Mirathi kwa watoto nje ya Ndoa

Mirathi kwa watoto nje ya Ndoa

Ukienda mahakamani ukafungua shauri la right to custody,wataangalia maslahi ya mtoto na kama anajitambua nayeye ataulizwa akae upande upi,best interest of the child ikilalia kwako unapewa.
Hichi kipengele mbona watanzania wnegi hatukijui, kwa kweli sheria ni pana sana, shauri la right to custody ina maana watoto watamtegrmea mke halali wa ndoa au sijakuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAHAKAMA TANZANIA YASEMA HAKUNA MWANAHARAMU, ILA KUNA WAZAZI HARAMU TU.

Kuna hukumu-rejea ilitolewa tarehe 28/5/2020 na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kupitia Mh. Jaji Mlyambina.

Ni hukumu ya kesi ya mirathi no. 50 ya mwaka 2016 (ina maana kesi ilichukua miaka 4 kwisha).

Ishu ya msingi katika kesi hiyo ni kuna mume wa mtu alifariki bila ya kuacha wosia. Aliacha mke ambaye alikuwa amemuoa kwa ndoa ya kikristo na watoto wa ndoa hiyo, na wengine wa michepuko (nje ya ndoa).

Watoto wa nje ya ndoa wakaweka pingamizi la mirathi maana walikuwa wameenguliwa wasipate kitu na msimamizi wa mirathi hiyo ambaye ni mtoto wa ndoa.

Wakati wa uhai wake, marehemu alikuwa anawasomesha watoto hao (ambapo wengine tayari walikuwa ni watu wazima), vyeti vyao vya kuzaliwa vilikuwa na jina la marehemu kama baba mzazi, na alishawatambulisha kwa mama yake na ndugu zake wengine.

Mahakamani mama na dada wa marehemu walitoa ushahidi kwamba wanawatambua hao watoto kama watoto wa marehemu.

Upande wa wa kwenye ndoa walikataa DNA test kufanyika kupima kama hao ni watoto wa marehemu.

Katika hukumu yake, Mahakama ikatumia sheria zifuatazo:

1. Katiba ambayo inasema watu wote ni sawa
2. Sheria ya Mtoto kifungu cha 5 ambacho kinakataza kubagua watoto
3. Sheria ya Mtoto kifungu cha 10 ambacho kinampa mtoto haki ya "ku-enjoy" mali ya mzazi wake.
4. Mikataba ya kimataifa kuhusu haki za mtoto ambayo Tanzania imeridhia.

Katika majumuisho yake, Mahakama ikasema, "Watoto hawana hatia maana hawachagui kuzaliwa au kwamba watazaliwa wapi. Msemo wa "kitanda hakizai haramu" maana yake ni hakuna watoto haramu. Ila kuna wazazi haramu."

Kwa hiyo mama za watoto wa nje ndoa ndo wakatambuliwa kwamba ni wazazi haramu na hawastahili kurithi mali ya marehemu. Ila watoto wa nje ya ndoa wakaingizwa katika orodha ya warithi, ambayo ilijumuisha na mjane wa marehemu na mama wa marehemu.

Pia ikaonekana mtoto wa ndani ya ndoa kusimamia mirathi hiyo haitakuwa vyema, ikateua Kabidhi Wasii Mkuu (yaani serikali) awe msimamizi.

------------------------------
Kwa kuwa hii ni hukumu-rejea kwa sasa hii ndo tafsiri ya sheria nchini Tanzania, mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo na Mahakama ya Rufaa, au mpaka Bunge litakapotunga sheria tofauti na tafsiri hii ya mahakama.

Je wewe unaonaje? Mahakama iko sahihi, au tuendelee kufuata misimamo ya kidini ambayo inawabagua watoto wa nje ya ndoa na watoto wanaozaliwa kabla ya ndoa?

