Habari wadau.
Kama mnavyojua suala la mirathi linavyotolewa macho hapa Tanzania.
Jirani kwetu kuna mama amefariki na kuacha nyumba nzuri tu na hajaacha mtoto hata mmoja.
Historia ya huyu mama (kabila mpogoro) mwaka 1991 aliolewa kwa ndoa ya kanisani na mume wake (kabila mchaga)
Baada ya kufunga ndoa walinunua kiwanja na mume wake na kuzaa mtoto mmoja wa kiume.
Mwaka 1994 mume wa huyu mama alifariki na kumuacha mke na mtoto mmoja wakiwa hai.
Taratibu za mirathi ya mume wake zilifanyika baada ya msiba. Mama na huyo mwanae wakapewa hiko kiwanja maeneo ya tegeta kikiwa kitupu hakijaanzwa ujenzi wowote.
Maisha yakaendelea. Mama huyu hakuolewa tena . Aliendelea kuishi na mwanae kwa kupanga nyumba ya NHC keko. Na mdogo mdogo akaanza ujenzi wa nyumba katika kiwanja walichoachiwa na mumewe.
Alijenga nyumba nzuri tu ya kisasa. Na zingine ndogo ndogo pembeni za kupangisha. Maana kiwanja kilikuwa kikubwa sana (maana enzi wananunua tegeta ilikuwa pori ardhi haina thamani miaka ya 90 muuzaji anakuuzia bonge la kiwanja kwa bei ndogoo)
Baada ya kumaliza ujenzi yeye na mwanae waliendelea kuishi nyumba ya NHC na kule tegeta walipojenga wakapangisha wapangaji kadhaa.
Mwaka 2015 mama alipata msiba mwingine wa kufiwa na mtoto wake huyo mmoja kwa ajali ya gari na hii ikamfanya mama kubaki peke yake bila mtoto wala mume.
Mama akaendelea kuishi mwenyewe mpaka na yeye mama alipofariki mwaka huu mwanzoni.
Mwili wa mama ulisafirishwa kwenda moshi kuzikwa walipozikwa mume wake na mwanae.
Shida imekuja kwenye nyumba zilizojengwa na huyo mama. Ukoo wa mume unasema ni mali zao. Na ukoo wa mke nao unasema ni mali zao maana zimejengwa kipindi mume wa huyo mama ameshafariki.
Wataalamu wa mirathi Kesi kama hii upande upi kati ya ukoo wa mume na ukoo wa mume una haki ya kurithi hizo mali za huyu mama.
Wazazi wa huyu mama wote wameshafariki pia.