Misemo kutokana na Vichwa vya Treni

Misemo kutokana na Vichwa vya Treni

Joined
Dec 16, 2016
Posts
18
Reaction score
48
IMG_20170706_210614.png

[HASHTAG]#Andiko[/HASHTAG]
'Basi vikashushwa vichwa vya Treni toka mbinguni kupitia baharini, mfalme akataajabu kwa baraka za mungu' Watanzania 6:18 = Bafaraj

nao makada na wapambe wakararua mavazi yao kwa Shangwe wakisema "utukufu huu uwe wa milele" Kupagawa 2 23-26!

"Watu wakasujudu na wakasema Mfalme umenena.Neno lako ndio letu, matakwa yako ndio yetu...tupeleke tunatii..bila ya pingamizi"...Wapofu 23:3

Nao mafarisayo walipoishaisikia amri Kuu ya kusulubu, wakajawa kiburi wakipiga na kukamata wenye akili timamu wasiosujudu Hatamu 4:26

"Nami nikaiangalia Kolomije, palipo njia Kuu kwenda Chato nikamuona yule aliye mwana wa mfalme akiamrisha kusulubu Wahangaika" Kilio 1:1

"Tukaitizama nchi kwa juu, busara ikasema tuingie ndani na kuona mchwa wamekula kila kitu...Kolomije ituokoe sote. Tuombe" ...Ufunuzi 43:5

"Mimi na Utawala wangu tutawanyoosha mnyooke" asema Bwana. Nalo neno hili likawaogopesha sana wadanganyika unyonge ukawajaa. Utumwa 15:20

Mfalme akatamalaki woga ukawajaa watawaliwa siku zile. Nao walionywa ole wake athubutuye kufumbua makanwa yake lisije mkuta jambo. Utumwa 16
 
"Basi Neema Ikaja Katika Nchi Ile Ndipo Vichwa Vya Treni Vikashushwa kando Ya Bahari, Maana Reli Ilikuwa Inajengwa Wakuu Na Watu Wake Wa Nchi Ile Wakastaajabu Wakisema Haleluya Haleluya Bwana Ametubariki." Tanganyika 5:42-44
 
Ndipo waDanganyika wote walipoinua macho yao mbinguni na kusema "Amina, na aihimidiwe Bwana Mungu wetu, milele na milele. Na huyu mfalme mtumishi wake atutawale mpaka itakaposhuka Boeing Dreamliner 787 kwa mtindo wa vichwa vya treni. Amina." (Chato 13:3-7)
 
Back
Top Bottom