bhachu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 8,443
- 9,854
Do you know the meaning of slums?
Kama picha inavojieleza hapo Juu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Do you know the meaning of slums?
Great discussion, personally naona watu wa mipango miji hawaendi kwa speed inayotakikana. Lakini pia naona kwenye baadhi ya halmashauri kama tanga mjini, longido huwezi kujenga bila kupata kibali kutoka ardhi hii ingeigwa na halmashauri zote nchini basi naona hili tatizo tungelipunguza sanaHabari wanajamvi.....?
Nachukua fursa hii ili tuweze kujadili kwa pamoja hoja husika kuhusu wizara husika kwa upande wa mipango miji kwa nchi yetu ya Tanzania."
kwanza niipongeze wizara kwa kujitahidi kusimamia utendaji wao japo si kwa kiasi kikubwa..
Kutokana na uzalendo na kupenda mandeleo kupitia sekta tofauti tofauti,Leo ningependa tulijadili hili swala la mipango miji yetu,,kiuhalisia wizara husika kama inalega kwa hili swala haswa kwa upande wa kupima maeneo ili jamii ijayo iweze kuishi sehemu yenye mpangilio bora kwani hii itasababisha hata miondo mbinu iweze kufika kirahisi pamoja na huduma nyinginezo muhimu za kijamii..
Tunaona miji inakuwa kinacholeta changamoto bado muendelezo wa makazi holela hata sehemu za makazi mapya ama miji mipya baadhi ya sehemu bado ujenzi hilela unaendelea na kuleta shaka kuwa hii hali ya ujenzi holela itaendelea kuwepo miaka na miaka na hii yote sababu wizara husika haijatia nguvu za kutosha kwa kutolea macho hili swala kwa kila sehemu inayoanzishwa makazi mapya na yale ya awali kwa kuhakikisha wanawapa watu utaratibu maalum kwa kuhakikisha nyumba zinakaa kwenye mpangilio..
hususani ni sehemu ambayo muhanga kwenye suala la ujenzi holela...
Kwa kweli hili swala la kuruhusu kila mtu ajenge atakavyo linaleta changamoto kimakazi ,japo ni sawa kila ajenge nyumba aitakayo lakini wizara inabidi isimamie utendaji wao kwa umakini zaidi kwa kuwapa watu mwongozo maalum...
Nawasilisha hoja mezani ili tuweze kulijadili hili kwa pamoja na kutoa ushauri bora kupitia hoja husika..
1.Je wizara husika utendaji wake unaridhisha..?
2.Je kipi kifanyike ili majiji ya Tanzanja yaweze kuwa kwenye moangilio mzuri wa kimakazi....?
karibuni
#TUIAMSHE WIZARA YA UJENZI NA MIPANGO MIJIView attachment 1564930View attachment 1564931View attachment 1564928View attachment 1564929
upo sawa mkuu ila mamlaka ndiyo yenye dhamana kuu,,,kazi yao ndogo tu wangekuwa wanatoa mwongozo na kuweka sheria kali penye miti mingi hapakosi wajenzi,,,,Kwanza lazima tukubali kwamba Wananchi wetu nao ni tatizo...tuna jamii ya Watu wasiotumia akili kabisa kabla hata ya Mamlaka husika na Watendaji wake, of course hata hao Watendaji ni miongoni mwa Wananchi hao hao.
Unakuta eneo ni jipya kabisa na ujenzi unaendelea tena nyumba za gharama kubwa lakini ukiangalia zilivyokaa shaghala baghala mpaka unajiuliza akili za hao Wanaojega.
Hivi hakuna namna nyinyi Wenye viwanja hapo mkakaa chini na kuona jinsi ya kuzipanga nyumba zenu kabla hata ya kila mmoja kujenga kivyake bila utaratibu?.
Kama ukikuta Mwenzako ameshatangulia kujenga kwa nini wewe usije na plan ambayo itaacha eneo lenu likiwa na muonekano mzuri badala ya nawe kujenga tu lijumba lako likubwa tena linagharimu mamilioni ya pesa na hakuna hata barabara ya kulifikia.
