Miradi ya mwanamfalme MBS kuibadili Saudi Arabia kuwa pepo ya dunia yaingia ukorofi

Miradi ya mwanamfalme MBS kuibadili Saudi Arabia kuwa pepo ya dunia yaingia ukorofi

Kwa sababu ziko kinyume na Elimu na usawa na hazina manufaa kwa ummah bali uharibifu. Vijana wanaharakati hawataki kuwasikiliza wanachuoni wanaofuata njia ya wema waliotangulia. Wanafuata emotions zao tu.

Ama kuhusu unafiki sijui umemaanisha nini ila udhaifu ni kwa sababu ya kuacha na kulegea kwetu katika Dini yetu. Tunaiacha njia ya wema waliotangulia. Huoni wewe leo hii wengi wetu tumeiacha Tawhid na kuzing'ang'ania Shirki? Wangapi leo wanaomba wafu bado? Wangapi leo tumeshikilia imani zisizofaa na itikadi zisizo sawa? Na kadhalika? Tumeacha Sunnah na kuidharau. Bali kuna wanaoipiga vita. Vipi ushindi utakuja?

Nusra haiji ila kwa kurudi katika Dini yetu kwanza. Na jambo la mwanzo ni kumpwekesha Allah kiukweli bila ya kumshirikisha na chochote. Na kuzisafisha nyoyo zetu kuondoa itikadi chafu na imani zisizofaa. Vipi utapambana na mayahudi na huwezi kupambana na nafsi yako kwanza?

Khaleed Ibn Waleed na Umar Al Farouq (Radhi za Allah ziwe juu yao) na Maswahaba wenzao (Radhi za Allah ziwe juu yao) walikuwa na itikadi za sawa. Walimpwekesha Allah wala hawakumshirikisha na chochote. Hawakuwa wakiomba wafu; hawakuwa wakiomba dua kwa mitume kutaka misaada kwenye makaburi yao, hawakuvaa hirizi, hawakuwa wakitukuza makaburi, wakinyanyua mikono kuomba wanamuomba Allah peke yake, hawakuamini mambo ya nyota wala kuamini kuna nuksi katika ndege wala katika siku au mwezi fulani, walipenda kwa ajili ya Allah na walichukia kwa ajili ya Allah, waliamini katika Qadar kiusahihi kabisa, walizithibitisha na kuziamini sifa na majina ya Allah kama alivyojisifia Yeye Mwenyewe katika Kitabu chake au kupitia kinywa cha Mtume wake (Swala na Salamu ziwe juu yake) bila ya Tahreef (kuzipotosha), Ta'teel (kuzikanusha), Takyeef (kusema zikoje/namna yake ikoje) wala Tamtheel (kuzimithilisha). Kiufupi walikuwa wamesimama sawa katika Tawhid.

Na walikuwa wanaifuata Sunnah ya Mtume wala hawakuikhalifu, wala hawakuzusha katika Dini, wala hawakuwa wakileta ubishi pale walipokuwa wakiambiwa wamfuate Mtume bali waliifuata Sunnah ya Mtume. Hebu tazama mfano mmoja tu kutoka kwa Umar ibn Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yake) ambaye umemtaja hapo, pindi alipochomwa kisu na yuko katika moments zake za mwisho lakini bado anamnasihi mmoja katika vijana waliokuja kumtembelea kuwa asiiburuze nguo yake alipoona nguo ya kijana inaburuza. Jinsi alivyokuwa haipuuzii Sunnah na jinsi alivyokuwa ni mwenye kushikamana nayo mno. Huyo ndio Amir wa Waumini 'Umar. Je, tunafuata njia yao? Bali wengi wetu ni wenye kuipuuza njia yao waliyoifuata.

Hata Salahuddin (Allah amrehemu) alikuwa ni katika waliosimama sawa katika Dini.

Nusra iliwajia kwa sababu walisimama sawa. Ila leo hii mnaamini watu ambao hawako sawa, tena kwa kushirikiana na wale wanaowatukana na kuwakufurisha wale mashujaa na wabora wa mwanzo kama Umar Al Farouq, Khalid Ibn Walid na wanaowatukana mashujaa wa baadae akina Salahuddin, eti nusra itashuka kwao.

Soma Surah An Nur aya ya 55, uione ahadi ya Allah.

Mtume kakaa Makkah miaka 13 katika utume wake, hakunyanyua silaha dhidi ya washirikina wala kupigana nao. Na Waislam walikuwa wanyonge na dhaifu wananyanyaswa na kukumbwa na mateso makubwa tena katika mji wa Makkah ambao ni bora kuliko ardhi ya Al Quds na Msikiti wa Makkah ambao ni mtukufu zaidi kuliko Masjid Al aqsa. Bali alichokuwa anakifanya ni kuita na kulingania katika Tawhid, kuzisafisha imani na itikadi za Maswahaba zake na kuwausia subra.

Tuache hamasa na jazba jazba

View: https://youtu.be/YQcD_2pr_rE?si=SvigyBl1FdDHUpbS

Kwahiyo mkuu hawa waislam wa leo wanaomba wafu na makaburi? Wala hawamuombi MUNGU MWENYEZI tena
 
Wtan
Kwanza sio kweli kuwa Waislam popote duniani wanapopata shida wanamtegemea Saudia.

Hayo ni mawazo yako tu na sio uhalisia ulivyo
KSA wanasaidia sana nchi nyingi tu na sio za kiislam tu
Lakini pia Ufalme kumbuka wana mikataba na makampuni makubwa ya uchimbaji wa mafuta kama Aramco na wazungu

MbS yeye alichukua hiyo post kibabe sio kwa ndugu zake bali ni post moja tu na ilikuwa ya Baba yake mdogo na kumuweka kizuizini na kujiweka yeye karibu zaidi na Ufalme

Ni kweli ana mambo ya kimagharibi zaidi na aliwaweka jela Hoteli ndugu zake wengi na kuwaambia kutoka lazima mrudishe hela mlizojilimbikizia

MbS, Magu, Modi, na Trump waliingia wakati mmoja madarakani au walipishana miezi na wote walikuja na mbwembwe za kila aina

Nikajisemea Dunia safari hii imevamiwa haswa
Ila Saudia kama kashindwa hiyo miradi basi ni ujinga wake wa kukurupuka kama baadhi ya viongozi wengine tu

Ila kuisaidia Gaza moja kwa moja kivita hawezi lakini misaada ya kibinadamu wanatoa nchi nyingi sana

Ila sisi ndio wanafiki kwani uwezo wa tani kadhaa za ngano na sukari hatushindwi lakini hatuna tabia ya kutoa na kujali wanaohitaji maana hili linaanzia nyumbani na viongozi walipitia malezi pia

Viongozi wetu ni walafi na wanafiki huwezi kusikia wakiliongelea bungeni

Wabongo ndiyo watoe msaada wa tani ya ngano?😂😂 Wao wenyewe wananunua ngano toka nje!
 
Back
Top Bottom