Misemo maarufu zaidi ya Yesu

......big up mtoa mada nimejisikia kubarikiwa na hii thread yako imekaa kitofauti, ni kweli hiyo misemo ni maarufu sana Kwa wasoma bible, pia kuna ile Yesu aliwazingua wazazi wake walipoenda kumtafuta akawaambia kwamba 'hamjui kuwa yanipasa kuwamo kwenye nyumba ya baba yangu' ikabidi wazazi wawe wanashagaa tu, sikumbuki ni kitabu gani na mstari wa ngapi.....
 


Haya si maneno ya Yesu

Yohana 3:16
[16]Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Yohana 3:5
[5]Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Yohana 8:7
[7]Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
 

Mathayo 5:28 SRUV​

lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
 
Malaki 2;16
Maana Mimi nakuchukia kuachana asema Bwana Mungu wa Israeli
 
Yesu ni mwana wa Mungu aliye hai,kumbuka akiwa duniani aliuvaa ubinadamu hivyo mwili ulizidiwa maumivu makali hadi kitamka hivyo.
1 Wakorintho 1:25 NEN

Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu.



Na huu pia ni msemo wake?
 
Rafiki yetu Lazaro amelala usingizi, lakini ninasafiri kwenda huko ili kumwamsha
 
Yohana 14:28
Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.

1Korintho 15:28
Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana(Yesu) mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
 
Yohana 15:1
Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

Mathayo 26:29
Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

Damu mpya aliyosema Yesu tunaikuta[emoji1484]

Ufunuo 11:6
Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.
 
Waacheni wafu wakazike wafu wao

 
Mathayo 19:26 "Yesu akawakazia macho, akawaambia kwa wanadamu hilo haliwezekani, bali kwa MUNGU yote yawezekana"
 
U na hakika hiyo namba moja alitamka Yesu?
 
Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, hukaa ndani yangu na mimi hukaa ndani yake
 
Mathayo 24:22
“Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.”

Siku zenyewe ziko:-

Ufunuo 20:6
Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu Baba na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
 
Wewe wasema.
Mimi ndimi.
Usiogope.
Nifuate.
Imeandikwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…