Misafara ya viongozi inaleta usumbufu usio wa lazima

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Japo naheshimu usalama wa viongozi kuwa kipaumbe ilinwahakikishiwe usalama maana wanapatikana Kwa gharama na Kuna ugumu kuwapata wengine

Leo nipo Mwanza Kuna foleni na usumbufu mkubwa barabara ya Buswelu kupitia Saba Saba,
Magari yamesimama masaa 3

Sijui Kuna kiongozi gani yupo Mwanza? Askari wametanda magari yamezuiliwa muda mrefu

Hawa Askari wangefanya shughuli zingine za kuzuia uhalifu kuliko kumlinda kiongozi mmoja

Hili linasababisha usumbufu Kwa wananchi wanawahi kupiganisha ili kupata ugali wa watoto

Kiongozi hawezi Kulala njaa wala familia yake, kwanini mlete usumbufu Kwa raia wengine

Nashauri viongozi watumie helicopter ili watue kwenye destination zao bila huu usumbufu
Au mnataka kulazimisha wananchi wajue kuwa kiongozi Fulani yupo
 
Poleni
Huyo atakuwa Naibu PM akitokea Bunda kimstiri ndugu yetu DG wa TANESCO, Kuweni na subira
 
Ungekua Dar Nyerere road sijui ungesemaje mhaya wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…