Nadhani kabla ya kuzisubiri mamlaka Wananchi nao wajiongeze.
Tena ni jipu kweli kweli na ndiyo wizara inayoturudisha nyuma, yn kuna rushwa wizara ya ardhi pengine kupita wizara zote.Waziri mwenye dhamana Lukuvi amekiri kuna uzembe wa kuchelewesha vibali na mda mwingine wanahitaji mpaka hongo..
sasa kama wanajua hivyo ni kipi kinashindikana kuwawajibisha ....yaani kuna uzembe wa hali ya juu,hii idara ni jipu tena kubwa
Nimefuatilia uzi ...Huu ni uzi safi kabisa na kama moderators wanaona.. ninaomba kusisitiza uzi upigiwe chapuo unatakiwa uonekane sana a na michango mingi ipokelewe.Hebu angalia upuuzi km huu, hawa c ni km nzi au mende waliojazana sehemu moja hawa, nyumba nzuri kweli kweli na zimejengwa na wananchi wa kipato cha kawaida tu, tofauti na wenzetu nchi zinazotunguka mwananchi kujenga nyumba km hyo ni kitu cha ajabu sana lkn Tz ni kawaida sn mwananchi kujenga tena nyumba ya kisasa kabisa but mpangilio ndo km unavyoona hapa [emoji116][emoji116][emoji116]
View attachment 1565171View attachment 1565172
Mipango miji mnatuangusha sana.
Magu inabidi alilipue hili maana watendaji kazi imewashinda ,na wakitaka kufanya watafanya kimihemko kisa mjomba kawashika....Tena ni jipu kweli kweli na ndiyo wizara inayoturudisha nyuma, yn kuna rushwa wizara ya ardhi pengine kupita wizara zote.
mkuu kwanza karibu sana...Nimefuatilia uzi ...Huu ni uzi safi kabisa na kama moderators wanaona.. ninaomba kusisitiza uzi upigiwe chapuo unatakiwa uonekane sana a na michango mingi ipokelewe.
Kwa utangulizi ninaomba kudeclare internet.. Mimi ni Town/Urban Planner.. lakini nitakachotoa sio shutuma wa utetezi..bali ni mawazo binafsi kama mtaalamu huru.
Shida ya mipango miji nchini..imeanza kukua baada ya kulikimbia azimio la Arusha.. kuna nadharia kutaka uhuru wa kibinafsi na kukwepa uwajibikaji kulikua Azimio la Arusha kumepelekea hapa tulipo kama nitakavyoeleza huko mbeleni.
Wana jamvi, kwanza kabisa, wataalamu wa mipango miji ndio walinzi wa ustaarabu wetu. Wanasaidia kujenga mifumo ya kujiendesha, mazingira ya kuendeshea mifumo hii kwa kuzingatia mahitaji yetu na rasilimali tulizonazo kuongeza tija.
Miji yetu sio mibaya, na inaweza kubadilika na kuwa miji bora kabisa tukiweza kurejesha uwajibikaji. Au kujenga mifumo ya kuwawajibisha wanaoenda kinyume na makubaliano..
Changamoto iliyopo wanasiasa wameingilia kati na wananchi wasiojua umuhimu wa maswala haya wameanguka katika tabia ya kulialia kwa wanasiasa juu ya kukosa makazi na kutaka kujenga kila mahali na bila kufuata utaratibu..
Sera ya Makazi inataka tuboreshe makazi na kuhakikisha kila mtu ana nyumba bora. Lakini inasisitiza maeneo na mazingira wanamoishi watu yawe yenye utaratibu. Na kwa ujumla wake makazi ni pamoja na biashara viwanda, viwanja vya michezo na huduma zote zinazofanya maisha yetu ya kila siku kuboreka.
Hii chapa tunayoiona, ninaamini its by design.. sio bahati mbaya.. utashangaa NGO nyingi zinatetea umiliki wa ardhi ila hazifundishi uwajibikaji juu ya miliki hizi.
