Miradi ya mwanamfalme MBS kuibadili Saudi Arabia kuwa pepo ya dunia yaingia ukorofi

Miradi ya mwanamfalme MBS kuibadili Saudi Arabia kuwa pepo ya dunia yaingia ukorofi

Kwanini unaita hamasa na jazba za kijinga?
Kwa sababu ziko kinyume na Elimu na usawa na hazina manufaa kwa ummah bali uharibifu. Vijana wanaharakati hawataki kuwasikiliza wanachuoni wanaofuata njia ya wema waliotangulia. Wanafuata emotions zao tu.
Huoni kwamba kila kinachoendelea kwenye hili suala la Palestina kinadhihirisha udhaifu na unafiki kwenye ummah wa Kiislam?
Ama kuhusu unafiki sijui umemaanisha nini ila udhaifu ni kwa sababu ya kuacha na kulegea kwetu katika Dini yetu. Tunaiacha njia ya wema waliotangulia. Huoni wewe leo hii wengi wetu tumeiacha Tawhid na kuzing'ang'ania Shirki? Wangapi leo wanaomba wafu bado? Wangapi leo tumeshikilia imani zisizofaa na itikadi zisizo sawa? Na kadhalika? Tumeacha Sunnah na kuidharau. Bali kuna wanaoipiga vita. Vipi ushindi utakuja?
Nusra haitopatikana kwa kutia huruma na kuomba sana,...Bali nusra itapatikana kwa kuingia kwenye vita,...jino Kwa jino, jicho Kwa jicho, mguu Kwa mguu, Bomu Kwa Bomu,.... Hiyo ndiyo kanuni toka enzi na enzi,
Nusra haiji ila kwa kurudi katika Dini yetu kwanza. Na jambo la mwanzo ni kumpwekesha Allah kiukweli bila ya kumshirikisha na chochote. Na kuzisafisha nyoyo zetu kuondoa itikadi chafu na imani zisizofaa. Vipi utapambana na mayahudi na huwezi kupambana na nafsi yako kwanza?
Zama hizi zimekosa kina Khalid bin Waleed,Umar Al Farouq, Salahuddin Ayoub
Khaleed Ibn Waleed na Umar Al Farouq (Radhi za Allah ziwe juu yao) na Maswahaba wenzao (Radhi za Allah ziwe juu yao) walikuwa na itikadi za sawa. Walimpwekesha Allah wala hawakumshirikisha na chochote. Hawakuwa wakiomba wafu; hawakuwa wakiomba dua kwa mitume kutaka misaada kwenye makaburi yao, hawakuvaa hirizi, hawakuwa wakitukuza makaburi, wakinyanyua mikono kuomba wanamuomba Allah peke yake, hawakuamini mambo ya nyota wala kuamini kuna nuksi katika ndege wala katika siku au mwezi fulani, walipenda kwa ajili ya Allah na walichukia kwa ajili ya Allah, waliamini katika Qadar kiusahihi kabisa, walizithibitisha na kuziamini sifa na majina ya Allah kama alivyojisifia Yeye Mwenyewe katika Kitabu chake au kupitia kinywa cha Mtume wake (Swala na Salamu ziwe juu yake) bila ya Tahreef (kuzipotosha), Ta'teel (kuzikanusha), Takyeef (kusema zikoje/namna yake ikoje) wala Tamtheel (kuzimithilisha). Kiufupi walikuwa wamesimama sawa katika Tawhid.

