Miradi Mikubwa ya Kimkakati ya JMT huko Zanzibar ni Ipi?

Miradi Mikubwa ya Kimkakati ya JMT huko Zanzibar ni Ipi?

Kwani mwanakijiji yupo ? Ni yule yule au Yule aliachana siasa yuko busy mambo yake ? Mmmmm kama nonyule bora angeacha tu sasa ni poyoyo hana mvuto wala mashiko
 
Kwa kweli kama kuna kitu watu watakumbuka ni jinsi gani serikali ya Rais Magufuli imekuja na miradi kadha wa kadha ya kimkakati. Mingi ni ile ya maendeleo, lakini pia ipo ile ya ufufuaji vile vilivyokufa na kuchakaa... tumeona mara kwa mara viongozi wa serikali ya JMT wakinadi mafanikio mbalimbali ya 'tuliahidi, tumetekeleza, na tunasonga mbele". Je ni miradi gani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo imetekelezwa katika miaka mitano iliyopita na ni ipi inaendelea kutekelezwa sasa. Na ni nani mwenye jukumu ya kulitaarifu Taifa juu ya utekelezaji wa miradi hiyo?
Mbona viwanda vingi tu vilivyokufaga vishafufuliwa kama irani na ahadi ya chama ilivyonadiwa chama kipewe madaraka kitatekeleza na hawatawaangusha watanzania..

1.General Tyre Arusha kwa sasa kina zalisha Matairi kwa wingi zaidi na yanauzwa na kusambazwa dunia Nzima kadi inayopatikana ni kubwa mno inazidi hadi utajiri wa Elon Mask

2. Kiwanda Cha katani kishafufuliwa baada ya yule jamaa kunyang'anywa baadhi ya Mashamba.. Sasa hivi Tanzania inaongoza kwa zao la Katani kama ilivyokuwa miaka ile ya Awamu ya Kwanza.

3. Canvas imerudi tena juu Morogoro inawaka waka ajira nyingi mno baada ya arab kunyang'anywa eneo la kiwanda aliloligeuza eneo la kulazia mbuzi..

4. Viwanda vya cement nadhani kama unavyoona vimeongezeka na bei ya bidhaa imepanda ni jambo la kushukuru sana wananchi ndio tulivyokuwa tunahitaji maana tulichoka na zile bei ndogo tulizokuwa tunauziwa yaani bei za kizamani ni kujirudisha nyuma kimaendeleo naiomba serikali iongeze kodi ili bei izidi kupaa... kodi ndio maendeleo.

5. zzk mbeya ashukuruwe mbunge mpya kule mby maana kumbe ndio alikuwa akihamasisha gov ifanye maendeleo makubwa tunayoyaona na kumbe yule mbunge aliyekuwepo wakati ule alikuwa amesinzia tu... so ufufuliwaji wa kiwanda cha zzk cha zana za kilimo ni jambo la kumshukuru mbunge mpya.. sasa hivi zana zinauzwa dunia nzima kutoka kiwanda hicho kilichofufuliwa mbeya zzk.

6. Shirika la ndege limefufuliwa upya ndege zimekuwa nyingi na nauli imepaa juu ni jambo la kushukuru yale mambo ya fastjet kizamani sana nauli elfu 69 hadi laki na nusu dar mwanza ilikuwa kuishi kimasikini sana wacha tuifaidishe nchi kwa nauli hizi za juu ili ipate faida hata kama watasafiri wachache faida ipatikane ndege ziwe nyingi tuwe dona country.

7. ufisadi umesimama kabisa asilimia kubwa... tumeona yale majengo makubwa yaliyokuwa yaje kuipendezesha nchi yamesimama kuendelezwa na sasa yanaonekana kama magofu na matembe hongera sana mkuu ikiwezekana yabomolewe tu maana ni miaka mingi ishapita yamegeuka chukizo la mji..

8. Hostel za vyuo ndio tiyari na nyufa zishazibwa. hivi ndio hamna tena zingine kwa vyuo vingine?

itaendelea....
 
..kulikuwa na utamaduni kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani lazima atoke Zanzibar.

..hivi ktk baraza jipya kuna mawaziri na manaibu waziri wangapi kutoka Zanzibar?
Ndio kwanza mpaka tumewapelekea Katibu mkuu kiongozi toka bars(Mpemba aliyehamia Bara akiwa na miaka miwili)

Wizara ya Mambo ya Ndani toka Ali Ameir Mohammed (Alikua mwenezi pia) ikaruka akaja kupata Shamsi Vuai baada ya hapo ni manaibu tu kina Masauni na huyu wa Sasa Hamza Chili sijui kwanini hawafuati "kautaratibu" hako
 
Uko sahihi mzee mwanakijiji, ila hii sio dalili njema kwako kwa kuwa zamani mada zako zilipata michango stahiki kutokana na misimamo yako ya wakati huo, ila kwasasa wengi wanakuona mwepesi, hivyo mada zako zimegeuka kama klabu cha pombe. Huenda hili sio kosa lako bali lao, lakini lazima ujiulize mada zimefikake kujadiliwa kwa Uduni huu.
Hahahaaa mkuu tindo na wala sio kwamba hajui sababu. Anaelewa sana ndomaana siku hizi anakuja na vimada vya para 2 halafu anapotea.