Kumiliki kitu sio guarantee lazima uruhusiwe kukitumia. Ni kwenye ardhi tu dio naona hii nadharia ikitetewa na wasomi wanasheria.. watu hawafuati utaratibu wa kisheria kabisa wa kutokuendeleza mpaka wapatiwe kibali..lakini bado wanatetewa na wanasheria nguli waachwe wanajitafutia mahali pa kuishi..ni Aibu.
Kurudi kwenye mada naomba niseme maswala machache kama ifuatavyo.
1) Lazima kuwe na mfumo utakaosaidia uongozi kwa ngazi ya mtaa na kata kufuatilia maendelezo yote katika ardhi. Mfumo wa taarifa na vibali unaoweza kuwa inspected na mtu yeyote. (Kuwe na Certificate ya uendelezaji inaitolewa kwa mtu ikiwa na development conditions)
2) kuwepo na mfumo wa kuziwasilisha biashara zinazofanyika katika maeneo yasiyo rasmi. Katika hili muuzaji na mnunuzi wanakuwa liable maana mnunuzi ndiye anachangia biashara hizi kukua na kukaa maeneo yasiyofaa
3) mipango inapoandaliwa iletwe mitaani katika lugha ambayo wana mitaa wanaweza kuielewa. Ili waweze kuisimamia kikamilifu
4) mitaa iwe na umiliki (Home owners association) ambapo waishio mtaani wote watakuwa sehemu ya association hiyo kisheria.. na watakuwa na uongozi ambao utasimamia na kuratibu shughuli uendelezaji, uboreshaji na utunzaji wa image ya Mtaa. Na utaweza kusimamia sheria ndogo ndogo kufanya lobbying kupata uwekezaji na usimamizi wa mabadiliko ya matumizi usio wa kiholela
5) kila mradi mpya wa miji, uandaliwe ukiwa na asilimia 15 ya ardhi yake itengwe kwa ajili ya watu wa kipato cha chini.. maeneo hayo yapangwe kwa viwanja vidogo vidogo vya sqm 240-300 na barabara nyembamba za mita 6-8 na viuzwe kwa nusu ya bei ya kawaida.
Kodi katika maeneo haya (ikiwa yatahodhiwa na watu wenye kipato kikubwa) itapangwa na serikali na wateja wataletwa na serikali kupitia wakala maalumu. Azma ni wale waliolengwa ndio waishi katika maeneo haya.. kila mji uliopangwa unahitaji watu wa kipato cha chini kwa shughuli mbalimbali kama kukata majani, usafi nk.. unapokosa kuweka hilo utapata Hananasif na Msasani bonde la mpunga.
6) kuweka msisitizo mkubwa katika maendeleo ya vijiji. Ikiwemo kuwa na standardized layout plan for village HQ. Na Kijiji kinapopewa hadhi wataalamu wafanye utafiti na washauri makao mapya ya kijiji yajengwe Katika eneo salama.. sio kwenye mashamba ya mpunga kisa tu mliwakuta watu wamejazana hapo.
7) serikali itoe Ramani za majengo kwa watu wasio na uwezo..pamoja na manual/guide for construction kwa aina zote ya nyumba kwa kuzingatia space standards. Kama mtu anaweza kuandika nyumba fupi kama ya kuingia kulala mbuzi kwann alitumia muda kukandika nyumba bora kwa ajili yake na wanae.!? Kukiwa na manual Basi veo kwa kuanzia anaweza kabisa kusimamia na kuhakikisha nyumba zote nchini zinajengwa kwa ubora.
Yako mengi na tutaendelea kuyazungumzia kadri yanavyojidhihirisha. Ila nakushukuru sana kwa michango na mleta uzi kwa jambo hili jema.