Na walikuwa wanaifuata Sunnah ya Mtume wala hawakuikhalifu, wala hawakuzusha katika Dini, wala hawakuwa wakileta ubishi pale walipokuwa wakiambiwa wamfuate Mtume bali waliifuata Sunnah ya Mtume. Hebu tazama mfano mmoja tu kutoka kwa Umar ibn Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yake) ambaye umemtaja hapo, pindi alipochomwa kisu na yuko katika moments zake za mwisho lakini bado anamnasihi mmoja katika vijana waliokuja kumtembelea kuwa asiiburuze nguo yake alipoona nguo ya kijana inaburuza. Jinsi alivyokuwa haipuuzii Sunnah na jinsi alivyokuwa ni mwenye kushikamana nayo mno. Huyo ndio Amir wa Waumini 'Umar. Je, tunafuata njia yao? Bali wengi wetu ni wenye kuipuuza njia yao waliyoifuata.

Hata Salahuddin (Allah amrehemu) alikuwa ni katika waliosimama sawa katika Dini.

Nusra iliwajia kwa sababu walisimama sawa. Ila leo hii mnaamini watu ambao hawako sawa, tena kwa kushirikiana na wale wanaowatukana na kuwakufurisha wale mashujaa na wabora wa mwanzo kama Umar Al Farouq, Khalid Ibn Walid na wanaowatukana mashujaa wa baadae akina Salahuddin, eti nusra itashuka kwao.
History often reveals that honor and freedom are sometimes secured through the sacrifices made on the battlefield, where actions speak louder than words.
Soma Surah An Nur aya ya 55, uione ahadi ya Allah.
@Baljurashi The Messenger himself (Alayhi Salam) was a Warrior na hajawahi kutia huruma dhidi ya dhulma.
Mtume kakaa Makkah miaka 13 katika utume wake, hakunyanyua silaha dhidi ya washirikina wala kupigana nao. Na Waislam walikuwa wanyonge na dhaifu wananyanyaswa na kukumbwa na mateso makubwa tena katika mji wa Makkah ambao ni bora kuliko ardhi ya Al Quds na Msikiti wa Makkah ambao ni mtukufu zaidi kuliko Masjid Al aqsa. Bali alichokuwa anakifanya ni kuita na kulingania katika Tawhid, kuzisafisha imani na itikadi za Maswahaba zake na kuwausia subra.
Qala wa Qala Wa Qala zisiwe nyingi.....
Tuache hamasa na jazba jazba

