Misemo kama ya aina hii inafaa kufutwa

"Mficha uchi hazai" hii methali imesababisha dada zetu kuvaa nguo za ajabu ajabu ilimradi wasiwe wagumba.
Misingi ya misemo ya zamani ya wazee wetu ilikuwa ni kukumea maovu, kuamrisha mema, na ukiona misemo kama hii ujue inazungumziwa kwa munasaba wa ndoa kwa maana ya kuchelewa chelewa kwani wao hawakuamini juu ya watoto wa nje ya ndoa.
 
mkianza kuchukulia hii misemo kama ilivyo mtaumia sana, hakuna kitu ya kufutwa hapa kila msemo unaweza kudadavuliwa kwa namna yake au mazingira husika.
 
Hapo mimi naona utata unauleta wew mtoa mada ila hiyo tungo sio tata.

Na utata wa tungo haimaanishi kuwa inapotosha jamii,naona unachanganya kuaminisha umma kuwa unachoamini ni sahihi.

Na ndio sababu haijawekwa maana moja kwa moja ili kila mtu atoe maana.leo ukiambiwa mtu ana mkono wa birika utahoji ni vipi mtu ana mkono uliojikunja,hutoishia hapo utahoji pia kuku anawezaje kutagia mibani....
 
"Mficha uchi hazai" hii methali imesababisha dada zetu kuvaa nguo za ajabu ajabu ilimradi wasiwe wagumba.
Hizi methali zote zina maana sana tu,,nadhani babu zetu wikuwa ni genus.. Hyo maana ya mficha uchi hazai sivyo Kama unavyofikiria wewe,, methali nyingi zinafanana ,,au zinapingana ili kukupa changamoto,,na zote zina maana,,mfano mficha uchi hazai,,na mficha maradhi kifo humuumbua,,zote ni maana moja,,kwamba ukificha tatizo mwisho wa siku ni tatizo kubwa zaidi,,au ukificha tatizo utasaidiwaje na wengine?eleza matatizo yako usaidiwe..hyo ndy maana,,unapaswa utafakari kwa kina maana hizi,,
 


Niwatake radhi kwa kosa lipi??!!.

Kuongea kiswahili sio tiketi kwamba wajua kiswahili au wewe ni mswahili.

Misemo yenye maana katika lugha ni ile inayoakisi uhalisia wa jambo lenyewe, mfano ukisema; "Fimbo ya mbali haiui nyoka" maana yake fimbo iliyo jirani nawe ndio yakupasa uitumie kuuia nyoka kabla hujaenda kuchukua fimbo ya mbali, huo ndio uhalisia wa msemo/ methali hiyo, kitamathali unaweza kusema hivi; Fimbo ni mwanamume aliyekaribu (mahali anapoishi) na Nyoka ni mwanamke hivyo mwanaume aliyekaribu na mwanamke ndiye anayeweza "kupata mzigo" kuliko mwanamme aliyekuwepo mbali.

Sasa tuje kwenye uhalisia wa msemo; Mpe mchawi alee mtoto, Swali wewe unaweza kumpa mchawi alee mtoto wako???!!.

Lazima ujue kwamba misemo/methali lazima kwanza zijengwe kwenye uhalisia ndipo baadaye zije tafsiri zingine, kama uhalisia ni hovyo basi msemo nao unakuwa wa hovyo na haufai kuwepo katika lugha ya watu wastaarabu wenye hekima, Kiswahili ni lugha ya watu wenye hekima.
 
Utasikua hata mtu mkubwa kabisa serikalini anasema wapinzania wanapaswa kuuwawa.
 
Mnyonge mnyongeni inatumiwa sana awamu inayojinasibu kutetea wanyonge. Wananyongwa mchana kweupe. Haki yao wataipata makaburini.
 
Utakuwa huzielewi maana za hizo methali/misemo. Tafuta maana yake halafu urudi hapa
 
Mchawi mpe mwana alee- katika jamii kama wengi mmekubaliana jambo mmoja mmemtambua anakubali kinafiki ndio afanywe kuwa kinara.

