Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Achana na lile vibe la msiba la waombolezaji, kwikwi na vilio vya chinichini, simanzi na majonzi wakati wa ibada.. Hayo mambo jana hayakuonekana kabisa
Kilichoonekana jana ni mambo ya kutisha sana
Ukimya usio wa kawaida
Hofu ya dhahiri nyusoni
Taswira zilizohamanika na kukosa utulivu kabisa
Kutojiamini kulikopitiliza
Watu waliokaa kwa machale
Nyuso zilizofubaa na kusawajika vilivyo
Mwonekano wa uchovu na kukosa usingizi kwa muda mrefu
Ulinzi mkubwa wa askari kanzu na wana usalama!
Tension ilikuwa kubwa sana na hata waliowekwa 'kimkakati' Wake pamoja walishindwa kabisa kuangaliana na kunong'onezana mawili matatu.. Kila mmoja akimuona mwenzake ni kero na kujitahidi kugeuza shingo pembeni kadiri awezavyo
Eye contacts zilikuwa adimu sana jana!
Kwenye misiba kama hiyo kuna prominent figures ambazo huwa na sehemu zao maalum na huwa kuna positive energies huwatambulisha hata kama ni msibani
Jana watu walifichwa/ walijificha pengine kwa sababu maalum! Ile sense of authority haikuwepo kabisa!
Misiba hukutanisha watu na kuna watu husahau majonzi na kusalimiana kwa tabasamu na kuongea machache kwa sauti za chinichini.. Jana waombolezaji walikuwa kama mazombi na kila mmoja akiwa na hofu ya kunyanyua kinywa chake! Niliogopa sana
Nyuso nyingi zilibeba mashaka na wasiwasi badala ya huzuni na majonzi.. Ule haukuwa ukimya wa msiba bali taharuhi ya hofu ya mengi.. Macho yanaongea na tuliyaona jana yakiongea
Hiyo ndio hali ilivyo nchini kwasasa kwa upande wao! Hawana furaha, na wametawaliwa na mashaka huku kiwango cha kutoaminiana kikiwa kimeongezeka maradufu
Kama angekuwepo mtoto mdogo jana anayechezea futuza kisha akalipasua.. Majeruhi wangekuwa wengi na pengine hata vifo!
Ukiwa na ukimya wa jana umetufunulia jambo moja kubwa sana! Hakuko shwari!