View: https://youtu.be/YQcD_2pr_rE?si=SvigyBl1FdDHUpbS
 
Waislamu duniani mara zote wanapopatwa na shida walitegemea wapate utetezi wa hali ya juu kutoka kwa utawala wa Saudi Arabia kwanza kabla ya kwengine kokote.Misaad hiyo ingeweza kuwa ya kimali,kijeshi na hata kauli za kisiasa.
Kinyume chake mara zote kumetokea maangamizi mabaya kwa waislamu bila kupata chochote kati ya hivyo kutoka kwao.Mfano wa maangamizi yaliyofanywa China kwa waislamu wa Uiyghur.Vile vile kule India tangu msikiti wa Babri ulipovunjwa.
Madhila mengine iliyokalia kimya na utwawala huo ni uchomaji moto wa nyumba za waislamu na kuuliwa kulikofanywa na mabuda kule Myamar.
Yote hayo yalionekana labda kwa vile yako mbali na wao.Hili la Gaza ndio limeleta masuali zaidi.Ambacho amekifanya kupinga sera ya Israel kwa Palestina ni kidogo sana kuliko uwezo wake.Mwanamfalme MBS amekuwa akitoa matamko mepesi anapotembelewa na viongozi wanaoiunga mkono Israel,matamko ambayo hayavunji kiu ya Israel kuendelea kuwakandamiza wapalestina.
Kuna muda baadhi ya waislamu walisema mwanamfalme huyo ni kizazi cha kiyahudi ndio maana huwa anawaunga mkono Israel kimya kimya.Hata hivyo hilo limeonekana kutokuwa na mashiko kwa kuzingatia historia ya makuzi yake na alipopatia elimu yake ya sheria.
Kwa mujibu wa baadhi ya wachambuzi ulimbukeni wake wa kutaka kuiga mila za kizungu na starehe zao ndhicho kilichomfanya awe hivyo anavyoonekana.
Tangu ajimilikishe ufalme kwa nguvu kwa kuwaondoa wenzake waliokuwa warithi wa kiti hicho amekuwa akibuni miradi ya ajabu ajabu inayokusudiwa kuibadili Saudi Arabia iwe nchi ya kisasa zaidi na eneo la starehe kuliko sehemu yoyote duniani.
Katika mpango huo magari yatakuwa yakiruka na kutua juu ya nyumba za wakazi wa miji hiyo mipya na kila kitu mtu atakuwa akikipata kwa kubonyeza kitufe tu kutoa amri.Hakutakuwa na kizuizi cha mtu kufanya alipendalo ikiwemo matamanio yake ya kimwili.
Katika miradi hiyo yenye majina ya kiulaya kama DAVOS na EXPO 2030 eneo lote la ufukwe wa bahari nyekundu umeshapata sura tofauti kutoka uasili yake.Viongozi wa kikabila waliokuwa na makazi yao maeneo hayo na waliopinga miradi hiyo kwa hoja za kiimani na kimazingjira ama wameuliwa au hawajulikani walipo.
Kutokea kwa mzozo mkubwa wa kivita katika eneo la mashariki ya kati baina ya Palestina na Israel na kabla ya hapo mzozo wa kule Ukraine baina ya Urusi na jirani yake huyo kumekuwa kama kumetibua mipango mingi ya miradi hiyo.
Watekelezaji wakubwa wa miradi hiyo ni makampuni makubwa ya kimataifa ambapo kila mwenye ubunifu wake alikaribishwa aupeleke kwenye maeneo hayo.
Tatizo lililojitokeza kwa makampuni hayo ni kuwa baadhi yao sasa wamezipuuza fursa walizopewa kutokana na ukata wa kiuchumi kiasi kwamba makampuni hayo yanatoa nyudhuru za kutokuwa na nauli na gharama za hata kupeleka wawakilishi wao kwenye mikutano muhimu ya kupanga miji hiyo ianayokusudiwa kuwa kama pepo ya dunia.
Kuingia mguu katika miradi hiyo na hamu ya kutaka kuiokoa inaweza kuwa ndiyo sababu ya ukimya na kutokuwa na ukakamavu wa kutetea wapalestina wanaouliwa kwa kukatiwa maji,kunyimwa chakula na kupigwa mabomu mfululizo kutoka angani na kuvamiwa majumbani mwao usiku na mchana.

Mkuu uislamu wa vita na visasi,kuchukia na kutenga wasio waislamu umepitwa na wakati dunia ya sasa imeshatoka huko siku nyingi. Wamebaki wajinga wachache nao taratibu wanaisha wanao kaza fuvu wanaishia kifo kibaya.

MBS anafahamu jinsi dunia inavyofanya kazi kila mwanadamu anahaki sawa juu ya uso wa nchi kuishi na kuamini kile anacho kiamini.

Middle east ya sasa sio ya zamani na haitokuja kuwa kama ya zamani mana westernization inazidi kuenea kwa kasi. Dubai sasahivi ni kama ulaya na watu wanaenjoy maisha dini za kale zilitutengenezea ukuta badala ya madaraja kati yetu.

Yesu Akbar.
 
Kwa hiyo hawa Waislam huchokonoa dunia wakitegemea kutetewa na Saudi.
 
Kama kawaida mshaanza kuilaumu Saudi Arabia. Wanaharakati mna nini?

Tunaumia mno kwa yanayowakuta ndugu zetu kule Gaza lakini hamasa za kijinga hazifai. Na hizi hamasa na jazba za kijinga hazileti manufaa bali madhara zaidi kwa Ummah. Hivi hamuoni?

Yaani mpaka katika vipindi vigumu kama hivi bado mnaendelea kuleta fitna tu na uchochezi?

