Miradi inakamilika kwa wakati, mnyonge myongeni haki yake mpeni

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Jana Tanzania tuliandika Historia kwa ufunguzi wa bwawa la Nyerere (JNHPP) kuanza hatua ya kwanza ya ujazaji maji hii ni hatua kubwa kwa taifa letu na kitu kingine nilichogundua ni kwamba Rais Samia Suluhu aliahidi atamaliza miradi yote iliyoachwa na mtangulizi wake amemaliza miradi mingi ikiwemo Stendi ya Magufuri (Nyamahongoro- mwanza) miradi mbalimbali ya miundombinu, maji , afya pia miradi ya elimu

Lakini kubwa zaidi ni suala la huu mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) Mhe. Dkt Samia ameingia Madarakani Mradi wa bwala Nyerere ulikuwa 37%, ndani ya mwaka 1.9, mradi umefikia 78.68%. Mkandarasi amelipwa shilingi trilioni 4.5 kati ya 6.5 sawa na asilimia 70, na hakuna deni analodai Kwaiyo hapa tukifanya calculation tunaona Rais Samia Suluhu ndani ya siku 644 toka aingie madarakani amefanya kazi kwa asilimia 41 kweli Rais Samia Suluhu anaendelea kufanya maajabu katika utendaji wake wa kazi

Lakini vilevile Rais Samia Suluhu ameona faida nyingi zitokanazo na bwawa hili na ndio maana amelipa kipaumbele baadhi ya faida ni katika kilimo cha umwagiliaji na uvuvi Kusaidia vijiji vya jirani katika huduma za afya na elimu Kurahisisha usafiri kati ya mikoa ya kusini na kaskazini mwa Tanzania.
 
Lazima ikamilike, kisiasa ni ✔
Pongezi kwa JPM ( rest easy) na SSH.
 
Pongezi nyingi zaidi ziende kwa wananchi kupitia kodi wanazozilipa na pia kubeba mzigo mkubwa wa deni la taifa, ambazo sehemu ya fedha zake zimetumika kujenga bwawa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana Tanzania tuliandika Historia kwa ufunguzi wa bwawa la Nyerere (JNHPP) kuanza hatua ya kwanza ya ujazaji maji hii ni hatua kubwa kwa taifa letu na kitu kingine nilichogundua ni kwamba Rais Samia Suluhu aliahidi atamaliza miradi yote iliyoachwa na mtangulizi wake amemaliza miradi mingi ikiwemo Stendi ya Magufuri (Nyamahongoro- mwanza) miradi mbalimbali ya miundombinu, maji , afya pia miradi ya elimu

Lakini kubwa zaidi ni suala la huu mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) Mhe. Dkt Samia ameingia Madarakani Mradi wa bwala Nyerere ulikuwa 37%, ndani ya mwaka 1.9, mradi umefikia 78.68%. Mkandarasi amelipwa shilingi trilioni 4.5 kati ya 6.5 sawa na asilimia 70, na hakuna deni analodai Kwaiyo hapa tukifanya calculation tunaona Rais Samia Suluhu ndani ya siku 644 toka aingie madarakani amefanya kazi kwa asilimia 41 kweli Rais Samia Suluhu anaendelea kufanya maajabu katika utendaji wake wa kazi

Lakini vilevile Rais Samia Suluhu ameona faida nyingi zitokanazo na bwawa hili na ndio maana amelipa kipaumbele baadhi ya faida ni katika kilimo cha umwagiliaji na uvuvi Kusaidia vijiji vya jirani katika huduma za afya na elimu Kurahisisha usafiri kati ya mikoa ya kusini na kaskazini mwa Tanzania.
Inakmilika kwa gharam kubwa sana mfano daraja la wami limeigharimu 20b zaidi ila chawa kama wew huwezi kuhoji zaidi ya kujua limekamilika
 
Back
Top Bottom