Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Waislamu duniani mara zote wanapopatwa na shida walitegemea wapate utetezi wa hali ya juu kutoka kwa utawala wa Saudi Arabia kwanza kabla ya kwengine kokote.Misaad hiyo ingeweza kuwa ya kimali,kijeshi na hata kauli za kisiasa.
Kinyume chake mara zote kumetokea maangamizi mabaya kwa waislamu bila kupata chochote kati ya hivyo kutoka kwao.Mfano wa maangamizi yaliyofanywa China kwa waislamu wa Uiyghur.Vile vile kule India tangu msikiti wa Babri ulipovunjwa.
Madhila mengine iliyokalia kimya na utwawala huo ni uchomaji moto wa nyumba za waislamu na kuuliwa kulikofanywa na mabuda kule Myamar.
Yote hayo yalionekana labda kwa vile yako mbali na wao.Hili la Gaza ndio limeleta masuali zaidi.Ambacho amekifanya kupinga sera ya Israel kwa Palestina ni kidogo sana kuliko uwezo wake.Mwanamfalme MBS amekuwa akitoa matamko mepesi anapotembelewa na viongozi wanaoiunga mkono Israel,matamko ambayo hayavunji kiu ya Israel kuendelea kuwakandamiza wapalestina.
Kuna muda baadhi ya waislamu walisema mwanamfalme huyo ni kizazi cha kiyahudi ndio maana huwa anawaunga mkono Israel kimya kimya.Hata hivyo hilo limeonekana kutokuwa na mashiko kwa kuzingatia historia ya makuzi yake na alipopatia elimu yake ya sheria.
Kwa mujibu wa baadhi ya wachambuzi ulimbukeni wake wa kutaka kuiga mila za kizungu na starehe zao ndhicho kilichomfanya awe hivyo anavyoonekana.
Tangu ajimilikishe ufalme kwa nguvu kwa kuwaondoa wenzake waliokuwa warithi wa kiti hicho amekuwa akibuni miradi ya ajabu ajabu inayokusudiwa kuibadili Saudi Arabia iwe nchi ya kisasa zaidi na eneo la starehe kuliko sehemu yoyote duniani.
Katika mpango huo magari yatakuwa yakiruka na kutua juu ya nyumba za wakazi wa miji hiyo mipya na kila kitu mtu atakuwa akikipata kwa kubonyeza kitufe tu kutoa amri.Hakutakuwa na kizuizi cha mtu kufanya alipendalo ikiwemo matamanio yake ya kimwili.
Katika miradi hiyo yenye majina ya kiulaya kama DAVOS na EXPO 2030 eneo lote la ufukwe wa bahari nyekundu umeshapata sura tofauti kutoka uasili yake.Viongozi wa kikabila waliokuwa na makazi yao maeneo hayo na waliopinga miradi hiyo kwa hoja za kiimani na kimazingjira ama wameuliwa au hawajulikani walipo.
Kutokea kwa mzozo mkubwa wa kivita katika eneo la mashariki ya kati baina ya Palestina na Israel na kabla ya hapo mzozo wa kule Ukraine baina ya Urusi na jirani yake huyo kumekuwa kama kumetibua mipango mingi ya miradi hiyo.
Watekelezaji wakubwa wa miradi hiyo ni makampuni makubwa ya kimataifa ambapo kila mwenye ubunifu wake alikaribishwa aupeleke kwenye maeneo hayo.
Tatizo lililojitokeza kwa makampuni hayo ni kuwa baadhi yao sasa wamezipuuza fursa walizopewa kutokana na ukata wa kiuchumi kiasi kwamba makampuni hayo yanatoa nyudhuru za kutokuwa na nauli na gharama za hata kupeleka wawakilishi wao kwenye mikutano muhimu ya kupanga miji hiyo ianayokusudiwa kuwa kama pepo ya dunia.
Kuingia mguu katika miradi hiyo na hamu ya kutaka kuiokoa inaweza kuwa ndiyo sababu ya ukimya na kutokuwa na ukakamavu wa kutetea wapalestina wanaouliwa kwa kukatiwa maji,kunyimwa chakula na kupigwa mabomu mfululizo kutoka angani na kuvamiwa majumbani mwao usiku na mchana.