Mwisho naomba niseme tukiendelea kubembelezana na kuoneana haya.. kudhani kura za wanyonge na kuwaacha walipe 20kili wafanye vyovyote wanavyotaka ni uongozi.. kitakachotupata huko mbeleni ni vilio maana tutadumaa na hawa wa elfu ishirini watakuwa wazee wasio na mafanikio na serikali itakuwa haina fedha za kuwahudumia kwa maana a waliua biashara za msingi zenye kulipa kodi .. zilizopoteza ajira kwa watu na kuongeza wimbi la umasikini.
Mipango miji makosa yake sio ya kesho ..yatachukua miaka 40 lakini yatafikia kama jua la asubuhi. na mengi tunayoyaonya leo kisiasa yatatutesa sana kesho. Mungu Ibariki Tanzania.
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
ujue hii dhana ya kufanya sehemu iliyopangika waishi wenye kipato na sehemu isiyopsngika waishi wasio na kipato kikubwa inatuletea shida na matabaka....Watanzania lazima wajue.. Mipango imeathiriwa pia na swala elimu.
Watanzania hawakufunzwa kukaa maeneo yaliyopangwa na kuwa wa utaratibu.
Mipango miji ni reflection ya ustaarabu wa jamii. Na watu wanastaarabika kupitia elimu.
Hushangai hakuna Mtu kutoka nchi zilizoendelea hasa za ulaya bajeti hiyo hivyo au kuishi kwenye makazi holela!?
Maana kilichopangwa ni akili yake. Na hivyo anafanya chaguzi sahihi.
Sisi mtu anaenda sehemu ya waenda kwa miguu mwenge, anapanga biashara..halafu anayekuja kununua ni jirani yake kule ununio..unashangaa kwann wote wawili wasiuziane kule ununio!? "Elimu" ni changamoto
Kudeka na Umimi .. ubinafsi mkubwa hasa kwa miaka ya karibuni umekuwa ni changamoto.. land grabbing imeongezeka sana..
Dawa hii tulete kodi ya matumizi ya Ardhi.. katika maeneo yenye uhitaji wa housing unitskuwe na kodi ndogo sana kwa wanaojenga nyumba za kupangisha ili watu waongeze units na kupangisha kwa bei nafuu.. na kwa maeneo yenye msongamano mkubwa kuwe na kodi kubwa kudiscourage ongezeko la watu katika maeneo hayo.
Lakini pia kuwe na kodi kubwa sana kwa viwanja vilivyo wazi mijini... Kupromote compact cities na kudiscourage Speculation.
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Miongoni Mwa Wazee Wazembe Wanaopewa Sifa za Kijinga-jinga..!hawezi kosa mkuu ndiyo waziri husika....
Shukran sana mkuu kwa uchambuzi yakinifu, tunaomba hili jambo lisiishie hapa bali lifike mbali zaidi ili wasikie hawa watu.Nimefuatilia uzi ...Huu ni uzi safi kabisa na kama moderators wanaona.. ninaomba kusisitiza uzi upigiwe chapuo unatakiwa uonekane sana a na michango mingi ipokelewe.
Kwa utangulizi ninaomba kudeclare internet.. Mimi ni Town/Urban Planner.. na nitakachotoa sio shutuma wala utetezi..bali ni mawazo binafsi kama mtaalamu huru.
Shida ya mipango miji nchini..imeanza kukua baada ya kulikimbia azimio la Arusha.. kuna nadharia kutaka uhuru wa kibinafsi na kukwepa uwajibikaji kulikua Azimio la Arusha kumepelekea hapa tulipo kama nitakavyoeleza huko mbeleni.
Wana jamvi, kwanza kabisa, wataalamu wa mipango miji ndio walinzi wa ustaarabu wetu. Wanasaidia kujenga mifumo ya kujiendesha, mazingira ya kuendeshea mifumo hii kwa kuzingatia mahitaji yetu na rasilimali tulizonazo ili kuongeza tija.
Miji yetu kwa sasa sio mibaya (sana), na inaweza kubadilika na kuwa miji bora kabisa tukiweza kurejesha uwajibikaji wa wakazi. Au kujenga mifumo ya kuwawajibisha wanaoenda kinyume na makubaliano..