Mfano ; mmepanga kujitolea kuchimba mtaro mtaani mmoja mnamuona anakubali kinafiki , yy huyo ndo mnamkabidhi sululu.

Mnyonge ,mnyongeni lkn haki yake apewe!- jamii iache dhulma, mwanajamii bila kujali hadhi yake akikosa aadhibiwe, akiwa hana kosa apewe stahiki yake.

Wahenga hakuna walichoacha ! Misemo ya sasa ndo ya MATEJA.
 
Kuna kipindi nilipotoka chuo na kurudi home mzee alisema maneno huku akinikabidhi duka lake ili niliendeshe

Mwanzo sikujua maana yake ila nilipoanza kushika shika viela vya pale zote zikawa zinaishia kwny anasa

Mzee alipoona hvy ilibidi nikabidhi funguo nikapauka sana

Kweli " MPE mchawi mwanao amlee"

Hapo duka ndio lilikua mtoto kwakua nilikua mchawi nikaa kuliroga..
 


Hao wanaopinga wakisoma maelezo yako nadhani watanielewa. 🤣
 
Ndugu yangu asante sana. Maelezo yako yanaonyesha umebobea kwenye hii fani. Kwa kifupi yanaelimisha sana. Mimi nadhani misemo na methali nyingi hazipitwi na wakati (naomba nisieleke kuwa napinga kuna mingine inapitwa). Hebu tuchukulie msemo kama ''haraka haraka haina baraka''. Huu msemo haiuhimizi watu wasifanye mambo kwa haraka kama wengi wanavyodhani. Huu msemo unahimiza watu kuwa na ustahamilivu kwa mambo yanahitaji muda kufikia lengo lake. Unawataka watu wasifanye short-cut kwa mambo yanahitaji process ndefu ili kufikia lengo. Hata hiyo mifano aliyotoa mwanzisha thread bado ina mantiki na mafunzo mazuri tu kwa jamii. Ila naona jamaa yeye anatafsiri kama ilivyo ndiyo maana anaona haifai. Misemo ya kupiga vita ni kama hii ya wanasiasa wa siku hizi wanayosema eg ''mheshimiwa ukiona inakupendeza.........''.
 
Asante sana sana kwa elimu. Mwanzisha thread yeye anaichukulia misemo kama ilivyo. Hivi siku hizi somo la lugha limeondolewa jamani?
 
"Mficha uchi hazai" hii methali imesababisha dada zetu kuvaa nguo za ajabu ajabu ilimradi wasiwe wagumba.
Hiyo ni tafsiri yako lakini msemo hauna nia ya kuhimiza watu wafanye ngono. Fasihi haifundishwi tena siku hizi?
 




Mkuu labda utakuwa hujanielewa vyema, nasema hivi; Msemo au methali kimsingi lazima kwanza iwe na maana ya moja kwa moja (literal sense) na baada ya hapo ndipo maana zingine hufuata, umetoa mfano wa; "Haraka haraka haina baraka" na ukatolea ufafanuzi na mimi naafiki ufafanuzi wako lakini maelezo yako yanaendana na uhalisia wa huo msemo yaani hakuna contradiction hapo na mimi sina shida na misemo ya aina hiyo ambayo uhalisia wake unaendana na tafsiri yake (intrepretation).

Shida ipo kwenye uhalisia wa; "Mpe mchawi amlee mwanao" je, tunaweza kupata tafsiri yake inayoendana na uhalisia wake?? (literal). Uhalisia ni kumpeleka mtoto wako kwa mchawi ili amlee, je unaweza??!.

Tafsiri na uhalisia ni muhimu vikubaliane/viendane ndipo msemo unakuwa na maana ya kimantiki.

Na huo ndio uzuri na utamu wa lugha, lugha ikiwa na maneno yasiyo na mantiki hiyo ni lugha mbovu.

Tujenge Kiswahili chetu tusikibomoe.
 
Asante sana. Una uelewa mpana sana kwenye hii fani.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…