Allah awanusuru ndugu zetu huko Palestina na ndugu zetu wanaoteseka kwengine kote duniani na awape ushindi dhidi ya adui zake na adui zao.

View attachment 2796402
105. Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.
(Qur-an 21:105)

Hapa ndio hua naona kurwan inazingua,zaburi na kumbukumbu la torati ni vitabu vya wayahudi na vimezungumzia mambo mengi sana at least kurwan inge qoute hivyo vifungu.
 
Kwanini unaita hamasa na jazba za kijinga?
Huoni kwamba kila kinachoendelea kwenye hili suala la Palestina kinadhihirisha udhaifu na unafiki kwenye ummah wa Kiislam?

Nusra haitopatikana kwa kutia huruma na kuomba sana,...Bali nusra itapatikana kwa kuingia kwenye vita,...jino Kwa jino, jicho Kwa jicho, mguu Kwa mguu, Bomu Kwa Bomu,.... Hiyo ndiyo kanuni toka enzi na enzi,

Zama hizi zimekosa kina Khalid bin Waleed,Umar Al Farouq, Salahuddin Ayoub,
Wamebaki viongozi wanaoitisha matamasha ya kina Shakira huko mjini Riyadh Saudia,..na matamasha ya Boxing.

History often reveals that honor and freedom are sometimes secured through the sacrifices made on the battlefield, where actions speak louder than words.

Baljurashi The Messenger himself (Alayhi Salam) was a Warrior na hajawahi kutia huruma dhidi ya dhulma.

Qala wa Qala Wa Qala zisiwe nyingi.....

Sasa mbona kipigo kikienda kwa wapalestina mnarudi kulialia ingieni ulingoni tuone kazi achaneni na hashtags na kutaka kuonewa huruma wakati kanuni mnaijua.
 
Lawama upande wetu hazina mashiko sana kwani tuko mbali na hatuna nguvu zozote za kimali wala kijeshi.Lawama zitakwenda kwao hasa hasa hao Saudia,Misri na Jordan.
tani ya ngano ya kazi gani kuipeleka Gaza.Kama ni kiasi hicho tupeleke hapo Congo.
Wapeleke Kongo wakiti WA tz Hali ngumu
 
Sasa mbona kipigo kikienda kwa wapalestina mnarudi kulialia ingieni ulingoni tuone kazi achaneni na hashtags na kutaka kuonewa huruma wakati kanuni mnaijua.
Okay,..wamalizeni wote mnaowachukia ili muishi Kwa raha kwenye Dunia.
 
Sasa mbona kipigo kikienda kwa wapalestina mnarudi kulialia ingieni ulingoni tuone kazi achaneni na hashtags na kutaka kuonewa huruma wakati kanuni mnaijua.
Tukitaka kuonewa huruma hatuombi kwa binadamu.Tunachofanya kwa binadamu wenzetu wenye madaraka ni kuwazindua kwa kuwaonea huruma.
 
Kwanza sio kweli kuwa Waislam popote duniani wanapopata shida wanamtegemea Saudia.

Hayo ni mawazo yako tu na sio uhalisia ulivyo
KSA wanasaidia sana nchi nyingi tu na sio za kiislam tu
Lakini pia Ufalme kumbuka wana mikataba na makampuni makubwa ya uchimbaji wa mafuta kama Aramco na wazungu

MbS yeye alichukua hiyo post kibabe sio kwa ndugu zake bali ni post moja tu na ilikuwa ya Baba yake mdogo na kumuweka kizuizini na kujiweka yeye karibu zaidi na Ufalme

Ni kweli ana mambo ya kimagharibi zaidi na aliwaweka jela Hoteli ndugu zake wengi na kuwaambia kutoka lazima mrudishe hela mlizojilimbikizia

MbS, Magu, Modi, na Trump waliingia wakati mmoja madarakani au walipishana miezi na wote walikuja na mbwembwe za kila aina