Changamoto iliyopo..wanasiasa wameingilia kati na wananchi wasiojua umuhimu wa maswala haya wameanguka katika mtego wa kulialia kwa wanasiasa juu ya kukosa makazi na kutaka kujenga kila mahali na bila kufuata utaratibu.. na wanasiasa wanaruhusu maana kuna kura hapo.
Sera ya Makazi inataka tuboreshe makazi na kuhakikisha kila mtu ana nyumba bora. Lakini inasisitiza maeneo na mazingira wanamoishi watu yawe yenye utaratibu. Na kwa ujumla wake makazi ni pamoja na biashara viwanda, viwanja vya michezo na huduma zote zinazofanya maisha yetu ya kila siku kuboreka.
Hii chaos tunayoiona, ninaamini its by design.. sio bahati mbaya.. utashangaa NGO nyingi zinatetea umiliki wa ardhi ila hazifundishi uwajibikaji juu ya miliki hizi. Mipango miji effective ndio msingi wa mafanikio ya kiuchumi... Na huo ndio utofauti wa China na India... Taiwani na Singapore Nigeria na South Africa. Lazima tujitathmini.
Ikumbukwe.
Kumiliki kitu sio guarantee lazima uruhusiwe kukitumia. Ukinunua gari serikali itakutaka ufanye mambo chungu mbovu kabla hujaiendesha.. ukinunua bunduki huwezi kupiga hovyo hivyo.. lazima kuna utaratibu wa kufuatwa..
Kwenye ardhi tu ndio naona hii nadharia ikitetewa na wasomi wakubwa tens wanasheria.. watu hawafuati utaratibu wa kisheria kabisa wa kutokuendeleza mpaka wapatiwe kibali..lakini bado wanatetewa na wanasheria nguli waachwe wanajitafutia mahali pa kuishi..ni Aibu.
Kurudi kwenye mada naomba niseme maswala machache kama ifuatavyo.
1) Lazima kuwe na mfumo utakaosaidia uongozi kwa ngazi ya mtaa na kata kufuatilia maendelezo yote katika ardhi. Mfumo wa taarifa na vibali unaoweza kuwa inspected na mtu yeyote. (Iwepo Certificate ya uendelezaji inaitolewa kwa mtu ikiwa na development conditions) jirani akianza tu mnamuhoji ulipata certificate ya uendelezaji!? Akiwa hana ni kosa.. akijenga na hana.. serikali inavunja.
2) kuwepo na mfumo wa kuzisitisha biashara zinazofanyika katika maeneo yasiyo rasmi. Katika hili muuzaji na mnunuzi wanakuwa liable maana mnunuzi ndiye anachangia biashara hizi kukua na kukaa maeneo yasiyofaa.. mkikamatwa wote korokoroni mnashirikiana kuhujumu biashara halali ziliko maeneo halali.
3) mipango inapoandaliwa iletwe mitaani katika lugha ambayo wana mitaa wanaweza kuielewa. Ili waweze kuisimamia kikamilifu. Picha na mipango ya utekelezaji yenye milestones.
4) Mitaa iwe na umiliki (Home owners association) ambapo waishio mtaani humo wote watakuwa sehemu ya association hiyo kisheria.. na watakuwa na uongozi ambao utasimamia na kuratibu shughuli uendelezaji, uboreshaji na utunzaji wa image ya Mtaa. Na utaweza kusimamia sheria ndogo ndogo kufanya lobbying kupata uwekezaji na usimamizi wa mabadiliko ya matumizi usio wa kiholela
5) Kila mradi mpya wa mipango miji, uandaliwe ukiwa na asilimia 15 ya ardhi imetengwa kwa ajili ya watu wa kipato cha chini.. maeneo hayo yapangwe kwa viwanja vidogo vidogo vya sqm 240-300 na barabara nyembamba za mita 6-8 na viuzwe kwa nusu ya bei ya kawaida.
