Misamiati maarufu vyuo vikuu

Mkuu, bila shaka umepitia pale musoma tech maeneo ya baruti kwa Bry, safi sana.

Nadhani pia utakumbuka samaki wa kukaangwa wa mafuta ya Mara Oil pale Nyarusurya! Vp waloko pale jikoni sijui kama bado wapo!
 
'Lampad' kukaa mda bila kula,imeitwa lampad coz anamashuti marefu.
 
Kuflongo- Kumpa lecturer penzi ili akupe maksi za upendeleo.
Kupigwa mkanda- Lecturer kutolewa nje penzi na denti wa kike.
Kuliwa sugu- Kupigwa mashine na walimu tofauti kwa wakati tofauti

heh! kweli mie mzee! enzi zetu tulisemaga tu maksi za chupi! ila nimecheka!
 
kupiga 4,4,2=kuangaliziana kwenye pepa au test!
kuingia na handout=kuingia namakaratasi yamajibu kwenye mtihani!
 
KD au VD pale mlimani ilikuwa Kiwango au Viwango duni wale wanaoingia chuo kwa pre-entry
 
-Shato pori-kutembea kwa miguu toka chuo hadi mabibo(udsm)
-RB-wali maharage
 
Wireless-desa liloloandikwa kwa kutumia kalamu isiyokuwa na wino kwenye plane, anayejua kilichoandikwa ni aliyeandika tu.

Hii kitu nasikia ilikua ikitumiwa na wanafunzi wa sheria ambao uwa wanaruhusiwa kuingia kwenye mitihani na references za aina fulani!
 
shake well before use - kujisomea/kukariri few minutes kabla ya kuingia kwenye mtihani!
 
Mabwenga - wahaya wa kiume, ambao wengi wao walikua wana akili sana na pia kwa kupenda ngono walikua hawajambo...usemi wa UCLAS sana na UD-Mlimani kidogo.
 
Kontena jipya - wanafunzi wa mwaka wa kwanza.(hasa wa kike)
 
Nadhani pia utakumbuka samaki wa kukaangwa wa mafuta ya Mara Oil pale Nyarusurya! Vp waloko pale jikoni sijui kama bado wapo!

Yes! Tulikula sana samaki tena walikua wanatoka kiwanda cha 'Mazara'. Kuhusu waloko sijui kama wapo mpaka sasa ila nawakumbuka pia wapishi wa jikoni miaka ile kama mzee Matogoro, mzee Sabato na mama Helena.
Mzee we pande zipi kwa sasa huenda tulikua bweni/darasa moja!
 
Sulvan Summit - kipindi cha kufanya sapu..
Triangle- Kufanya mambo matatu 1.Kwenda Lecture 2.Kwenda bweni 3. Library
 
kimfaacho mtu chake-kuingia na nondo kwenye mtihani

Face book - mbele ya ofisi ya dean of student pale RUCO IRINGA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…