Mipango miji Tanzania

Kuna vurumai kila sekta, mipango miji ni mfano tu, angalia kwenye elimu, tiba, na huduma nyingine za kijamii ni tafrani, hakuna standards. Shule au hospitali inajengwa kariakoo uzio wake ni maduka au bars. Ni mfumo mzima wa maisha yetu una walakini
 
Kuna vurumai kila sekta, mipango miji ni mfano tu, angalia kwenye elimu, tiba, na huduma nyingine za kijamii ni tafrani, hakuna standards. Shule au hospitali inajengwa kariakoo uzio wake ni maduka au bars. Ni mfumo mzima wa maisha yetu una walakini
Ni kama tumevurugwa makusudi.
 
Nikweli mkuu nilienda Lindi Kijiji kimoja kinaitwa Liwale kiukweli ni kijijini kweli na nyumba haziko standard kivile lkn zimepangiliwa vzr yn mpk raha, unakuta mpk nyumba za udongo zipo ktk mpangilio mzuri barabara zimeachwa mita kadhaa kunapendeza kweli kweli yn.
 
Viko vingi sana ..sema ni zile sheria wakati huo, zilifanya watu wakimbie kuanzisha vijiji hovyo hovyo... Hawataki kuwajibika.

Its high time wenyeviti wa mitaa, halmashauri za vijiji zifunguliwe mashataka kwa uholela huu.. maana watu hawa wanapita kwenye ofisi za vijiji na mitaa.. halafu unawakuta wamejenga bondeni.. how!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Miongoni Mwa Wazee Wazembe Wanaopewa Sifa za Kijinga-jinga..!


Mipango Miji bongo unaweza toa Machozi.
si umeona kwenye taarifa yake hapo juu anakali Kuwa kuna uzembe halafu hatoi kauli yenye action yakuwawajibisha wanaofanya uzembe ,it means naye ni mzembe hivyo hawezi kuwajibisha wazembe wenzake.....


kiroho safi jamani
 
ni sawa kabisa,tuondoe hii dhana kabisa maana wasiojiweza wengi mind set yao kwa asilimia kubwa wanajua kuwa kulikopimwa ni kwa wenye nazo hivyo hawawezi kuefford manunuzi ya viwanja....

na fikra hizi zinatokana na utaratibu m'bovu uliopangwa...
 
Sio kazi ya serikali za mitaa kupima viwanja,mhusika ni wizara ya ujenzi huku halmashauri wana watu wao tu ambao wanasubili waelekezwe wapi wakapime.Sheria inazuia ujenzi holela lakini utekelezaji wake unakwama maana anayetakiwa kupima viwanja watu wajenge ni serikali,pili bei wanazouza serikali wakishapima sio rafiki kwa mtu wa kawaida lakini na utaratibu wa kupata viwanja una urasimu na mlolongo mkubwa na kupeana vimasharti vya kukiendeleza plus kodi ya kila mwaka.
Mikoani eneo la ndani ya km 8 kutoka katikati ya mji viwanja kwa watu binafsi ni kati ya 1-2mlns vyenye ukubwa wa 20x30 wakati hicho hicho kiwanja serikali inakiuza kwa zaidi ya 2.5lns sasa hapo kwa nini mtu asiende kwenye cheap.
Dawa hapa ni serikali kuainisha maeneo yote ya makazi na huduma zingine na kuyapima na kuuza bei rafiki na bila masharti ya ajabu ajabu,imefika mahala kupata plot iliyopimwa ni ufahari na anasa
 
Kitu usijokijua ni kwamba ,hiyo ya kujenga mpaka kibali inachukuliwa kama njia ya mapato kwenye halmashauri na maofisa wa ardhi bila kujalisha ni plot au squatter..Wao walipe pesa yao 50,000 wachukue watu wa ardhi wakuchoree ramani na uwapeleke site kuzuga ,hiyo kumtoa ofisini ni pesa inakuwa imetoka hiyo.
Point kuu ni wazuie ujenzi kwenye squatters na wapime viwanja na tuvipate kwa bei rafiki full stop tofauti na hapo watakua wanakula pesa na ujenzi holela unaendelea kama kawaida maana na mimi nimeshiriki hiki nachosema ndio inavyofanyika.Ukiona umepigwa pin ya x nyekundu ubomoe ujue hujalipa pesa tu,ukilipa mambo yanaendelea as usual
 
Usisingizie sera ya kibepari sijui uliberali hakuna kitu kama hicho,kwani kwa hao walioanzisha hizi sera tulizokopi kumejaa slums kama huku? Ni uzembe wa serikali moja kwa moja.Mkoa wa Rukwa kwa mfano wananchi wamejitahidi kujenga kwa space na mitaa ya wao wenyewe kujipangia kuanzia mjini hadi vijijini kote huko japo miaka ya hivi karibuni uhamiaji umekua mkubwa mambo ya uhovyo na uholela kwenye ujenzi umeanza kuja kwa kasi.
Halmashauri kazi yao wanapima viwanja buku wanapotea hata haviuziki kwa bei za kitapeli
 
Hata elimu na uzuri wake inaweza kutumika kama silaha ya kukukandamiza.

Sera inategemea ulipokeaje .. nimekupa mfano.. darasalam yote kuanzia city center mpaka Magomeni, Chang'ombe, kinondoni.. squatter zinahesabika na si kubwa..