Katika maeneo haya (ikiwa yatahodhiwa na watu wenye kipato kikubwa) kodi itapangwa na serikali na wateja wake wataletwa na serikali kupitia wakala maalumu.
Azma ni wale waliolengwa tu: ndio waishi katika maeneo haya aidha kwa kupanga wa kujenga.. Kila mji uliopangwa unahitaji watu wa kipato cha chini kwa shughuli mbalimbali kama kukata majani, usafi nk.. unapokosa kuweka hilo utapata Hananasif na Msasani bonde la mpunga.
6) Kuweka msisitizo mkubwa katika maendeleo ya vijiji. Ikiwemo kuwa na standardized layout plan for village HQ. Na kila Kijiji kinapopewa hadhi wataalamu wafanye utafiti na washauri makao mapya ya kijiji yajengwe Katika eneo salama huku kikiwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.. na sio kwenye mashamba ya mpunga kisa tu mliwakuta watu wamejazana hapo.
7) Serikali itoe Ramani za majengo kwa watu wasio na uwezo..pamoja na manual/guide for construction kwa aina zote ya nyumba kwa kuzingatia space standards. Kama mtu anaweza kukandika nyumba fupi (kama ya kuingia kulala mbuzi) kwann asitumie muda kukandika nyumba bora kwa ajili yake na wanae.!?
Kukiwa na manual Basi VEO kwa kuanzia anaweza kabisa kusimamia na kuhakikisha nyumba zote nchini zinajengwa kwa ubora.
Yako mengi na tutaendelea kuyazungumzia kadri yanavyojidhihirisha. Ila nakushukuru sana kwa michango na mleta uzi kwa jambo hili jema.
Mwisho naomba niseme tukiendelea kubembelezana na kuoneana haya.. kudhani kura za wanyonge na kuwaacha walipe 20k wafanye biashara vyovyote wanavyotaka ni "uongozi"?.. kitakachotupata huko mbeleni ni vilio maana tutadumaa na hawa wa elfu ishirini watakuwa wazee wasio na mafanikio na serikali itakuwa haina fedha za kuwahudumia kwa maana a waliua biashara za msingi zenye kulipa kodi .. zilizopoteza ajira kwa watu na kuongeza wimbi la umasikini.
Mipango miji makosa yake sio ya kesho ..yatachukua miaka 40 lakini yatafikia kama jua la asubuhi. na mengi tunayoyaona na kuyafanya leo kisiasa yatatutesa sana kesho. Mungu Ibariki Tanzania.
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Masikini hana rafiki.. ndugu yake ni serikali.. sasa kama tunataka kuendelea kuwa inclusive Basi lazima kuwe na haki na usawa.ujue hii dhana ya kufanya sehemu iliyopangika waishi wenye kipato na sehemu isiyopsngika waishi wasio na kipato kikubwa inatuletea shida na matabaka....
inabidi kuclear haya makosa watu wabaki kushindana kwa majumba pekee....
Sera ya Ujamaa ilianzisha Vijiji vya ujamaa,. Ni chini ya sera za ujamaa miji kama Arusha, Moshi, Songea, Mtwara, lindi, Mbeya, Iringa, Bukoba.. nk ilipangwa .. na unaweza kuona utofauti wake na miji ya kibepari kama pembezoni mwake miji hii yote, Miji mipya kama, Mkata, Chalinze, Mikese, Mikumi ..imekuja na uliberali ambao kwa uwazi unaona lack of generalized focus na mji unakuwa simply a collection of household ...zenye fikra maono na malengo tofauti.. its just chaotic..Kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa. Nadhani sera za ujamaa zilichochea ukuaji wa mipango miji ya jadi (kienyeji au kiswahili). Ile dhana ya watu kuishi kijadi maisha ya kifukara ya kuombana chumvi kaya hadi kaya. Umasikini na unyonge ulikua ni alama ya uzalendo wengine wakiitwa mabepari na mabeberu. Hayo ndiyo matunda yake hapa kwetu Tz, huko kwingine sijui. Kama unabisha andamana.