Mirathi ya nyumba iliyojengwa na mjane yazua balaa; ukoo wa mume na ukoo wa mke wanaigombania

Mirathi ya nyumba iliyojengwa na mjane yazua balaa; ukoo wa mume na ukoo wa mke wanaigombania

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa, mali inayopatikana KATIKA ndoa ni mali ya wanandoa-ni marital property. Hata mtu ujifanye unajenga kisirisiri. Ukifa ikajulikana hiyo nyumba au mali inakuwa ya mwenzako aliyebaki hai. Hata mkeo akihongwa ujue pesa au mali aliyohogwa ni yenu ninyi nyote wawili katika ndoa. Na mume wa mtu ukihonga ujue umemfanya hata mkeo akahonga😀

Kwa kesi ya huyu mama mali aliyopata baada ya mume kufa nadhani ni yake yeye peke yake, maana ndoa ilivunjwa na kifo, hivyo ndugu zake wana haki juu ya mali hiyo.
Ikiwa kuna mali walipata pamoja na mumewe, ni mali ya wanandoa....hivyo ndugu zao wote (nadhani hasa wazazi wao pande zote mbili) wana haki kwa mali hiyo.
Uko sahihi
 
Hapo hakuna cha malezi wala mchango,nyumba ni ya mwanamke aliyefariki hao ndugu wa mme wanahusika vipi hapo?ndugu wa huyo mke aliyekufa ndio wenye mamlaka na hiyo nyumba very simple

Hati ya Kiwanja ina jina la marehemu mume. Maana mama alipewa kwenye mirathi ya mume wake
 
Mambo ya kuzika na nyumba kuna uhusiano gani?sioni mantiki yoyote hapo

Kigezo kilichofanya akazikwa mahali Fulani ndio vigezo hivyohivyo vitakavyowapa umiliki hao wanaomiliki eneo Kaburi lake lilipo.

Unasema huoni mantiki, hujiulizi Kwa nini alizikwa Huko?
 
Kwa mila na desturi za kichaga Mali zinaenda kwa ukoo ,Kama huyo mwanamke kazikwa ukooni uchagani tayari huyo alikuwa familia nyingine
 
hapo ni kuuzwa kisha wagawe mafungu mawili,upande wa mume wapate na mke pia wapate
 
Kiwanja alinunua mume enzi za uhai wake. Na kwenye mirathi ya mume hiko kiwanja alipewa mtoto wa huyo mama ambae ni ukoo wao pia. Ameshafariki wamezika kwao.
Hiyo inaamuliwa na wa kijana wa kiume,Kama anakaka yake wa baba mdogo ndiye mrithi,ndivyo wachaga tunafanya Mambo kwa taratibu,
 
Hiyo inaamuliwa na wa kijana wa kiume,Kama anakaka yake wa baba mdogo ndiye mrithi,ndivyo wachaga tunafanya Mambo kwa taratibu,

Mtoto aliepewa kiwanja kwenye mirathi ya baba yake alitangulia kufa kabla ya mama yake. Baada ya mtoto kufa mwaka 2015 maana yake mali zote za mtoto zilirudi kwa mama yake aliyebaki pekee
 
Na ndio umuhimu wa kuandika mirathi. Huyo mama baada ya kufiwa na mwanae alipaswa aandike wosia.
Kwa hapa wazazi wa pande zote wanapata mgao wa mali sawia
 
Kazi kwelikweli. Je hao ndugu wa mwanamke hawana hata chembe ya aibu ?? Bado wanadai mahari au mwanamke hakulipiwa mahari ?
Ungejaribu kufafanua kidogo utata uliopo hapo, kumbuka hao wote ni "third parties"

Kama issue ni mahari nafikiri alielipa ni mume, ambaye ni marehem pia.
 
Uhalali upo sababu mume alitoa mahari na pia mwanae kazikwa hapo. Mfumo mnaoutetea ulishapitwa na wakati.
Hakuna uhalali. Nadhiri ya ndoa ya kikristo inasema mpaka kifo kitakapowatenga. Hivyo mojawapo anapofariki na mirathi yake ikakamilishwa, anayebaki ni single na mali zake zinawahusu watoto au ndugu zake wa karibu. Je angeolewa halafu ndo amefariki mume wake mpya si angerithi hizo mali? Huu ndio uelewa wangu.
 
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa, mali inayopatikana KATIKA ndoa ni mali ya wanandoa-ni marital property. Hata mtu ujifanye unajenga kisirisiri. Ukifa ikajulikana hiyo nyumba au mali inakuwa ya mwenzako aliyebaki hai. Hata mkeo akihongwa ujue pesa au mali aliyohogwa ni yenu ninyi nyote wawili katika ndoa. Na mume wa mtu ukihonga ujue umemfanya hata mkeo akahonga😀

Kwa kesi ya huyu mama mali aliyopata baada ya mume kufa nadhani ni yake yeye peke yake, maana ndoa ilivunjwa na kifo, hivyo ndugu zake wana haki juu ya mali hiyo.
Ikiwa kuna mali walipata pamoja na mumewe, ni mali ya wanandoa....hivyo ndugu zao wote (nadhani hasa wazazi wao pande zote mbili) wana haki kwa mali hiyo.
Hapo ina make sense!
Lakini historia inaonesha wazazi wote washadanja!
Sasa hapo inakuwaje?
 
Ni kwamba ndugu wa mume hawahusikia maana ndoa ilishavunjwa na alishakufa mume..Mali zilishakuwa transfered kwa upande wa mke kama kiwanja ni Mali ya mke kwa kuachiwa na mumewe yeye akajenga bila msaada wa Mume alikuwa marehemu

Hao ndugu wa mume wanatokea wapi kama sio Tamaa?
Imagine huyo mama angekufa akiwa kaolewa na mtu mwingi izo Mali zingeenda hata kwa huyo Mume wake mpya..yule marehemu hana chake kwanza hakuacha nyumba.
Hii statement inaingia akilini.
 
Back
Top Bottom