Nikajisemea Dunia safari hii imevamiwa haswa
Ila Saudia kama kashindwa hiyo miradi basi ni ujinga wake wa kukurupuka kama baadhi ya viongozi wengine tu

Ila kuisaidia Gaza moja kwa moja kivita hawezi lakini misaada ya kibinadamu wanatoa nchi nyingi sana

Ila sisi ndio wanafiki kwani uwezo wa tani kadhaa za ngano na sukari hatushindwi lakini hatuna tabia ya kutoa na kujali wanaohitaji maana hili linaanzia nyumbani na viongozi walipitia malezi pia

Viongozi wetu ni walafi na wanafiki huwezi kusikia wakiliongelea bungeni
Yaani kusema..........wapigane wenyewe sisi tutoe ngano na sukari uko sawa wewe? Kira mtu ashinde mechi zake...........wakiona inauma wataacha ugomvi
 
Yaani kusema..........wapigane wenyewe sisi tutoe ngano na sukari uko sawa wewe? Kira mtu ashinde mechi zake...........wakiona inauma wataacha ugomvi
Sio lazima kutoa kwani sisi ni tabia zetu za majibu ya hivyo hata Rais aliepita alikuwa anasema kwa wananchi wake
"Kwani mimi ndio nimeleta tetemeko?
Basi acha wapambane nao
.
 
Una roho katili sana wewe
Mwenye roho katili ni yule aliewadharau wana Kagera na kuwatukana
Wewe niambie umechangia hata senti kwa wapalestina?
Unajua hata wanaokusanya hela kila leo kuwasaidia
Roho mbaya mnayo nyie mnaopeleka michango na sadaka kwa mtu mmoja huku ukimpita masikini anaeomba barabarani

Nimesema waswahili hamna tabia ya kusaidia sasa unanishambulia mimi wakati niko tofauti na nyie ?
 
