana mamlaka ya kujenga jengo lolote pasipo kupata ruhusa kutoka mipango miji, yn kuwe na utaratibu fulani ambao ikitokea mtu kauvunja basi jengo lake livunjwe pasipo kuwa na huruma yyte.

Mfano katika kila ofisi ya serikali ya mtaa kuwe afisa mipango miji na kwamba mtu haruhusiwi kujenga mpk huyo afisa ajiridhishe kwamba mjenzi amejenga eneo sahihi na katika muundo unaotakiwa.

Na hii kwa kiasi kikubwa imetokana na watu kuuziana viwanja kiholela holela unakuta mtu ana kiwanja chake kakikata nusu kamuuzia mwengine hapo ndio chanzo cha ujenzi holela unakuta nyumba hii imegeukia huku uwani kuna nyumba nyingine imegeukia kule yn hovyo hovyo kabisa.

Serikali kupitia mipango miji na wizara ya ardhi kwa ujumla tunaomba msilifumbie macho jambo hili cz tunaona kazi kubwa mnayoifanya lkn itakuwa haina maana kama tuna nyumba nzuri lkn zimelundikana hovyo hovyo kama slums, tunaomba serikali iitazame ofisi hii ya mipango miji kwa jicho la mwewe cz imekuwa ni ofisi mzigo kwa miaka mingi ss.
mkuu hii ya kila ofisi ya serikali ya mitaa kuwa na afisa mipango miji imekaa sawa sana......naunga mkono nilikuwa na wazo kama hili umeniwahi
 
Back
Top Bottom