Miradi ya Kimkakati wa Maendeleo na Ubonereshaji Fursa za Ujasiriamali Zimekwama Wapi?

Miradi ya Kimkakati wa Maendeleo na Ubonereshaji Fursa za Ujasiriamali Zimekwama Wapi?

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2020
Posts
3,443
Reaction score
4,006
Wana Jukwaa Bingwa,

Miradi ifuatayo imetupwa kapuni au giza limetanda wananchi hawaoni?

1. Barabara ya mzunguko (Ring road) Km 100-Dodoma
2. Uwanja wa Michezo wa Kimataifa (Dodoma International Stadium)-Dodoma
3. Ujenzi Ikulu Chamwino (State House)-Dodoma
4. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato (Msalato International Airport )-Dodoma
5. Mji wa Mfano wa Serikali Mtumba-Dodoma
6. Ujenzi wa Balozi wa nchi mbalimbali kwenye viwanja walivyopewa awamu ya tano
7. Ukamilishaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya treni mwendo kasi (SGR) Dar-Morogoro itaisha lini na kuanza kutumika lini? Hali kadhalika Morogoro-Makutupora
8. Upanuzi wa barabara kutoka Morogoro-Dodoma
9. Maendeleo ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere (Julius Nyerere Hydro Power Generation Dam)-Rufiji Pwani
10. Upanuzi wa barabara njia nane Dar-Kibaha
11. Matumizi bora ya stendi kuu ya mabasi ya Magufuli (Magufuli Bus Terminal)-Mbezi Louis Dar
12. Matumizi shirikishi ya masoko ya kisasa kwenye miji mbalimbali Tanzania kama Kisutu-Dar, Chifu Kingalu VI-Morogoro, Chuno-Mtwara, Mwanza, Mwanjelwa-Mbeya
13. Ujenzi wa daraja Kigongo-Busisi (Mwanza-Sengerema)
14. Ujenzi wa Meli Kubwa ziwa Viktoria umefikia wapi kama walivyoanza waKorea?
15. Ujenzi na uendeshaji wa kiwanda cha sukari huko Morogoro vijijini (Mbigiri Sugar Factory) chini ya ufadhili wa NSSF umefikia wapi?
16. Upanuzi wa barabara ya Dar-Lindi/Mtwara umefikia wapi?
17. Ujenzi wa masoko mapya ya kisasaa Arusha na Moshi mjini umefikia wapi?
18. Kufufuliwa kwa hoteli ya Musoma (Musoma hotel) umefikia wapi?
19. Ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa Serengeti kama kivutio kikuu cha utalii Tanzania umefikia wapi?
20. Kuanza kwa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Tongoleani Tanga utaanza lini?
21. Ufufuaji na ujenzi wa meli ya mizigo ziwa Tanganyika na Nyasa umefikia wapi?
22. Kufikisha umeme wa gridi ya Taifa Kigoma utakamilika lini ili kuondoa matumizi ya jenereta za mafuta?
23. Vinu vya kuchenjulia makinikia na kuongeza ubora wa madini Kahama na Mwanza vitakamilika lini?
24. Ununuzi wa ndege ya mizigo mali ya Tanzania utafanyika lini?
Nk.,
 
kichwa kinauma, ngoma nzito, dereva jasho linamtoka
 
Back
Top Bottom