Kauli zako hazina takwimu kuthibitisha nani mwenye roho mbaya kati yangu na wewe
 
Waislamu duniani mara zote wanapopatwa na shida walitegemea wapate utetezi wa hali ya juu kutoka kwa utawala wa Saudi Arabia kwanza kabla ya kwengine kokote.Misaad hiyo ingeweza kuwa ya kimali,kijeshi na hata kauli za kisiasa.
Kinyume chake mara zote kumetokea maangamizi mabaya kwa waislamu bila kupata chochote kati ya hivyo kutoka kwao.Mfano wa maangamizi yaliyofanywa China kwa waislamu wa Uiyghur.Vile vile kule India tangu msikiti wa Babri ulipovunjwa.
Madhila mengine iliyokalia kimya na utwawala huo ni uchomaji moto wa nyumba za waislamu na kuuliwa kulikofanywa na mabuda kule Myamar.
Yote hayo yalionekana labda kwa vile yako mbali na wao.Hili la Gaza ndio limeleta masuali zaidi.Ambacho amekifanya kupinga sera ya Israel kwa Palestina ni kidogo sana kuliko uwezo wake.Mwanamfalme MBS amekuwa akitoa matamko mepesi anapotembelewa na viongozi wanaoiunga mkono Israel,matamko ambayo hayavunji kiu ya Israel kuendelea kuwakandamiza wapalestina.
Kuna muda baadhi ya waislamu walisema mwanamfalme huyo ni kizazi cha kiyahudi ndio maana huwa anawaunga mkono Israel kimya kimya.Hata hivyo hilo limeonekana kutokuwa na mashiko kwa kuzingatia historia ya makuzi yake na alipopatia elimu yake ya sheria.
Kwa mujibu wa baadhi ya wachambuzi ulimbukeni wake wa kutaka kuiga mila za kizungu na starehe zao ndhicho kilichomfanya awe hivyo anavyoonekana.
Tangu ajimilikishe ufalme kwa nguvu kwa kuwaondoa wenzake waliokuwa warithi wa kiti hicho amekuwa akibuni miradi ya ajabu ajabu inayokusudiwa kuibadili Saudi Arabia iwe nchi ya kisasa zaidi na eneo la starehe kuliko sehemu yoyote duniani.
Katika mpango huo magari yatakuwa yakiruka na kutua juu ya nyumba za wakazi wa miji hiyo mipya na kila kitu mtu atakuwa akikipata kwa kubonyeza kitufe tu kutoa amri.Hakutakuwa na kizuizi cha mtu kufanya alipendalo ikiwemo matamanio yake ya kimwili.
Katika miradi hiyo yenye majina ya kiulaya kama DAVOS na EXPO 2030 eneo lote la ufukwe wa bahari nyekundu umeshapata sura tofauti kutoka uasili yake.Viongozi wa kikabila waliokuwa na makazi yao maeneo hayo na waliopinga miradi hiyo kwa hoja za kiimani na kimazingjira ama wameuliwa au hawajulikani walipo.
Kutokea kwa mzozo mkubwa wa kivita katika eneo la mashariki ya kati baina ya Palestina na Israel na kabla ya hapo mzozo wa kule Ukraine baina ya Urusi na jirani yake huyo kumekuwa kama kumetibua mipango mingi ya miradi hiyo.
Watekelezaji wakubwa wa miradi hiyo ni makampuni makubwa ya kimataifa ambapo kila mwenye ubunifu wake alikaribishwa aupeleke kwenye maeneo hayo.
Tatizo lililojitokeza kwa makampuni hayo ni kuwa baadhi yao sasa wamezipuuza fursa walizopewa kutokana na ukata wa kiuchumi kiasi kwamba makampuni hayo yanatoa nyudhuru za kutokuwa na nauli na gharama za hata kupeleka wawakilishi wao kwenye mikutano muhimu ya kupanga miji hiyo ianayokusudiwa kuwa kama pepo ya dunia.
Kuingia mguu katika miradi hiyo na hamu ya kutaka kuiokoa inaweza kuwa ndiyo sababu ya ukimya na kutokuwa na ukakamavu wa kutetea wapalestina wanaouliwa kwa kukatiwa maji,kunyimwa chakula na kupigwa mabomu mfululizo kutoka angani na kuvamiwa majumbani mwao usiku na mchana.
Saudi Arabia ni nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta, pia ni nchi ilyoendelea zaidi kuliko nchi nyingine yoyote ile ktk Arab world. Lakini kutokana utawala wa Saudi Arabia kuwa na sera za misimami mikali zaidi ya 'kibedui', utawala wa sheria kali zsidi za kislamu (Sharia), kukosekana kwa utawala bora wa Kidemokrasia na kuwepo kwa utawala wa kifalme na wa kidikteta, wananchi wa nchi hiyo wamejikuta kuwa ni 'mateka wa watawala, ' hawafaidiki chochote kutokana na utajiri mkubwa wa mafuta uliopo ktk nchi yao na wekuwa hawako huru na kukosa furaha na amani ktk nyanja zote za maisha yao ya kila siku na mwisho kuoneka kuwa ni miongoni mwa watu wanaoishi kwenye umaskini wa kutupwa hapa duniani.
 
Nchi yoyote inayotawaliwa na wafalme haina maana hata chembe.Wanawakandamiza raia kwa faida zao za kidunia na hawakumbuki akhera kabisa.Wako tayari kufanywa vibaraka ilimradi wabaki madarakani.
Hamas wakimaliza kazi Israel na hawa nao wasiwawache wakaendeleza ujinga wao.
 
Saudi Arabia's 100-Mile Skyscraper Is Turning Into a Disaster

Saudi Arabia's plans for Neom, a futuristic fever dream which includes a massive all-inclusive resort on the coast, a second ski resort in the mountains, and an up to 106 miles-long pair of 1,600-foot skyscrapers called The Line, is running into major financial problems.
 
Back
Top Bottom