Hukumu hii inapatikana hapa:[emoji116]

https://tanzlii.org/tz/judgment/hig...me-mwimbe-other-prob-admincause-no50-2016.pdf

Sent from my HUAWEI VNS-L31 using JamiiForums mobile app
Upande wangu mahakama ipo sahihi, navyujua ukishazaa mtoto anakua na nafasi kubwa kushinda
 
Na dondosha swali hapa wabobezi msemi kitu kama sheria inatoa nafasi hawara/mchepuko kushtakiwa kwa kuingilia ndoa ya mke mmoja na mume mmoja iweje bado iwape nafasi watoto wa nje, au pia inawezekana watoto wa nje wakapewa chochote na mama yao akashtakiwa na je adhabu yake inakuaje kwa huyu aliengilia ndoa ya mtu

This makes sense.Wazazi haramu na sio watoto haramu
 
Ndo maana nasema hizi dini Ni UPUMBAVU.

Siamini ata Mungu anaweza kufurahia upumbavu Kama huu.

Mtoto Hana hatia,
hakujizaa Wala kushinikiza kuzaliwa.

Yanini ateseke kwa starehe za wazazi wake.
Unamfokea nani sasa?

Ukiambiwa kuwa wewe ndie MPUMBAVU utajisikiaje?
 
Na dondosha swali hapa wabobezi msemi kitu kama sheria inatoa nafasi hawara/mchepuko kushtakiwa kwa kuingilia ndoa ya mke mmoja na mume mmoja iweje bado iwape nafasi watoto wa nje, au pia inawezekana watoto wa nje wakapewa chochote na mama yao akashtakiwa na je adhabu yake inakuaje kwa huyu aliengilia ndoa ya mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliyeingilia ndoa ya wengine atashtakiwa na atadaiwa fidia na mwenye ndoa.Wakishapatikana watoto ,watoto wana haki kwa baba yao kwani wao hawakuchagua kuzaliwa nje ya ndoa halali.Sheria za Tanzania zinawatambua na kuwapa haki sawa.
 
The funniest part is, huyo mtoto wa nje akiprosper kwenye maisha akawa vizuri, wote (watoto wa ndani ya ndoa na mke halali wa ndoa na baba) wanamgeukia na kuhitaji misaada wakati angekua duni wanamuengua hata kwenye urithi.
 
Tuzae wisely.

Mtoto hujacheza naye, hajakufulia nguo, hujamtuma dukani, n.k anakuja kugawana sawa na wale waliokunywesha dawa ukiwa mgonjwa, kukufulia, kukupikia, kuzungumza nawe daily, kukuchekesha, kukutoa stress n.k
Kwa nyumba ndogo ulikua huendi kuona watoto ama?
 
Na dondosha swali hapa wabobezi msemi kitu kama sheria inatoa nafasi hawara/mchepuko kushtakiwa kwa kuingilia ndoa ya mke mmoja na mume mmoja iweje bado iwape nafasi watoto wa nje, au pia inawezekana watoto wa nje wakapewa chochote na mama yao akashtakiwa na je adhabu yake inakuaje kwa huyu aliengilia ndoa ya mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ameingilia ndoa ama mume katongoza mwanamke nje?

Hv kuna mwanaume anaelazimishwa kuwa na mchepuko?
 
