Mirathi kwa watoto nje ya Ndoa

Dini ipi ya kikristo au Kiislamu

Lakini pia kama dini inatambua hivyo ni Kwanini sasa mahakama inaenda kinyume ilihali mahakama inatambua sheria za mila, sheria za kidini nk

Dini ya Kiislamu.
Mahakama za Tanzania hazitoi hukumu zake kwa kutegemea sheria za dini.
 
Hii inaitwa mkanganyiko wa kisheria
 
Kwa hio?
Ibn zinaa maanake nini kwa kiswahili maarufu? Usilete hapa ubishi wenu wa kiwahabi right.
mtoto aliyetokana na zinaa ( wa kiume) ila hajaitwa wa haram, hiyo haramu ni matusi ya walimwengu
 
Mimi sio mtaalamu wa haya mambo ila kina rafiki yangu yeye na mme wake ni wakristo na mme kafariki mwaka juzi. Watoto wa mke wa ndoa ni wakubwa wote wana maisha yao halafu kuna kengine mme alizaa nje hat hajafika 10 years. Mme hakuacha wosia. Ila mahakama hawakumpa haki huyyu mtoto wa nje kwa kuwa mke wa ndoa ndio alikuwa main bread winner. Sana sana nyumba ya kijijini kwa baba ake ndio baba ake alijenga ikaamuliwa either iuzwe ili asomeshe au ipangishwe isaidie huyu mtoto wa nje. Lakini zile investments kubwa zote ni jasho la mke wa ndoa so watoto wake wanastahili kufaidi jasho la mama yao.
 
Dini ya Kiislamu.
Mahakama za Tanzania hazitoi hukumu zake kwa kutegemea sheria za dini.
Okey,
Sasa unakuta watoto wa nje wana miaka chini ya 18

Na watoto wa ndoa wako above 18

Kwenye mgao kama watoto wote wana haki pia sheria inaanglia umri watoto wenye umri mdogo watapewa zaidi, sasa kwa kesi hiyo hao watoto wa nje ambao wapo chini ya miaka 18 watapewa zaidi kuliko wa watoto wa ndoa hii imekaaje mkuu, yani kama pesa wawo wana mgao mkubwa kwenye hili mahakama wanalitekelezaje?
 
Safi sana umetoa mfano mzuri sana, hilo linawezekana ndiyo, na ndoa za kikristo zina masharti sana, kuna wakati mke wa ndoa wa marehemu ambae alifunga ndoa ya kikristo ya mke mmoja na mume mmoja yeye kama yeye anapewa usimamizi na kumiliki mali za mume wake kama kuna mtoto wa nje ni yeye akiamua kugawa au lahasha.
 
Ndiyo napitia sheria hapa mama watoto ili vimada wasije kukusumbua [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Wosia unasaidia sana, kuepusha mlolongo mrefu kama huu sasa
 
Usichoelewa haki inayotajwa ibara ya 19 ya katiba ni uhuru wa kuabudu na kueneza dini na siyo haki ya kutumia dini yako kubagua wengine.Limitation ya haki ni pale haki yako inapoingilia haki ya mwingine na ku undermine serikali.Tunachojadili hapa siyo haki ya kuabudu ni haki ya kurithi.Unajaribu kuchanganya mada eti ile kesi ya Kenya yule bwana alikuwa mwisilamu jina.Yule alikuwa mwisilamu na ndo maana mirathi iliamuliwa na Kadhi.Kwakuwa kwa mujibu wa sheria ya kiislamu haiwezi kutumika kuamua hatima ya asiye muislamu,mama na watoto wake walienda mahakama kuu na kisha rufaa na wakapata haki kwa kuwa jurisdiction ilikuwa ni high court na sheria husika ni .Unaweza Succession Act na si Islamic law kwakuwa mama na watoto hawakuwa waislamu kudai mbona haitokei Sana Ni kwamba mtu akiishi dini yake ni ngumu kuzaa nje ya ndoa na kwa waislamu wanaruhusa ya kuongeza mke hivyo katika urithi watoto na mama zao kuwa halali mbele ya sheria ya kiislamu.Ikitokea tofauti sheria ya kidini inapoteza jurisdiction juu ya shauri husika.Acha kuchanganya haki ya kuabudu na haki ya kurithi.
 
Dini ya Kiislamu.
Mahakama za Tanzania hazitoi hukumu zake kwa kutegemea sheria za dini.
Shehe,kwenye ndoa,talaka,mirathi sheria ya kiislamu na kimila zinatumika lakini pale ambapo wahusika wote ni waislamu na wanaishi Kama waislamu na Kama sheria husika haikinzani na sheria za nchi na katiba yake.Zinapokiuka sheria za nchi ama wahusika wa kesi siyo si wa dini hiyo basi sheria ya dini inawekwa kando.
 
Hapa Ni sawa,Tanzania Kwanza hakuna mtoto haramu,kama Kuna sheria inamtaja mtu hivyo hiyo sheria na taratibu Ni unconstitutional.Katika kumiliki mali kwa wanandoa Kuna Mali binafsi na Mali ya pamoja,kwa kesi hiyo dogo alistahili kurithi kwa baba yake tu.
 

Asante kwa elimu ndugu[emoji1431]
 

Ni hivi mkuu: mtoto aliezaliwa nje ya ndoa bila kujali umri wake harithi kabisa/chochote kwa baba yake na pia baba yake halazimiki kumhudumia. Anarithi tu kwa mama yake na ndie mwenye majukumu ya kumlea na kumtunza kwa kila kitu. Ama kuhusu mambo ya mahakama sijui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…