Miradi ya majengo iliyotelekezwa na mashirika kama NHC ni hasara ya nani?

Miradi ya majengo iliyotelekezwa na mashirika kama NHC ni hasara ya nani?

Nyumisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
13,499
Reaction score
19,292
Juzi kati nilipita maeneo ya kawe nikashuhudia majengo ya maghorofa yakiwa magofu yakionyesha hali ya kutelekezwa, kuulizia nikaambiwa ni majengo ya NHC.

Hivi ni kwa nini pesa za umma zitumike kuanzisha miradi ambayo haifiki mwisho ili kuleta tija na wala hakuna mtu yoyote anayewajibika kwa hilo na badala yake tunakuja kuwakamua wanyonge kwa kuwalundikia tozo?
 
Serikalini ndiyo sehemu ambayo uzembe na kutowajibika, mtumishi anaweza kufanya.
 
Juzi kati nilipita maeneo ya kawe nikashuhudia majengo ya maghorofa yakiwa magofu yakionyesha hali ya kutelekezwa, kuulizia nikaambiwa ni majengo ya NHC.

Hivi ni kwa nini pesa za umma zitumike kuanzisha miradi ambayo haifiki mwisho ili kuleta tija na wala hakuna mtu yoyote anayewajibika kwa hilo na badala yake tunakuja kuwakamua wanyonge kwa kuwalundikia tozo?
Mkuu ulikuwa wapi past
 
NHC ilifungwa mikono na miguu. Hawakutelekeza hiyo miradi
 
Siyo NHC pekeyake hata Miradi NSSF mzizima Tower posta, NSSF hotel ya Capri point mwanza yote ilisimamishwa na mwendazake alipoingia madarakani 2015
 
Nadhani hayo majengo ndio yale ya 711 project ambayo ilipgiwa promo sana ila sasa naona mambo yamemuwa sio mambo, pia hii Morocco Square nayo mpaka sasa sioni dalili yeyote ya kutumika.

Nashangaa kwa nini mchina kaja na kujenga apartments pale victoria na palm village chap tu na kaaza kupiga vibunda. Tatizo liko wapi haswa?
 
Back
Top Bottom