Mimi sio mtaalamu wa haya mambo ila kina rafiki yangu yeye na mme wake ni wakristo na mme kafariki mwaka juzi. Watoto wa mke wa ndoa ni wakubwa wote wana maisha yao halafu kuna kengine mme alizaa nje hat hajafika 10 years. Mme hakuacha wosia. Ila mahakama hawakumpa haki huyyu mtoto wa nje kwa kuwa mke wa ndoa ndio alikuwa main bread winner. Sana sana nyumba ya kijijini kwa baba ake ndio baba ake alijenga ikaamuliwa either iuzwe ili asomeshe au ipangishwe isaidie huyu mtoto wa nje. Lakini zile investments kubwa zote ni jasho la mke wa ndoa so watoto wake wanastahili kufaidi jasho la mama yao.
Yes madam Inawezekana mwanamke akashida, ninavyojua Mimi sheria za TZ, Mali zinazopatikana kwenye ndoa Ni za wanandoa wote.
Kwa kipengele hicho Unaweza ukajitetea kuwa huyo mtoto asirithi hizo Mali, kwa kuwa wanandoa wengi wanafanya vitu kea kusaidiana wote kwa pamoja,
Sasa mwanamke ukiwa unaushahidi wa kutosha ulio hai kabisa Unaweza ukapeleka mahakamani kwa kuonyesha hizo mali na wewe umezichangia kea kiasi chake , ukiwa unaushahidi wa kutosha, kesi Ni rahisi kushida kabisa asilimia miamoja kabisa.
Ndoa maana wanawake wengine wakiamua kujenga maisha pamoja na mumewake anajitahidi kuweka ushahidi Mali hizo yeye kachangia sehemu kubwa, na SI mumewake , ukiwa na ushahidi wa namana hio, vitu wanachukua mwanao kirahisi,
So inategemeana na vieleezo utakavyopeleka mahakamani.
 
MAHAKAMA TANZANIA YASEMA HAKUNA MWANAHARAMU, ILA KUNA WAZAZI HARAMU TU.

Kuna hukumu-rejea ilitolewa tarehe 28/5/2020 na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kupitia Mh. Jaji Mlyambina.

Ni hukumu ya kesi ya mirathi no. 50 ya mwaka 2016 (ina maana kesi ilichukua miaka 4 kwisha).

Ishu ya msingi katika kesi hiyo ni kuna mume wa mtu alifariki bila ya kuacha wosia. Aliacha mke ambaye alikuwa amemuoa kwa ndoa ya kikristo na watoto wa ndoa hiyo, na wengine wa michepuko (nje ya ndoa).

Watoto wa nje ya ndoa wakaweka pingamizi la mirathi maana walikuwa wameenguliwa wasipate kitu na msimamizi wa mirathi hiyo ambaye ni mtoto wa ndoa.

Wakati wa uhai wake, marehemu alikuwa anawasomesha watoto hao (ambapo wengine tayari walikuwa ni watu wazima), vyeti vyao vya kuzaliwa vilikuwa na jina la marehemu kama baba mzazi, na alishawatambulisha kwa mama yake na ndugu zake wengine.

Mahakamani mama na dada wa marehemu walitoa ushahidi kwamba wanawatambua hao watoto kama watoto wa marehemu.

Upande wa wa kwenye ndoa walikataa DNA test kufanyika kupima kama hao ni watoto wa marehemu.

Katika hukumu yake, Mahakama ikatumia sheria zifuatazo:

1. Katiba ambayo inasema watu wote ni sawa
2. Sheria ya Mtoto kifungu cha 5 ambacho kinakataza kubagua watoto
3. Sheria ya Mtoto kifungu cha 10 ambacho kinampa mtoto haki ya "ku-enjoy" mali ya mzazi wake.
4. Mikataba ya kimataifa kuhusu haki za mtoto ambayo Tanzania imeridhia.

Katika majumuisho yake, Mahakama ikasema, "Watoto hawana hatia maana hawachagui kuzaliwa au kwamba watazaliwa wapi. Msemo wa "kitanda hakizai haramu" maana yake ni hakuna watoto haramu. Ila kuna wazazi haramu."

Kwa hiyo mama za watoto wa nje ndoa ndo wakatambuliwa kwamba ni wazazi haramu na hawastahili kurithi mali ya marehemu. Ila watoto wa nje ya ndoa wakaingizwa katika orodha ya warithi, ambayo ilijumuisha na mjane wa marehemu na mama wa marehemu.

Pia ikaonekana mtoto wa ndani ya ndoa kusimamia mirathi hiyo haitakuwa vyema, ikateua Kabidhi Wasii Mkuu (yaani serikali) awe msimamizi.