Moshi mijini, Kahama mjini, tabora mjini nk.. kote miji inatazamika.. nini kimefanya hii miji imegeuka ghafla!? Maana haijengwi na serikali hii.. inajengwa na watu.. kitu gani kimewaingia mpaka wameanza kuvuruga hovyo!?

Umesema juu ya ongezeko la ghafla la watu ..unataka kusema kukiwa na watu wengi tu lazima kuvurugike!?

Nikusaidie ..wanasema Garbage in, Garbage out. Usipoboresha akili za wakazi wa mijini.. utakuwa na watu wa kijijini wanaoishi mjini na utofauti utauona tuu.. na ndio huu.. sera zinasehemu kubwa sana katika hili. Jisomee tu.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Chief usipaze sauti unapokuwa haujui... Uliza ufundishwe.

Kwanza wizara ya ujenzi inapima ardhi tangu lini!? Wizara ya ujenzi inajenga tena hukoooo kwenye miundombinu. Wizara ya ardhi ndiye msimamizi wa ardhi yote Nchini.. ikiwemo hata hiyo miundombinu inakojengwa na ujenzi.

Kwa mujibu wa Katiba ardhi yetu Tanzania tunaimiliki collectively ya umma. Mtu mmoja mmoja anapewa kitu tunakiita user rights.. haki ya kuoccupy na kutumia Ardhi hiyo. Na unalipia kupata hiyo nafasi na unalipa kwa wengine kukosa ila ukapewa wewe.

Msimamizi wa ardhi yote ni Commissioner wa Ardhi. Huyu anateuliwa na rais kuisimamia adhi kwa niaba yake. sasa huko ujenzi wana huyu kamishna!?

Kinachofanya kiwanja kilichopimwa kuwa ghali ni security that comes with it. Serikali ya Tanzania inakupa guarantee kuwa kipande hicho unachouziwa hakina tatizo na ukimilikishwa serikali itasimama nyuma yako kukulinda wewe na maendelezo yako. Hiyo ndio sababu unalipa zaidi.

Sasa kanunue kwa sh. Laki sita upambane na ndugu wa familia, ukoo,majirani.. haitoshi ukutane na serikali pia inataka kupitisha miundombinu.. maana yote hayo hayawezi kuwa shida ikiwa eneo litakuwa lilipangwa na kupimwa kwa mujibu wa serikali.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app

Ujue kabisa msimamizi wa miji ni local government tu.. serikali kuu inasimamia sera, sheria na kanuni pamoja na kuzishauri local authorities ktk kujenga miji bora.
 
Wanapita kimya kimya wanajifanya hawaoni,kawapelekee kule kule EAC forums
mkuu mbona hakuna tatizo ,uzi upo kwaajili ya kujenga kwa kuangalia mapungufu pia kutoa mawazo mbadala....hao wote ni wadau tulikubaliana hili ,hakuna tatizo
 
Bahati Mbaya sana Serikali Haijaona hili jambo la kutopanga Miji kama Janga kubwa linaloimaliza hii nchi..

Kutopanga miji kuna madhara makubwa sana.

Kwanza msongo wa mawazo , magomvi yasiyoisha kwa majirani mfano unakuta hapa ni Bar pembeni Shule kule mbele kidogo Jalala na hapo hapo Hospitali au kituo cha Afya.

Mkanganyiko kama huu lazima ugomvi uanze na mamlaka zetu za kuzuia hili zinajikuta hata wakienda hawana la Kufanya .


Katika Hali ya Kawaida Kutopanga miji ni chanzo kikuu cha magonjwa kwasababu maeneo mengi hasa mijini watu wamerundikana sana sana..hakuna hewa, hakuna mitaro ya maji ya mvua wala maji taka kila mtu anajitiririshia kama anavyotaka ni tatizo kubwa sana.


Magonjwa kama Kipindupindu hayaezi kuisha kama hatutapanga miji uchafu hauzolewi wala miji mingi inakua haina Majalala wala mifumo ya kuzoa taka hili linasababisha taka za aina zote ziwe ngumu au maji kumwaga hadharani Popote.

Kwenye kampeni Tunawasihi Wanasiasa zingatieni usafi wa Mazingira .Sijasikia kabisa Wanasiasa wakigusia
 
sure mkuu
 
kwa sehemu kama izo apo kwe picha si lazima wapime(wajenge square.
wavunje baadhi ya nyumba na kupitisha barabara ata kama ni ya kupindapinda naamini bado italeta aerial view nzuri tuu

nafkiri hii njia itaweza kupunguza gharama
 
Huu uzi usilale wakuu ndio ngao yetu hii tupambane mpk kieleweke ndugu zangu cz nchi kwa ss inakwenda kuwa super power in East and Central of Africa so ni lazima tuwastue hawa ili kuwe na uhalisia wa mambo wakuu.
 
kinachonipasua kichwa na kunisikitisha ni kwamba sheria za kimkakati zipo ,,,,ila hawa wenye dhamana na hili swala la mipango miji dhahiri inaonyesha kuwa hawapo serious kwenye usimamizi...

tupate darasa kidogo

 
Tanzania urban planners are the cause of this desease called slums at its best
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…