Hii misafara aisee acha tu kuna siku nilipewa adhabu ya kimya kimya ila nilishika adabu,kulikuwa na msafara nikaegesha garimsafara upite nikaanza kuufukuzia nyuma kwa kasi ili niepuke jam za barabara kwa advantage ya huo msafara kufika kama kilometa moja gari lililokuwa mwisho wa msafara likakaa pembeni kidogo likapunguza mwendo kabisa nikalipita akaanza kunifuata nyuma kwa spidi ya hatari nikajua kimewaka nikiwasha indicator ananibana nisikate ikabidi ninyooshe nao wanapokwenda nilitokea moshi nikapelekwa hadi karibia na makuyuni mafuta yakaniishia na mie nilikuwa naishia bomang'ombe ,jamaa wakajua adhabu inanitosha baada ya kuona gari kama inamiss miss wakajua ni wese hilo limekata ndiyo wakanipita ,sitakaa nisahau lile tukio maisha