------------------------------
Kwa kuwa hii ni hukumu-rejea kwa sasa hii ndo tafsiri ya sheria nchini Tanzania, mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo na Mahakama ya Rufaa, au mpaka Bunge litakapotunga sheria tofauti na tafsiri hii ya mahakama.

Je wewe unaonaje? Mahakama iko sahihi, au tuendelee kufuata misimamo ya kidini ambayo inawabagua watoto wa nje ya ndoa na watoto wanaozaliwa kabla ya ndoa?

Hukumu hii inapatikana hapa:[emoji116]

https://tanzlii.org/tz/judgment/hig...me-mwimbe-other-prob-admincause-no50-2016.pdf

Sent from my HUAWEI VNS-L31 using JamiiForums mobile app
Ndio hivyo ilivyo, hasa kama marehemu ali watambua hao watoto.
Ila sasa sheria hiyo haiapply kama familia ni ya kiislamu
 
Tuzae wisely.

Mtoto hujacheza naye, hajakufulia nguo, hujamtuma dukani, n.k anakuja kugawana sawa na wale waliokunywesha dawa ukiwa mgonjwa, kukufulia, kukupikia, kuzungumza nawe daily, kukuchekesha, kukutoa stress n.k
Tena huyu anapaswa kupata zaidi kwani angalau wenzake walipata mengi kwa kukaa karibu na wazazi, fanya starehe zako kwa utaratibu.
 
Sheria za dini yetu hazina reform ndugu. Wenyewe tumeridhika nazo.
Kwenye nchi hii Sheria za dini zipo chini ya Sheria za nchi. Haiwezekani mtu azae hovyo hovyo ikifika kwenye mirathi akimbilie kichaka cha dini.Wakati akizini hakuwa na Sheria ya dini? na hao watoto anataka waishi vipi?
 
Huo mfano wako hauingii hapo kwa sababu nimeshasema issue sio marehemu kuwa Mwislamu, na ndo maana nikasema kabla ya kutumika sheria ya Kiislamu, mahakama inatakiwa kujiridhisha ikiwa marehemu alikuwa Mwislamu anayeuishi Uislamu alikuwa ni Mwislamu Jina tu na kwahiyo kuna watu wanataka kutumia kete ya Uislamu ili kuwatupa wengine nje!!

Huo mfano wako haujitoshelezi kwa sababu ulitakiwa kuonesha marehemu alikuwa ni mwislamu aliyekuwa anaishi kwenye misingi ya Uislamu na sio just because he's a muslim! Lakini kwa upande mwingine, pia ulitakiwa kueleza sheria za mirathi nchini Kenya zinasemaje kwa sababu Tanzania kuna sheria za aina tatu zinatumika ambazo ni sheria ya serikali/secular law, sheria ya kimila na sheria ya kiislamu!!
Hapa tumepigwa kamba. Serikali ichunguze marehemu kama aliuishi uislamu kweli?? Anauishije kweli wakati kazaa nje ya ndoa.
 
Bahati nzuri sheria zetu za dini zinasema mtoto aliezaliwa nje ya ndoa halali (mwanaharamu) huyo ni mtoto wa mama yake na harithi chochote kwa baba.
Labda kwa dini ya ushia, ila Kauli hii haina dalili kabisa kusema kwamba mtoto wa nje ya ndoa ni wa mama.
Haina dalili kabisa katika uislamu.

Mtoto wa nje ya ndoa ni wa baba ikiwa baba yake atamkubali asipomkubali atajinasibisha na babu yake mzaa mama na hii ndio Kauli yenye nguvu upande wa pili wa khilaf hauna nguvu na wala hakuna dalili.
 
Bahati nzuri sheria zetu za dini zinasema mtoto aliezaliwa nje ya ndoa halali (mwanaharamu) huyo ni mtoto wa mama yake na harithi chochote kwa baba.
Huku ni kumnyima mtoto haki yake kutoka kwa baba yake.
 
Back
Top Bottom