Hawezi kuandika uchambuzi wa Mwanakijiji yule na vi inzi vyake watu tukachangia. Kwakua ameshachagua upande na upande aliopo unaumiza watu wengi kwa sasa
 
Kwa kweli kama kuna kitu watu watakumbuka ni jinsi gani serikali ya Rais Magufuli imekuja na miradi kadha wa kadha ya kimkakati. Mingi ni ile ya maendeleo, lakini pia ipo ile ya ufufuaji vile vilivyokufa na kuchakaa... tumeona mara kwa mara viongozi wa serikali ya JMT wakinadi mafanikio mbalimbali ya 'tuliahidi, tumetekeleza, na tunasonga mbele". Je ni miradi gani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo imetekelezwa katika miaka mitano iliyopita na ni ipi inaendelea kutekelezwa sasa. Na ni nani mwenye jukumu ya kulitaarifu Taifa juu ya utekelezaji wa miradi hiyo?
Kuuza nyumba za umma kwa hawala zao?
Kununua mindege na kuipaki pale kipawa?
Kuiba kura na kukamatwa wapinzani?
Miradi gani???
Wewe ulikuwa na chuki na kikwete huna lolote
 
Uko sahihi mzee mwanakijiji, ila hii sio dalili njema kwako kwa kuwa zamani mada zako zilipata michango stahiki kutokana na misimamo yako ya wakati huo, ila kwasasa wengi wanakuona mwepesi, hivyo mada zako zimegeuka kama klabu cha pombe. Huenda hili sio kosa lako bali lao, lakini lazima ujiulize mada zako zimefikaje kujadiliwa kwa uduni huu.
Ni dalili mbovu kuwa na mtizamo kuwa lazima mtu aikosoe serikali iliyopo madarakani ndio umuone ana msimamo thabiti.

Kama hakuna vya kukosoa kwa nini ulazimishe mtu kukosoa?
 
Yaaaaani we mzee mwenzangu toka utetee Lissu kupigwa risasi na kusapoti ma dictator umepoteza sana social legitimacy
 
Ndio kwanza mpaka tumewapelekea Katibu mkuu kiongozi toka bars(Mpemba aliyehamia Bara akiwa na miaka miwili)

Wizara ya Mambo ya Ndani toka Ali Ameir Mohammed (Alikua mwenezi pia) ikaruka akaja kupata Shamsi Vuai baada ya hapo ni manaibu tu kina Masauni na huyu wa Sasa Hamza Chili sijui kwanini hawafuati "kautaratibu" hako

..bila kusahau Prof.Mbarawa alipoteuliwa ktk wizara ya maji, wakati wizara hiyo siyo ya muungano.

..nadhani wanaogopa kuwapa Waznz wizara zinazogusa maslahi yao, kwani huwezi jua wanaweza kuanza kutetea haki zao ktk muungano.

..Wizara ya Fedha, Mambo ya Ndani, Katiba na Sheria, Mambo ya Nje, ni baadhi ya wizara ambazo wangeweza kuteuliwa mawaziri toka Znz.

..Hata ktk Bunge naamini Naibu Spika alipaswa kuchaguliwa toka Znz.
 
Mkuu, huo utaratibu ulikuwa lini, maana tumeona akina Kitwnga, Masha, Chiligati, Mrema, Kimario na wengine wakiwa mawaziri katika hiyo Wizara....!!

..baadhi ya wanasiasa wa Znz waliopata kuwa Mawaziri wa Mambo ya Ndani:
1. Hassan Nassor Moyo 2. Ali Hassan Mwinyi 3. Dr.Salmin Amour 4. Ali Ameir Mohamed 5. Omar Ramadhan Mapuri 6. Shamsi Vuai Nahodha
 
kuna wengine mnaweza kupata zero kwenye mitihani kirahisi kweli kweli...
mimi nina ushahidi wa kijana mtukutu aliekuwa haendi shule lakini kafaulu form four. suala la kupata zero sasa hivi halipo...ufaulu umeongezeka.
 
Mzee Mwanakijiji. Ni vema kujua kwanza hiyo miradi mikubwa ya kielelezo inayofanyika huku bara inaangukia kwenye masuala yepi baina ya yale ya muungano au yasiyo ya muungano.

Zaidi ya hapo tulimsikia rais juzi hapo akiwaomba Wachina watusaidie kujenga highway ya km zaidi ya mia kule zenji.
 
Back
Top Bottom