Sio Utapeli.
Kama MKE kazikwa upande wa mume, tafsiri yake bado ni Mali ya Ukoo wa mumewe.
Kama Ndoa ilivunjika au ilivunjwa, sio sababu ya kuzika MKE upande wa mumewe.
Hao Ndugu wa Mke ndio wanashida.
Sema ni vile Watu hawaelewi haya Mambo.
Mwanamke akishaolewa anakuwa hayupo Chini ya umiliki WA ukoo wake tena, anaenda kwenye umiliki wa ukoo WA mwanaume.
Ni vile kizazi cha sasa kimeshavurugwa
1.Kuzika marehemu siyo kigezo au sababu ya kuwa na uhalali wa kisheria wa kurithi mali za marehemu uliyemzika.
2.Sheria ya Mirathi inawatambua warithi halali ni (i) Mjane (ii) Watoto wa Marehemu (iii) Wazazi wa Marehemu.
Endapo kama wote hawa hawapo, basi, ndugu zake wa karibu ndio wanaofuata kuwa warithi halali. Ndugu hao ni kama vile dada zake wa damu, kaka zake wa damu, n.k.
3. Kwa kuwa mume wa huyo mama marehemu alitangulia kufa, kisheria hali hiyo inajulikana kama "kaukimbia urithi" kwenye mali/ardhi inayomilikiwa kwa umiliki wa maslahi ya pamoja yasiyogawanyika (joint occupation or matrimonial property ownership), hivyo, ndugu wa huyo mume hawana haki yoyote ile kwenye hizo mali/nyumba kwani ndugu yao alijitoa mapema kwenye umiliki wa hiyo nyumba na kisha umiliki huo wote kuhamia kwa mkewe na mtoto waliobaki hai.
4. Ndugu wa huyo mama wanapaswa kufungua kesi ya mirathi ya usimamizi wa mali za huyo mama na wamteue msimamizi wa mirathi, hao ndugu wa mume wa marehemu endapo kama watakuwa na pingamizi lolote basi watawasilisha huko Mahakamani, na kwa vyovyote vile pingamizi hilo lazima litakosa mashiko na litatupiliwa mbali na Mahakama.
5.Mwisho.
Mali na nyumba zote za huyo mjane ni urithi halali kwa ndugu zake, ndugu wa mumewe hawana haki ya kurithi mali hizo.