KERO Mipeko - Mkuranga umeme ni mdogo, mwaka wa pili sasa TANESCO wameahidi kuweka Transformer kubwa

KERO Mipeko - Mkuranga umeme ni mdogo, mwaka wa pili sasa TANESCO wameahidi kuweka Transformer kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Mkuranga Mkoani Pwani maeneo ya Mipeko (MSIKITI wa KIPATI) tuna changamoto ya umeme, ni mdogo sana (low voltage) ni shida, ikifika Saa moja Jioni unakatika na kurejea Saa 6 Usiku.

Giza linasababisha kutokuwepo kwa usalama katika baadhi ya maeneo, watu wanafanyiwa uhalifu.

Umeme unaporejea unakuwa hauna nguvu, vitu vyetu vinaungua sana mchana napo hauna nguvu pia, mashine hazifanyikazi, matumizi yameongezeka, tunahitaji Transformer kubwa.

Tushatoa sana taarifa TANESCO tumeandikiwa kuwekewa transformer na Sasa ni karibu mwaka wa pili (tangu Aprili 2025), hii kero inatutesa sana.
 
Habari ndugu mteja.

Asante kwa kuwasiliana nasi, na pole kwa changamoto mnayopitia.

Tumepokea taarifa hiyo kwaajili ya ufatiliaji lakini pia tafadhali tupatie namba yako ya simu pamoja na taarifa kamili za eneo unalopatikana, ikiwemo Kata, Mtaa/Kijiji ili tuweze kukupatia msaada zaidi.^RS
 
Habari, ndugu mteja wetu,

Tunaomba radhi kwa changamoto za upatikanaji na ubora wa huduma ya umeme katika eneo la Mipeko na maeneo mengine yaliyoathirika, Wilayani Pwani. Tunaomba tukureje na majibu baada ya ufuatiliaji.

Tafadhali fahamu kuwa TANESCO tayari imebaini na kufanya tathmini katika maeneo yenye changamoto na inaendelea kutekeleza miradi ya kuboresha nguvu ya umeme (Voltage Improvement) ili kuimarisha ubora na upatikanaji wa huduma ya umeme.

Maeneo yaliyopo katika mpango huu wa maboresho ni pamoja na Mipeko, Luzando Mbuyuni, Tambani Juland, Vikindu kwa Nditi (nyuma ya Chuo cha Ualimu), Ngunguti, Kisemvule kwa Mzee Simba, Kisemvule Black Stone pamoja na Mwemanani. Kwa upande wa Mwemanani, maboresho yaliyopangwa tayari yamekamilika.

Kwa Mipeko, utekelezaji wa maboresho unatarajiwa kuanza wiki ijayo. Kwa ujumla, miradi hii inayolenga kutatua changamoto za umeme mdogo na kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo yaliyotajwa inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.

Tunaomba uvumilivu na ushirikiano wenu wakati kazi hizi zikiendelea. TANESCO itaendelea kufuatilia utekelezaji kwa karibu na kutoa taarifa pale inapohitajika.

Asante kwa uvumilivu na ushirikiano wenu.

Asante. ^MY
 
Back
Top Bottom